SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Katika hoja hii ukweli upo kwa asilimia furani, kwamba ugali unachangia ufahamu kuwa finyu. Siyo ugali tu hata mikate hii mweupe, na hata chai ya rangi pia.
Ugali wa mahindi hasa hizi sembe, mikate mweupe, yaani ngano iliyo kobolewa, majani ya chai, maharage, vyote hivi vina asili furani ya ulevi. Kama unabisha kula ugali wa sembe na maharage, lazima ndani ya dakika furani kunauchovu unaupa.

Kunywa chai ya rangi na mkate, nakuhakikisha kuna uchovu lazima utaupa. Kwa kifupi huo uchovu ndiyo unadumaza ufinyu wa kufikili.

Ndiyo maana tunashauliwa tule matunda na mboga mboga za majani kila wakati, angalau kuupa ufahamu nguvu.

Tuelewe kitu chochote kinacho leta ulevi/uchovu huwa ni adui wa ufahamu. Ndiyo maana tukifanya kazi tukachoka inabidi tupumzike kwa muda furani ili kuupa ufahamu nguvu tena.

Baadhi ya nchi zilizo endelea hazili kabisa ugali na vyakula ambavyo hupelekea kulegeza ufahamu.
Mfano kwa Africa ni Nigeria & Ghana, hizi nchi ni nadra kukuta mtu anakula Ugali wa mahindi, na kama ukiukuta ugali wao lazima kuna vitu wamevichanganya ili kufanya ugali huo kutokufanya ufahamu uchoke.
Ndiyo maana Nigeria inaogopeka sana duniani kote, maana watu wao wanaakili nyingi mno.

Kwa Africa bado tunahitaji elimu ya chakula ili tuweze kujenga afya za fahamu na miili yetu.
Mtu mwenye afya njema si yule aliye nenepa bali mwenye ufahamu wa kufikili haraka.
 

Ati Afrika tunahitaji elimu ya Chakula.
Una matatizo sehemu. Kwasababu....unataka kulazimisha madai ambayo tayari yalishwa tolewa ufafanuzi; Ulaji Ugali haudumazi akili.
Sijui ulikula nini kuja kuyasema hayo uliyoyasema. Baga?
 
Mimi hula ugali sana na sidhani kama kweli akili yangu imedumaa. Aaliyeleta madai hayo tuje tupimwe IQ zetu kama yeye atakuwa na IQ kubwa kuliko mimi. Mimi ni shabiki wa jamaa huyu

View attachment 2638430
Muinjilisti na mhubiri Lemma wa CHADEMA ndiye aliyenukuliwa. Hatahivyo, kuna genge lililo shikilia bango suala hili kwa lengo la kufedhehesha tu. Shaming. Ni lugha ya wakimbari. Racist and Bigoted.
Watashindwa na walegeee!
 
kitu cha TMK hakijawahi kuwaacha watu salama yaani watu ugali unaleta udumavu ooooohhhh NOOOOOO uongo kabisaaa
 
Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli

Ugali ni mlo hatari ni kama sumu ndio maana hata wanyama wachoyo kama mbwa, nguruwe, paka, nk. Hawana akili lakini katu huwakuti wakila ugali maana ni chakula kisicho na nutrients zozote mwilini.

Hapa Tanzania jamii na makabila makabila makubwa hatupendelei ugali mfano sisi watu wa mkoa wa Kagera, Moshi(wachaga) na Mbeya hawali ugali lakini Tanzama mikoa duni kama Dodoma, Singida, Lindi, na watu wa Pwani wala ugali

Wenzetu wamataifa mengine wana afya afya na wala hawajui ugali ni nini Tazama wenzetu kutoka west Africa hawali maugali kama Watanganyika wana body zimejengeka.

Waganda, Wakenya, Wanyarwandwa hawali ugali. Mtu ukila ugali kwanza unalewa kama umepiga jibapa la Konyagi masaa mawili, ukila ugali wa Mara digestion ni ngumu mwilini chakula hakushuki hupati choo siku mbili, sasa hicho chakula au uchafu tu.

Wazungu na warabu wako vizuri kiafya wala hawayajui maugali ni nini wao wanajilia ngano, wali, nyama na maziwa, sisi Watanganyika kutwa usiku tunakula maugali na milenda kama tumerogwa

Madhara ya ugali kwa watu wetu, tumekosa washiriki wazuri kwenye michezo yani leo umpeleke Kibwana amkabe Sadio Mane AFCON haiwezekani.

Watoto hawana akili mashuleni wapo tu wamechoka yaani wamelewa chakali shuleni hawaewi kisa kula maugali.

Miili kama midogo kama digidigi unakuta mwanaume Dar anavamiwa na panya road anajificha kisa kula maugali

Sipendi ugali nakushauri usije ukala haya sumu ya akili na mwili ugali ni sumu kali

Nikiwa Rais nitapiga marufuku ugali

#kataa ugali Mtanganyika
 
Na ukisoma historia zinadia kuwa kabla ya wakoloni kuja Afrika, Afrika haikuwa na utamaduni wa kula ugali.

Kwa hiyo ujio wa wakaloni ndio mwanzo wa ugali.

Kabla ya wakoloni Afrika ilikuwa na wazee timamu sana kwenye kichwa ila hayo yote yalikuja ku change ghafla baada ya ugali kuwasili.

Ukifanya tafakuri ya kina utaona wakoloni walitumia ugali kama bio weapon ya kuwadhoofisha wazee wetu kiakili.

Na sehemu wakoloni waliyokuja kumaliza mchezo kwa kuwavuruga akili mazima wazee wetu ni pale walipoingia porini kutafuta majani yanayoteleza na kuyapa jina la mlenda na kufanya hiyo ndio combinations bora ya mlo wa ugali.

Baada ya hapo ndio tumefikia hapa tulipo kila mtu amepoteana, tumekata ringi hatuna dira.

And sometimes if we're being honest, we gotta admit to speak the truth, that the world is better off without us.
 
Sina uhakika kuhusu faida za ugali mwilini, ila umedanganya kuhusu mataifa mengine kula ugali. Africa nzima chakula kikuu ni ugali kama unasema Nigeria, Ghana, Cameroon na west kwa ujumla hawali ugali basi inaonekana hujasafiri kwenda popote. Halafu hujui hata Corn flakes, pop corn 🌽 wanazobugia wazungu ni mahindi hayohayo tofauti ni mbeguna mapishi tu?.. kama ugali ungekuwa na shida yoyote basi hata shuleni na vyuoni kusingekuwa na wakufunzi, maana wote wamelelewa na ugali na maharage. Sema nini, unaonekana una ulimbukeni fulani hivi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…