SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

SI KWELI Ulaji wa Ugali husababisha udumavu wa akili

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na madai kuwa ulaji wa ugali hudumaza akili. Madai haya yana ukweli kiasi gani?

02692B18-05FE-4851-857F-7A5DA6E174CD.jpeg
 
Tunachokijua
Ugali ni chakula kinachotumika sana Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa utafiti wa Onu Okpa et al (2019), “Sub-Saharan African Maize-Based Foods - Processing Practices, Challenges and Opportunities” mahindi huchangia 30% ya nishati za vyakula wanavyotumia watu wa ukanda huu kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti huu, kila mtu anayepatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara hutumia wastani wa kati ya gramu 52-450 za mahindi kwa siku. Ni chanzo kikuu cha ugali unaotumika kila siku kwenye nchi hizi. Kwa Tanzania, 64% ya wananchi wake hula chakula hiki walau mara 5-7 kwa wiki.

Takwimu hizi zinaonesha kuwa ugali ni chakula kinachotumika sana, pengine kuliko aina nyingine za vyakula. Baadhi ya watu huutengeneza kwa kutumia unga wa mhogo, mtama, ulezi pamoja na aina zingine za nafaka.

Bila kujali tofauti ndogo za mgawanyiko wa virutubisho, nafaka zote husifika kwa kuwa na kiasi kikubwa cha nishati na wanga, pia kiasi kidogo cha madini na vitamini muhimu kwa afya.

Kuhusishwa na udumavu wa akili
Kitaalamu, udumavu wa akili husababishwa mambo mengi ikiwemo baadhi ya changamoto za kijenetiki mfano Down’s syndrome, kukosa hewa ya kutosha wakati wa kuzaliwa, maambukizi makali ya homa ya uti wa mgongo, utapiamlo, matumizi ya baadhi ya madawa na pombe wakati wa ujauzito pamoja na sababu zingine siziso wazi sana.

Kwa kurejea mgawanyiko wa virutubusho vinavyopatikana kwenye nafaka zinazotumika kutengenezea ugali, hakuna uhusiano wa moja kwa moja unaoweza kutajwa, au pia kuhusishwa na kusababisha udumavu wa akili kwa watu. Virutubisho na madini yake havina athari hasi kwenye afya ya ubongo.

Pia, JamiiForums imezungumza na wataalamu wa lishe ambao wamethibitisha kuwa chakula hiki ni salama, hakiwezi kusababisha madhara tajwa.

Hivyo, JamiiForums imebaini kuwa madai haya hayana ukweli uliojengwa kwa hoja za kisayansi. Ni uzushi usio na uthibitisho wa tafiti au takwimu.
Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli

Ugali ni mlo hatari ni kama sumu ndio maana hata wanyama wachoyo kama mbwa, nguruwe, paka, nk. Hawana akili lakini katu huwakuti wakila ugali maana ni chakula kisicho na nutrients zozote mwilini.

Hapa Tanzania jamii na makabila makabila makubwa hatupendelei ugali mfano sisi watu wa mkoa wa Kagera, Moshi(wachaga) na Mbeya hawali ugali lakini Tanzama mikoa duni kama Dodoma, Singida, Lindi, na watu wa Pwani wala ugali

Wenzetu wamataifa mengine wana afya afya na wala hawajui ugali ni nini Tazama wenzetu kutoka west Africa hawali maugali kama Watanganyika wana body zimejengeka.

Waganda, Wakenya, Wanyarwandwa hawali ugali. Mtu ukila ugali kwanza unalewa kama umepiga jibapa la Konyagi masaa mawili, ukila ugali wa Mara digestion ni ngumu mwilini chakula hakushuki hupati choo siku mbili, sasa hicho chakula au uchafu tu.

Wazungu na warabu wako vizuri kiafya wala hawayajui maugali ni nini wao wanajilia ngano, wali, nyama na maziwa, sisi Watanganyika kutwa usiku tunakula maugali na milenda kama tumerogwa

Madhara ya ugali kwa watu wetu, tumekosa washiriki wazuri kwenye michezo yani leo umpeleke Kibwana amkabe Sadio Mane AFCON haiwezekani.

Watoto hawana akili mashuleni wapo tu wamechoka yaani wamelewa chakali shuleni hawaewi kisa kula maugali.

Miili kama midogo kama digidigi unakuta mwanaume Dar anavamiwa na panya road anajificha kisa kula maugali

Sipendi ugali nakushauri usije ukala haya sumu ya akili na mwili ugali ni sumu kali

Nikiwa Rais nitapiga marufuku ugali

#kataa ugali Mtanganyika
Sikuwahi kufiki kama Una akili mbovu hivi.
Unapataje ujasiri wa kupanga ubora wa makabila hapa Tanzania? Masikini akinunua smartphone Ni anahesabu kavuka Mto
Hivi kuna mtanzania ambae chakula chake kikuu Sio ugali kweli?
Na Ni bahati mbaya sana kuwa Wewe hujatembea Hata hiyo Kenya yenyewe unayoisemea hujafika ukaona. Kwa post hii Ni ulimbukeni tu wa Smartphone unao
 
We kula maugali yako
 
Kwa hela ipi?
ugali maharage, mchicha utumbo,dagaa ndio tunaviweza.
Togwa, mlenda.
Kuku mpaka sikukuu, nyama weekend ukijitahidi sana.
kama huna "hela" ya kula vizuri ni tatizo lako. Unataka alibebe nani?
 
Huwa nakula ugali kwa hamu tu
Kiukweli sio chakula kile 😝😝😝
 
Watu wengi wanaamini ugali ndio chakula pekee cha kuupa mwili nguvu na afya njema lakini si kweli

Ugali ni mlo hatari ni kama sumu ndio maana hata wanyama wachoyo kama mbwa, nguruwe, paka, nk. Hawana akili lakini katu huwakuti wakila ugali maana ni chakula kisicho na nutrients zozote mwilini.

Hapa Tanzania jamii na makabila makabila makubwa hatupendelei ugali mfano sisi watu wa mkoa wa Kagera, Moshi(wachaga) na Mbeya hawali ugali lakini Tanzama mikoa duni kama Dodoma, Singida, Lindi, na watu wa Pwani wala ugali

Wenzetu wamataifa mengine wana afya afya na wala hawajui ugali ni nini Tazama wenzetu kutoka west Africa hawali maugali kama Watanganyika wana body zimejengeka.

Waganda, Wakenya, Wanyarwandwa hawali ugali. Mtu ukila ugali kwanza unalewa kama umepiga jibapa la Konyagi masaa mawili, ukila ugali wa Mara digestion ni ngumu mwilini chakula hakushuki hupati choo siku mbili, sasa hicho chakula au uchafu tu.

Wazungu na warabu wako vizuri kiafya wala hawayajui maugali ni nini wao wanajilia ngano, wali, nyama na maziwa, sisi Watanganyika kutwa usiku tunakula maugali na milenda kama tumerogwa

Madhara ya ugali kwa watu wetu, tumekosa washiriki wazuri kwenye michezo yani leo umpeleke Kibwana amkabe Sadio Mane AFCON haiwezekani.

Watoto hawana akili mashuleni wapo tu wamechoka yaani wamelewa chakali shuleni hawaewi kisa kula maugali.

Miili kama midogo kama digidigi unakuta mwanaume Dar anavamiwa na panya road anajificha kisa kula maugali

Sipendi ugali nakushauri usije ukala haya sumu ya akili na mwili ugali ni sumu kali

Nikiwa Rais nitapiga marufuku ugali

#kataa ugali Mtanganyika
Tatizo hujui ladha ya ugali,kachumbali na pande la nyama choma wewe...
 
Kwani nutrients unazipata kwa kula kitu kimoja pekee? Je, huo ugali unaliwa peke yake?. Wewe sema huna hela ya kununua samaki wa kula na ugali.
Wangapi wanauwezo wa kununua samaki wa bei ya TZS 13,000/= kwa kilo wakati na familia zetu zina wanakaya wasiopungua 10. Pia kiafya potion ya ugali inatakiwa isizidi 1/3 katika sahani lakini ulaji wetu wa Kiafrika potuon ya ugali ni 90% then mboga aina moja. Matunda hadi tuumwe na tuandikiwe na daktari.
 
Back
Top Bottom