Ulaya hali tete, Ufaransa yakatiwa gesi

Ulaya hali tete, Ufaransa yakatiwa gesi

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2017
Posts
458
Reaction score
1,280
Vita vya Russia na Ukraine vikiendelea na vikwazo vya nchi za Magharibi vikiwekwa Moscow,mauzo ya gesi ya Russia kwa Ulaya yamepungua sana na kuziacha nchi nyingi za bara hilo zikikumbwa na tatizo la kujidhamini nishati na kuongezeka gharama ya bidhaa hiyo,Shirika la gesi la Gazprom la Russia limetangaza kupunguza kwa asilimia 50 mauzo ya gesi kwenda Italia.

Mtiririko wa gesi katika mitandao ya usambazaji wa nishati kwa nchi zingine za Ulaya pia umekatishwa vyanzo vya Ufaransa vimethibitisha kwamba nchi hiyo haijapokea gesi kutoka Russia kupitia bomba.

Kampuni ya Usafirishaji wa gesi ya Ufaransa GRTgaz imesema kuwa mtiririko wa gesi ya Russia kupitia Ujerumani umesitishwa na kwamba nchi hiyo haijapokea gesi yoyote kutoka Russia kupitia bomba hilo tangu Juni 15,Ufaransa ambayo inategemea sana nishati ya Russia inadhamini takriban asilimia 17 ya gesi inayotumia kupitia mtandao uliounganishwa na Ujerumani.

Wiki iliyopita Gazprom ilionya kwamba itapunguza kwa kiasi kikubwa usambazaji wa gesi kwa Ulaya kutokana na masuala ya kiufundi yanayotokana na vikwazo vya Magharibi,Gazprom inahusisha masuala hayo na ucheleweshaji unaofanywa kwa makusudi na shirika la Ujerumani la Siemens,ambalo limejiunga na vikwazo vya Magharibi dhidi ya Russia.

Usambazaji wa gesi ya Russia kwenda Ulaya kupitia bomba hilo umepungua kwa asilimia 60 wiki hii,na hivyo kusababisha bei ya gesi barani Ulaya kupanda sana.

Katika kipindi cha miezi michache iliyopita,na kufuatia kuanza vita vya Russia na Ukraine nchi za Ulaya zimebuni na kutekeleza vifurushi mbalimbali vya vikwazo kwa ajili ya kutoa mashinikizo dhidi ya Russia.

Lakini vikwazo hivyo sasa vimefanya mambo kuwa magumu kwa nchi za Ulaya zenyewe,ambazo zinategemea sana rasilimali za nishati za Russia.

Pia bei ya mafuta barani Ulaya imepanda kwa kasi kubwa na hivyo kusababisha bei za bidhaa na huduma nyingi kupanda,huku nchi nyingi za bara hilo zikikabiliwa na mfumuko wa bei na kushuka kwa ukuaji wa uchumi.

Bei ya saa moja ya megawati ya gesi asilia katika masoko ya Ulaya, imefikia euro 130,hii ni katika hali ambayo bei hiyo wiki iliyopita ilikuwa euro 100 na mwaka uliopita euro 30.
 
Maumivu huanza taratiiibu mwishowe yanakuwa kansa
 
Nchi za Ulaya ni kama wanajitekenya na kucheka wenyewe, athari za vikwazo walivyomwekea Urusi atimaye vimeanza kuwarudi wao wenye,Kingine unafiki umewajaa sana viongozi wa Ulaya na kujipendekeza kwa Amerika.
 
Yes, naona Sasa vikwazo vinang'ata sawasawa, Russia hoi, dikteta anatumia Ngao ya kukata gesi ili vikwazo viondolewe apumue, kamwe hatoachiwa apumue ila atazidi kubanwa mbavu hadi ajisaidie haja kubwa. Dunia ya Sasa haiitaji madikteta.
 
Viwanda kibao huko ulaya vimelazimika kusitisha uzalishaji kutokana na kupanda kwa gharama za uzilishaji baada ya Urusi kupungunza usambazaji wa gesi kwa nchi za ulaya, sasa ndio tutajua nani kashika mpini?
Ndiyo wakati nzuri na fursa kwa nchi za Africa hasa zile zenye nishati ya Gesi, kutumia kama fursa ya kibiashara, Tuchimbe gesi tuwauzie nchi za ulaya, km VP walete technologia yao tuchimbe kisha tugawane gesi pamoja na mauzo yake kwa makubaliano yenye tija kwa pande zote mbili.
 
mkuu hata tukichimba .....kuisafirisha kwa meli kutaongeza bei ya hii nishati
itawachukua muda mrefu kujenga mabomba ya gesi kutoka middle east au west africa kwenda europe....
kwa hiyo watapoteza manufacturing prowess yao...
 
Ndiyo wakati nzuri na fursa kwa nchi za Africa hasa zile zenye nishati ya Gesi, kutumia kama fursa ya kibiashara, Tuchimbe gesi tuwauzie nchi za ulaya, km VP walete technologia yao tuchimbe kisha tugawane gesi pamoja na mauzo yake kwa makubaliano yenye tija kwa pande zote mbili.
Unaongelea Afrika? Hadi sasa hatujaona fursa, hadi wazungu waje kutuambia. Sqsa hv sisi tunayumba wafadhili wetu wanalia tutaishije. Ujinga wa karne

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo wakati nzuri na fursa kwa nchi za Africa hasa zile zenye nishati ya Gesi, kutumia kama fursa ya kibiashara, Tuchimbe gesi tuwauzie nchi za ulaya, km VP walete technologia yao tuchimbe kisha tugawane gesi pamoja na mauzo yake kwa makubaliano yenye tija kwa pande zote mbili.
😄😄 Nchi hizi za ki-Africa zinafaidikaje kwa kupewa royalty ya 3% tu?Jiulizeni Kipi kiliifanya Libya ikawa tajiri Sana kwa Mafuta yake na kipi kimezifanya nchi za kiafrica zishindwe kua tajiri Kama Libya wkt zinauza Gas,Mafuta na madini yake kwa wazungu.
 
Back
Top Bottom