Ulaya kuzinyima nchi za Afrika Mashariki misaada kwa kutokuridhia EAC-EU EPA


Kwa mara ya kwanza nashawishika kukubaliana nawe, pamoja na kwamba binafsi naunga mkono mkataba wa EPA lakini haya mambo ya kukomoana ni upuzi mtupu. Ni ukoloni mambo leo, nchi zisizokua na uwezo au ubavu wa kuhimili shughuli za EPA hazifai kulazimishwa.
 
unaona jinsi hii dili LA EPA linawapa wazungu faida kubwa kupitia soko hili la bidhaa zao la Africa Mashariki,
wameanza kutokwa povu. na naamini huenda wakatumia ubabe kulazimisha hii kitu
Let's stop being cowards bwana.
 
Itakuwa ni vizuri wakizuia hiyo misaada ili tupate akili ya kujisaidia wenyewe. Kwanza hiyo wanayotoa sio misaada maana hakuna msaada unaotaka return.
misaada mingi ni soft aids, maana wanatoa misaada ya vyandarua sijui condom na virainishi. misaada siyo jambo la kujisifu nalo, becouse neocolonialism came in a new style of International NGOs operation, mfano CARE Tanzania is pure american domination in Tanzania. watoe misaada ya maana kama vile kujenga viwanda kama kweli wana nia ya kutusaidia.
 
hahah umenifurahisha, niliwahi changia hivi siku moja kwenye kundi moja la whatsapp. kuhusu tishio hili la kunyimwa misaada kuna watu hawakunielewa, naunga mkono kwamba misaada hii inatulemaza kabisa. mfano huku tabora wakulima wa tumbaku wanakopeshwa mbolea kila mwaka cha ajbu watu hawajajikwamua na umasikini mpaka wamezeeka wanakopa mbolea, ni lini watasimama wenyewe.
 
Hahahaaa yaani wamekaa wakafikiria wakaona tatizo la Afrika ni uhaba wa KY Jelly [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Nation Media Group ya Kenya ndo wamiliki.

Ndio zenu, mkilemewa kwa hoja mnaanza kutapatapa, gazeti limeandika kwa kumnukuu secretary-general of ACP Mr. Gomes

“The truth is that Tanzania, Uganda and Burundi, which are sluggish in signing the deal, could end up losing important development aid from the EU,” Mr Gomes told the 32nd conference between the ACP and the European Union (EU) in Nairobi on Wednesday.
 
Nation Media Group ya Kenya ndo wamiliki.
hahahahaha wameshapewa virainishi wametepeta, najiuliza hivi familia zetu zinashindwa kununua vyandarua, siamini katika kushindwa kwasababu kila familia ya kijijini wanamiliki kuku.
 
Kwani uongo? Linasukuma pro-Kenya agendas.
 
njoo kwenye hoja ni kweli wakenya mnahitaji hizo soft aids, hiyo misaada imekuwa haina tija kwasababu tumesaidia miaka mingi sana na bado hatuafanikiwa kujitegemea wenyewe, nafikiri hili ni tatizo la africa nzima.
 
Tulishindwa kujitegemea toka zamani sasa ngoja tupewe masharti kama tuko kwa sangoma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…