Ulaya na Marekani wakibana, hata miradi kama SGR na Ujenzi wa Bwala la Umeme vyote vitakwama

Ulaya na Marekani wakibana, hata miradi kama SGR na Ujenzi wa Bwala la Umeme vyote vitakwama

Nchi ngapi za kiafrika zimeweza bila wao? Na zilichukua muda gani kufikia hatua ya kujitegemea bila misaada yao? Tutajie mifano michache tu.
Lbda tuanze na Zimbabwe ya Mugabe! wamefikia wapi?
Hatuhitaji mfano tunatoka kivyetu
 
European Union sio watu wa kukurupuka,wako slow lakini salama,hasa nchi za Afrika.

Hawataishabikia Tanzania kuvunja utawala wa Demokrasia lakini hawataiadhibu kama ilivyoadhibiwa Zimbabwe kwakuwa maslahi yaliwahusu wazungu wakulima wakipigiwa upatu na Uingereza.

Lakini utawala bora sio Demokrasia tu, kuna kudhibiti ufisadi, kukusanya kodi na kusimamia miradi kwa ufasaha. Kwa hayo mazuri ya Serikali ya Magafuli inaweza isichukuliwe hatua yoyote ya kuikwaza lakini wakiendelea kumshawishi afungue milango zaidi ya demokrasia.

Wazungu wa EU wanachojali Tanzania tokea enzi za Mwalimu Nyerere ni ikiwa amani itatoweka,lakini mengine ni subsidiary tu.
 
Hata dunia nzima ikikataa hapa nazungumzia pesa za kiserikali bado nchi itaenda vizuri tuu, ila tutakuwa tunapata mikopo ikiwa ghari kutoka taasisi za kifedha za kibifafsi.

Kwa level yetu sasa hivi ni haina shaka kabisa ila MKULU ni muoga sana sana wa madeni. Tuna uwezo wa kupata mpaka trillion 40 kwa mwaka bila taabu yeyote kwa interest ya 4% kwa miaka 10 tofauti na interest ya 2.5% kwa miaka 20 ya World Bank under IDA.

Kuna pesa nyingine dollars 5 billion ya kujenga reli kutoka Angola mpaka Dar es Salaam inatusubiri. Sio shida sana ila tutaendesha serikalini kwa gharama kubwa kuliko tulivyo zoea.
 
Yule Mpenda bifu na ligi ayajui hayo. Ni mweupe kuhusu external world and social economic integration
 
European Union sio watu wa kukurupuka,wako slow lakini salama,hasa nchi za Afrika.

Hawataishabikia Tanzania kuvunja utawala wa Demokrasia lakini hawataiadhibu kama ilivyoadhibiwa Zimbabwe kwakuwa maslahi yaliwahusu wazungu wakulima wakipigiwa upatu na Uingereza.

Lakini utawala bora sio Demokrasia tu, kuna kudhibiti ufisadi, kukusanya kodi na kusimamia miradi kwa ufasaha. Kwa hayo mazuri ya Serikali ya Magafuli inaweza isichukuliwe hatua yoyote ya kuikwaza lakini wakiendelea kumshawishi afungue milango zaidi ya demokrasia.

Wazungu wa EU wanachojali Tanzania tokea enzi za Mwalimu Nyerere ni ikiwa amani itatoweka,lakini mengine ni subsidiary tu.

Lkn hawawezi toa pesa zao zikatumike kuuwa demokrasia.Ubungo kimara walisitisha kutoa hela sababu haki za watu zilikiukwa.Watu ambao ni civilized na educated ujali Sana kuhusu haki za watu
 
Hata dunia nzima ikikataa hapa nazungumzia pesa za kiserikali bado nchi itaenda vizuri tuu, ila tutakuwa tunapata mikopo ikiwa ghari kutoka taasisi za kifedha za kibifafsi.
Kwa level yetu sasa hivi ni haina shaka kabisa ila MKULU ni muoga sana sana wa madeni. Tuna uwezo wa kupata mpaka trillion 40 kwa mwaka bila taabu yeyote kwa interest ya 4% kwa miaka 10 tofauti na interest ya 2.5% kwa miaka 20 ya World Bank under IDA.

Kuna pesa nyingine dollars 5 billion ya kujenga reli kutoka Angola mpaka Dar es Salaam inatusubiri. Sio shida sana ila tutaendesha serikalini kwa gharama kubwa kuliko tulivyo zoea.
Maisha yatakuwa magumu sana.
 
Lkn hawawezi toa pesa zao zikatumike kuuwa demokrasia.Ubungo kimara walisitisha kutoa hela sababu haki za watu zilikiukwa.Watu ambao ni civilized na educated ujali Sana kuhusu haki za watu
Nimekwambia hawatashabikia kuuwa demokrasia kama vile vile wasivyotaka serikali inayofuga ufisadi na kushindwa kusimamia miradi ya umma.
Lakini Afrika Yetu ni ngumu kupata serikali inayofanya kila kitu sawa.
 
Pinga pinga mtalia vilio vyote mwaka huu Jiwe alichowafanya hamtakaa muamini 🤣
 
Kiujumla vijana wa UFIPA hamna tofauti na popo hamueleweki ni wanyama au ndege.
 
Safari hii hawa WAHUNI wataendesha serekali yao kupitia vitambulisho vya wamachinga, walalahoi mkae chonjo.
 
Sasa hiyo yote kumkomoa magu? Tatizo washikishwa ukuta na mabeberu mnawashwa sana!
 
Ulaya na Marekekani wakibana na Marekani wakatumia influence yao kwenye mashirika kama Benki ya dunia, nchi hii miradi mingi itakwama na hata hiyo SGR na ujenzi wa Bwawa la Umeme vyote vinaweza kuathirika ikiwemo kukwama kabisa kwa miradi hiyo.

Hata kama fedha za hii miradi hazitoki Ulaya na Marekani, bado naamini support kubwa ya hawa tunaowaita mabeberu ndio inawezesha serikali kugharamia hiyo miradi kwa kuiongezea serikali uwezo wa kifedha kugharamia hiyo miradi sambamba na mambo mengine ya muhimu kama afya,maji,umeme.

Vile vile Benki ya Dunia-moja ya taasisi za fedha za kimataifa inayotukopesha- wametuwezsha kukamilisha miradi mingi ambayo CCM wanaitumia kujisifu: Ubungo interchange, soko la Ndugai kule Dodoma, Stendi ya kisasa Dodoma, n.k.

Kwakweli tuache kiburi na tuwe na shukurani kwani bila hawa watu tusingiweza kufanya baadhi ya mambo ambayo leo hii tunajisifu kuyafanya na zaidi tuache Kejeli za kuita hawa watu mabeberu ikiwa hata huduma za msingi kama elimu, afya na maji zinatushinda kuzitekeleza bila support yao.
Mkuu Hati ya Malipo,

Wewe ni Mtanzania na unaishi Tanzania pamoja na ndugu zako?

Roho yako sio, ila ili uridhike na dhima yako tafadhali washawishi hayo mashirika wafanye unavyotaka na badala yake hizo hela zipelekwe akaunti ya chama chako uone hazijapigwa pini hata kama utapitishia kwenye asasi zisizo za kiserikali na mashirika ya kutetea haki za binadamu huwezi kuzitumia ndani ya mamlaka ya Tanzania kwa sasa kisha utaambulia makosa ya utakatishaji pesa na uhujumu uchumi.
 
Hivi huwa mnafikiria kuwa wazungu wanafurahia kuona nchi ya kiafrica inajitutumua na kufanya jitihada za kujiendeleza, especially kwa ku-ignore misaada/mikopo yao? Kama huwa mnafikiria hivyo inabidi muanze kufikiri upya!

Na kwa kuwa wameshawapandikizia dhana potofu ya kuamini kwamba hamuwezi kufanya chochote kizuri bila wao, ndo wamewamaliza kabisa.
Closed minds. TZ siyo kisiwa.
 
Kuna baadhi ya wana CCM wasioelewa mambo wanasema ati Tanzania sasa imefikia hatua ya kujiendesha yenyewe bila kutegema wahisani wala mikopo ya masharti toka taasisi za fedha duniani.

Kwamba hawa the so called mabeberu wa EU na USA watuache!
 
Funguweni akili mgando hizo na muache kuwasujudu wazungu nao ni watu Kama nyie tu tofauti rangi tu.
Sawa tuache pia kuwasujudia mabeberu wa humu eti kwa vile ni weusi wenzetu.
Ubeberu hauna rangi wala kabila. Amen.
 
Back
Top Bottom