Kimsingi na kiuhalisia ilitakiwa kuwa hivyo, kinachoikwamisha Ulaya hasa Ulaya Magharibi ni kwamba Wana eneo dogo Sana la kijiografia, sambamba na kuwa na idadi ndogo sana ya Watu.
Viinchi vyao ni vidogo vidogo Sana, havina Ardhi ya kutosha ya kuweza kufanya Uwekezaji mkubwa zaidi wa miundombinu ya viwanda vikubwa zaidi vya kutengeneza silaha nzito sana' za maangamizi, viwanda vikubwa vya kutengeneza mitambo mikubwa mbalimbali, n.k. Na hawawezi kuongeza idadi kubwa sana ya Watu kwa njia za Uhamiaji wa Wataalamu kutoka nje ya bara hilo kwa sababu za ukosefu wa Ardhi ya kutosha kwa ajili ya miundombinu ya makazi na uchumi mkubwa zaidi.
Nchi ya Urusi peke yake ndio ina Ardhi kubwa zaidi barani Ulaya na duniani kote kwa ujumla. Njia pekee ya kuifanya Ulaya ya Magharibi kuwa na nguvu kubwa zaidi za Ushawishi wa kisiasa, kijeshi na kiuchumi ni kwa kuidhoofisha Urusi kwanza, kuimegamega zaidi na zaidi nchi hiyo ya Urusi na kisha kuisambaratisha kabisa kama vile ilivyofanyika kwa nchi ya Yugoslavia. Na mwisho kabisa kuziteka nchi mpya zitakazozaliwa baada ya kuisambaratisha Urusi ziwe upande wa nchi za Ulaya ya Magharibi kisiasa, kiuchumi, kisera, kimitizamo, n.k.