Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni nani MMILIKI wa hayo Mafuta na Gesi? Tuelezee hapa tujue mgawanyo wa mapato yanayotokana na mauzo ya hayo mafuta. Nchi ya Uganda inapata asilimia ngapi na Wageni wavunaji wa hayo Mafuta wanapata asilimia ngapi kwa kila Pipa la Mafuta?Kama wewe ni wale waafrika wanahamaki wanamapinduzi tukiwaita wamagharibi mabeberu kutokana na ulevi wa fikra waliyofanikikiwa kukupandikiza, na kama uko Afrika ya mashariki yafaa uzinduke sasa.
Kutokana na mipango ya nchi za maghararibi nchi za Uganda na Tanzania haziruhusiwi kuendeleza miradi ya gesi na mafuta kwa sasa hata kama wao watataka kufanya hivyo ila tu pale wao wakiona itaendana na mipango yao ya kinyonyaji.
Nchi za ulaya ya magharibi baada ya kuona vibaraka wao wameshindwa kuzuia mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania sasa wanatapatapa. Kupitia bunge la ulaya eti wamepitisha azimio kukataza uendelezaji wa mradi wa bomba hilo eti litaharibu mazingira na kuwaondoa watu wengi kwenye ardhi zao.
Tangu lini hawa wakoloni wa Afrika wameanza kua na huruma na waafrika? Siku hizi eti wanatufundisha haki za binadamu ambapo kipau mbele eti turuhusu ushoga ndoa za jinsia moja na utoaji mimba. kusema kweli hawa wazungu wanatudharau na kutukosea heshima kwa kiwango kikubwa.
Bunge la Uganda tayari wamepitisha azimio kulaani azimio hilo la bunge la ulaya. Inafaa bunge la Tanzania pia tulaani azimio hilo la kibeberu lisilo na haki wala ukweli wowote.
Nchi zetu za Uganda na Tanzania tusishtuke wala kukwazika na ubeberu wa magharibi. Tuendelee na mpango wetu na sio kukubali kupelekeshwa na wamagharibi ambao mipango yao ni kuzinyonya nchi zetu na kuhakikisha hazipati maendeleo ya kweli yenye kuwapa wananchi wetu maisha bora.
Baada ya kuondokewa na Magufuli Watanzania tunakutegemea mzee Museveni kuongoza mapambano dhidi ya mabeberu hawa kuhusu huu mradi wa bomba la mafuta.