Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

Uganda akiongea Kiingereza, sawa tu manake wale jamaa wana bifu na Kiswahili!!

Kenya, kwa kuwakomoa tu, anapaswa atumie Kiswahili manake Kiswahili wanakijua vizuri lakini kutokana na ulimbukeni wao wa kumsujudia Mzungu, wanajifanya hawakijui!!
Aliyekwambia hatujui Kiswahili ni nani? Ama wewe ndio msemaji wa KE?
 
Hata kuna yule waziri mmoja sijui wa nini, alikuja from Tz na kuhutubia kwa Kiswahili pale KICC, so sioni issue hapo kwa kutumia lugha yoyote ile atakayojiskia.
 
Facts. Kitu kingine kuhusu UG, niliambiwa na mganda mmoja tulikuwa tunafanya kazi wote kanda flani, kua kwao vyuo vya polisi na jeshi ndio wanapata masomo ya Kiswahili ila huku shule za raia, kiswa kiko rare, yaani rare kufundishwa. Ni kizungu, na kikwao, period. Sijui kanidanganya yule dogo lkn ndio ivyo! 🤣
 
Wewe angalia picha za tv basi, nani kakunyima kusoma ukaelewa kudhungu, lugha ya biashara kimataifa?! Nyau wee!
 
Ni kweli... kiswahili kiliingia zaidi UG kupitia soldiers, wakati wa vita kwani wengi walipata mafunzo Tz...ama sivyo kwa raia wengi ni wazito kutaka kujifunza na kukitumia, wakipendelea English na local languages...
 
Akili za kitumwa hizi...mwendazake hayupo and will never come back...
Wake up...!

Mwanadamu unahitaji flexibility ili uweze ku win hearts and minds of people, na namna mojawapo is thru speaking people's tongues...
 
Zumbukuku kingeli inaitwaje? Wewe ndugu ni lofa mwenzangu tu acha hizoo
Mimi sio lofa mwenzako. Usijipendekeze.
Oh Lofa wa Mwendazake
 
..kuna kitu kinaitwa " WORKING LANGUAGE " ambacho Watz lazima tufahamu maana yake.

..working language maana yake ni lugha rasmi zinazotumika ktk shughuli na mawasiliano ya shirika fulani la KIMATAIFA.

..tunapotafuta kazi ktk MASHIRIKA NA TAASISI ZA KIMATAIFA ni lazima tuwe na uwezo wa kuwasiliana ktk working languages zinazotumika ktk mashirika hayo.

..Ni vizuri kuipenda na kuienzi lugha yetu ya Kiswahili, lakini tuzingatie ukweli huo hapo juu.

cc Chige, Nguruvi3, Masanja
 
Ni jambo jema.
 
Safi sana
 
Kwahiyo huwezi kufanya diplomasia bila kizungu? Ona jinga hili!

Wachina na warusi mbona wamekupiku kwenye kila jambo pamoja na hicho kiingereza chako cha kuokoteza?

Ati diplomacy sijui nini nini!

Umejipiiindaa mwenyewe unaandika uharo mtupu!
What makes one set of words more convincing than another, and how can language best be put to work in the service of diplomacy and international relations?

This course promotes language awareness as a means of improving the skills of opinion shapers. Close attention is paid to case studies of treaties, presidential speeches, public announcements, government advertising and media materials in order to link theoretical discussion to practical examples. Since effective communication has much to do with reading intentions and contexts correctly, insights are provided into relevant cultural, social and psychological variables.

Read more: Language and Diplomacy course | DiploFoundation

 
Nakubaliana na wewe kwa asilimia zote ndo maana hapo juu nikashauri, tunatakiwa kufundishwa Kiingereza kama Second Language na sio kama somo!!!

Ukifundishwa lugha as a second language inakuwa rahisi sana kui-master kuliko ukifundishwa kama somo!!

Unapofundishwa as a second language, mtaalamu una-focus sana kwenye kui-master lugha kama nyenzo ya mawasiliano na sio kui-master lugha from technical side of the language!!

Ni kutokana na hilo, ndo maana hata mtu anayejifunza Kiswahili kama second language/lugha ya mawasiliano, inakuwa rahisi sana kuki-master kwa sababu yale mambo sijui mofimu, mara tungo changamano, and all that, yanakuwa sio ya msingi kwa mtu anayejifunza lugha kama chombo cha mawasiliano!!
 
Wakenya wote hufikiri kwa Lugha ya kigeni huona ni ufahari kuongea kingereza kuliko hata Lugha zao za Asili
Upo sahihi kwa 100%, matokeo yake, wapo wapo tu!! Sio Top kwenye uzungumzaji wa Kiingereza hata Afrika! Sio Top kwenye uzungumzaji wa Kiswahili!! Sio Top kwenye uzungumzaji wa lugha yoyote ile!!
 
Rais wao pia kila akitutembelea anatumia Kiswahili..ata msiban aliongea Kiswahili vizuri Sana kuliko baadhi ya mawaziri wetu
Ndo suala ambalo mara kwa mara nimekuwa nikiwahoji Wakenya kwamba, Uhuru ana exposure kubwa sana, amekulia maisha mazuri sana kuliko majority of Kenyans lakini anaongea Kiswahili vizuri sana, na ni mara chache sana utamkuta anatumia Kiingereza mbele ya hadhira kubwa ya Wakenya!!

Leo hii kama utapanga orodha ya viongozi wa Kiafrika hapa Afrika Mashariki na kati, sina shaka Uhuru ndie anaongoza kwa kutoijua kabisa shida!!

Ndipo nawahoji, inakuwaje nyie watoka shamba huko, tena kwenye familia duni, lakini mkishafika tu Nairobi ndo mnajifanya hamkijui Kiswahili!!! Hili swali bado sijawahi kujibiwa
 
Man,

Mbona marais wetu kule bungeni huwa wanatumia Kiswahili hata kama kuna wageni wasiojua Kiswahili?!

That's one but second, Samiah anahitaji kueleweka na Mabeberu waliopo Tanzania na sio waliopo Kenya!!

Kama shida yake ni kueleweka na Mabeberu, anaweza kuandaa meeting na Mabeberu wote waliopo Tanzania, kuanzia diplomats hadi wafanya biashara!! Anapoongea na hawa, hakuna shaka hata kidogo kwamba atatumia Kiingereza TU!!

Hawa, ndio watapeleka ujumbe kule kwao kwamba hali ya kisiasa na kiuchumi Tanzania ipo abc!!! Lakini pale Kenya, yeye ameenda kuongea na Wakenya... hao wengine kama watakuwepo basi watakuwa ni waalikwa tu!!

Simtarajii Balozi wa Marekani nchini Kenya kwa mfano, aripoti suala la Samia na siasa za Tanzania wakati Tanzania kuna Balozi wa Marekani, na ni yeye ndie mwenye huo wajibu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…