Heheheee....
Kuwa kiongozi sio swala la kuvaa tu ushungi na kurembua. Uongozi ni kipawa.
Kwa tunaofuatilia siasa za kimataifa, tunaelewa nini maana ya Kiongozi mwenye kipawa cha uongozi.
Nikupe kijikazi kidogo — fuatilia hotuba ya Obama ndani ya bunge la uingereza.
Nina uhakika kwamba, itamchukua Bibi sasha zaidi ya miaka mia kuweza kumudu ile mastery ya oratory skills.
Ndio maana, sisi wenye utambuzi wa mambo, tunashangaa anapotusomea vizungu vya kwenye makaratasi.
Lakini kwa ninyi magoigoi msiojua dunia inaenda wapi, kwa hakika anawakoga sana kwa kile kizungu chake butu.
..sio sahihi kuzungumzia "kurembua macho," na "kuvaa ushungi," halafu ukamtaja Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
..kuhusu Barack Obama, yule anajulikana kama mmoja wa wazungumza mahiri kabisa popote duniani.
..pia lazima uelewe kwamba hotuba ya Rais Obama ambayo umetutaka tuiangalie ni hotuba ambayo imeandikwa na alikuwa akisoma kutumia kifaa kinaitwa teleprompter.
..mimi nadhani sio sahihi kumtaka Rais wetu atoe hotuba kwa viwango vya Barack Obama, na haijalishi hotuba hiyo ni ya Kiingereza, au Kiswahili. nadhani tutakuwa hatumtendei haki hata kidogo kunatokana na kipaji cha kipekee alichokuwanacho Barack Obama.
..Rais Samia Suluhu awe na utaratibu wa kuandikiwa hotuba, na ahakikishe anafanya mazoezi ya kusoma hotuba hizo kabla ya kwenda mbele ya hadhira. Na haijalishi hotuba hizo ni za Kiswahili au Kiingereza. Viongozi wote wa mataifa makubwa hu-practice hotuba zao kabla ya kupanda majukwaani.
..Hotuba ya Obama nimeiweka hapo chini.