Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

Unaandika mambo meeeeengii... ujinga mtupu! — Kuandika kwenyewe hujui.

Ni sawa, Kiingereza kina umuhimu wake. Lakini pia kina mahala pake.

Tutambue mahala sahihi pa kukizungumza.
 
ningependa Bi Mkubwa atumie Kiswahili!

hua nafurahi sana nikiona viongozi mbali mbali wa asia hasa wa Kichina wakitumia lugha yao.
 
Nina uhakika kuwa umahiri wangu wa kuzungumza Kiingereza ni mara mia mbili zaidi yako.

Sibabaiki kwa sababu ninakijua vilivyo.

Kwahiyo usinitishe tishe hapa bwana mdogo.
 
Uganda siku ile, pamoja na waganda kukijua kiswahili lakini hadhira ile ilihusisha pia na wawekezaji wa bomba la mafuta ambao hawajui kiswahili bali kiingereza, kuna sababu gani kulazimisha kiswahili kama Magufuli aliyekuwa hajui hiyo lugha nyingine?
 
Hii lugha ya kiswahili haina soko. Kwasabb ilipaswa kubeba teknolojia/maarifa ambayo ndiyo yangevutia watu kujifunza kiswahili
Lugha yenyewe watz wengi siku hizi ni shida, hata afadhali kule Mombasa Kenya wanatushinda,,tumebaki na kiswahili cha mitaani kisicho rasmi...Mama wewe soma hotuba ya kiingereza tu ujiondokee...
 
Uganda siku ile, pamoja na waganda kukijua kiswahili lakini hadhira ile ilihusisha pia na wawekezaji wa bomba la mafuta ambao hawajui kiswahili bali kiingereza, kuna sababu gani kulazimisha kiswahili kama Magufuli aliyekuwa hajui hiyo lugha nyingine?
Lazima lugha inayotumiwa iakisi "hadhira pana" inayolengwa.

Hao unaowaita wawekezaji walikuwa hawazidi hata kumi.

Lakini kulikuwa na maelfu ya wananchi ambao walihitaji kusikia mambo yakizungumzwa kwa Kiswahili.

"Muktadha". Zingatia sana.
 
Uganda akiongea Kiingereza, sawa tu manake wale jamaa wana bifu na Kiswahili!!

Kenya, kwa kuwakomoa tu, anapaswa atumie Kiswahili manake Kiswahili wanakijua vizuri lakini kutokana na ulimbukeni wao wa kumsujudia Mzungu, wanajifanya hawakijui!!
Ujue pia akiwa pale Nairobi bungeni atakua haongei na wakenya pekee, balianaongea na jumuiya ya kimataifa kupitia bunge la Kenya. Peleka watoto shule waweze kupambana duniani mkuu.
 
Lazima lugha inayotumiwa iakisi "hadhira pana" inayolengwa.

Hao unaowaita wawekezaji walikuwa hawazidi hata kumi.

Lakini kulikuwa na maelfu ya wananchi ambao walihitaji kusikia mambo yakizungumzwa kwa Kiswahili.

"Muktadha". Zingatia sana.
Kwa Uganda pale unadhani kuna mtu hakumuelewa? Pengine angeongea kiswahili ndio wengine wasinge muelewa
 
Ukitaka kuendelea kuonekana kituko kwenye nchi za Commonwealth endelea kuongea Kiswahili.

Hivi mnataka kuendelea na UMBUMBUMBU wa Mwendazake ambaye anadai ana PhD ya Chemistry lakini hawezi kutengeneza sentensi ya English yenye correct grammar??

Hapana, Hapana, Hapana. Tutaongea Kiswahili kwenye masuala yetu lakini kwenye jumuiya za kimataifa kuna lugha 7 kubwa; Chinese, English, French, Portuguese, Spanish na Russian
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…