Tumesikia Bi. Samia anaenda Kenya kwa ziara ya kikazi mnamo hapo kesho.
Ni matumaini yangu na fahari yangu kwamba atatumia Kiswahili katika shughuli zote atakazoalikwa kuzifanya.
Hivi majuzi tu alipoenda Uganda, tuliona anatumia kizungu kuhutubia.
Wengi wa wananchi wetu nina uhakika hawakuelewa hata anachozungumza.
Ifahamike kwamba, Kiswahili si lugha ngeni Afrika Mashariki. Tuachane na Viingereza pasipo na ulazima.
Sijui ni nani aliyewalaghai kwamba kuongea kizungu ni ufahari na usomi?
Hata katika mazingira yasiyohitaji kizungu, bado watu watajing'ang'aniza kuongea kizungu hata kama hawakiwezi na tunajua kwa hakika kwamba hawakiwezi.
Hebu tuachane na hizi "You Know You know ofcozi zea zea" mingi mingi. Tunajiaibisha na kujidunisha.
Tunayo lugha adhimu ya Kiswahili. Tuitumie hiyo.
Nasubiri kuona hiyo Kesho vile Bibi SASHA atakavyojitutumua na viingereza vyake uchwara.
Ashauriwe vyema. Maana shughuli za aina ile sio mahali pa kuonesha mbwembwe za kuzungumza kwa lafudhi bandia za kimalkia.
Tunahitaji kusikia "maswala" yakijadiliwa na kuzungumzwa. Hatuhitaji mikogo ya lafudhi bandia za Kizungu.