Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

Commonwealth ipi wewee, wacha kujitutumua hapa.

Nina uhakika hata maana tu ya "Commonwealth" huijui.

Haya kamanda, hebu tueleze... "Commonwealth" ni kitu gani?
 
Ujue pia akiwa pale Nairobi bungeni atakua haongei na wakenya pekee, balianaongea na jumuiya ya kimataifa kupitia bunge la Kenya. Peleka watoto shule waweze kupambana duniani mkuu.
Kwani anapoongea Bungeni, Tanzania inakuwa hakuna watu wa mataifa ya nje?! Btw, suala la kuongea Kiingereza/Kiswahili linahusiana vipi na kupeleka mtoto shule?
 
english ndio international language. hakuna ubaya kama hadhara anayoenda kuhutubia ina uelewa.
 
Japo sikijui vizuri kiingereza ila kiingereza, kina maneno ikiyasema unaonekana yanatoka moyoni kabisa. Mfano mtu akikuambia, Nakupenda, na mwingine akakuambia i love you🤣🤣😁😁 kuna tofauti kubwa sana.

Mwache mama aongee lugha anayoona akiongea atafikisha ujumbe. Maana hata hao wakenya wanatuona hatujui hii lugha ya malkia.
 
Nina uhakika kuwa umahiri wangu wa kuzungumza Kiingereza ni mara mia mbia zaidi yako.

Sibabaiki kwa sababu ninakijua vilivyo.

Kwahiyo usinitishe tishe hapa bwana mdogo.
Isijekuwa kiingereza chako ni kama kile cha Jiwe au mlachako?
 
Mleta mada sema wewe hujui English . Kinakusumbua na umekichukia . Samia anamudu lugha hiyo na huhitaji kumuwekea mipaka .

Rais akiwa ugenini kule hawahutubii waTz wenye matatizo na English . Bali anawahutubia wenyeji wake wenye uelewa wa English . So si lazima uhangaike na hotuba ya Rais akiwa ughaibuni. Subiri Msigwa atakutafsiria.
 
J. K. Nyerere alishasema English ndo Kiswahili cha dunia.. pamoja na kukikuza sana Kiswahili, alikijua Kiingereza vilivyo.

Ukiamua kujifunga kongwa la Kiswahili pekee ni juu yako
 
Uganda akiongea Kiingereza, sawa tu manake wale jamaa wana bifu na Kiswahili!!

Kenya, kwa kuwakomoa tu, anapaswa atumie Kiswahili manake Kiswahili wanakijua vizuri lakini kutokana na ulimbukeni wao wa kumsujudia Mzungu, wanajifanya hawakijui!!
Kenya mtaaniu wanaongea Kiswahili, hata kiongozi akiwa anahutubiua wananchi naongea Kiswahili, taarifa ya habari mara nyingi pia wanasoma pia kwa Kiswahili Kikwete alipohutubia Bunge la Kenya alitumia Kiswahili

Tofauti na Uganda, waganda wengi Kiswahili hawafahamu
 
Tupeleke watoto shule ...tuache kujificha kichaka cha kiswahili....watoto waweze compete karne hii yenye ushindani mwingi sana
 

Kiingereza anachoenda kuongea ni cha kusoma, na kusoma anaweza. Ww sema hutaki aongee hicho kiingereza ili kumfichia aibu Magufuli maana alikuwa hakiwezi. Asiyejua kiingereza huku kwetu kuna uchambuzi wa hicho atakachokuwa ameongea.
 
Uganda akiongea Kiingereza, sawa tu manake wale jamaa wana bifu na Kiswahili!!

Kenya, kwa kuwakomoa tu, anapaswa atumie Kiswahili manake Kiswahili wanakijua vizuri lakini kutokana na ulimbukeni wao wa kumsujudia Mzungu, wanajifanya hawakijui!!
Kiswahili ni lugha ya kupigia Majungu na kufanyia ushirikina. Ni lugha duni isiyoweza kukusogeza kokote kwa maana, zaidi ya kuwasiliana na wanyonge a.k.a makondoo wenzako.
 
Itoshe tu kusema kwamba wewe ni mpuuzi aliyechangamka!
Mpuuzi ni wewe usiejua lugha. Ukidhani wote hawajui . Jiwe ametuletea balaa la wajinga wengi sana, nawe ni miongoni mwao.

Samia anakiweza kizungu na usimpangie . Shame on you pro Jiwe [emoji107][emoji3517]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…