Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

Ulazima wa Kiingereza cha Rais Samia ziarani nchini Kenya

Ambokile Amanzi

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2018
Posts
965
Reaction score
1,333
Tumesikia Bi. Samia anaenda Kenya kwa ziara ya kikazi mnamo hapo kesho.

Ni matumaini yangu na fahari yangu kwamba, atatumia Kiswahili katika shughuli zote atakazoalikwa kuzifanya.

Hivi majuzi tu alipoenda Uganda, tuliona anatumia kizungu kuhutubia.

Wengi wa wananchi wetu nina uhakika hawakuelewa hata anachozungumza.

Ifahamike kwamba, Kiswahili si lugha ngeni Afrika Mashariki. Tuachane na Viingereza pasipo na ulazima.

Sijui ni nani aliyewalaghai kwamba kuongea kizungu ni ufahari na usomi?

Hata katika mazingira yasiyohitaji kizungu, bado watu watajing'ang'aniza kuongea kizungu hata kama hawakiwezi na tunajua kwa hakika kwamba hawakiwezi.

Hebu tuachane na hizi "You Know You know ofcozi zea zea" mingi mingi. Tunajiaibisha na kujidunisha.

Tunayo lugha adhimu ya Kiswahili. Tuitumie hiyo.

Nasubiri kuona hiyo kesho vile Bibi SASHA atakavyojitutumua na viingereza vyake uchwara.

Ashauriwe vyema. Maana shughuli za aina ile sio mahali pa kuonesha mbwembwe za kuzungumza kwa lafudhi bandia za kimalkia.

Tunahitaji kusikia "maswala" yakijadiliwa na kuzungumzwa. Hatuhitaji mikogo ya lafudhi bandia za Kizungu.
 
Kenya lugha ya taifa ni English
Ndio maana unaitwa Denlson.

Mnyaturu wa singida ndani huko mavumbini unaitwa DENLSON...... Aisee!!!

Kwa kukusaidia tu "Bwana Denlson", Lugha ya Taifa ya Kenya ni Kizungu pamoja na Kiswahili. Na zote ni lugha rasmi zinazotambuliwa na Katiba yao mpya.

Kwako DENLSON.
 
Watanzania tuna shida kubwa sana, kwani kulikuwa na ulazima gani kuandika hivi? Subiri magazeti yatakuandikia kiswahili
Tujifunze kuwa kiswahili sio lugha ya kila mahali na sio rafiki ya kila mtu ukiwamo wewe.
 
Teknolojia kama ipi kwa mfano?

Hebu tueleze kamanda!
China ndiyo wazalishaji wakubwa wa bidhaa za viwandani kwa Sasa, mpk USA anaihofia. Hapa bongo % kubwa ya biashara zetu zinategemea bidhaa kutoka China. Ndiyo maana hata tahasusi za kichina zimeanzishwa hapa bongo.

Sasa wewe mswahili unazalisha nn kinachopendwa duniani?
 
Dunia ya sa hv kingereza ni lazima ukijue tena vizur ..tusijidanganye kabisa ..... Kwa Kenya haina shida wale ni waswahili Tu fresh , lakn zaidi ya yote kingereza ni lazima ukijue ili utoboe.

Kenya wametuzidi sababu most of them Wana fluent English , wanaweza toboka popote pale duniani ni issue ya nauli na visa tuu.... Na duniani ndo kuna fursa ,sasa wewe mabonde kuinama , mdomoni umejaza kimakonde na Kiswahili cha tabu hata ukipewa nauli uende Vietnam lazima uchochore tuu na kilimo kwanza
.
Ndo ujinga wa jiwe anawakomoa na mikodi mizito alaf hela anaenda kununua ndege 🤣
 
Tumesikia Bi. Samia anaenda Kenya kwa ziara ya kikazi mnamo hapo kesho.

Ni matumaini yangu na fahari yangu kwamba atatumia Kiswahili katika shughuli zote atakazoalikwa kuzifanya..
Kwanza, English haikwepeki dunia hii, jifunze tu kama huwezi utaishi sana kwa stress.

Pili, Rais Samia hajasema atahutumia Kiingereza au Kiswahili tayari wewe umemhukumu na kuja na upumbavu wako.

Kama hujui, Kikwete amewahi kuhutubia bunge la Kenya na alitumia Kiswahili.

 
Watanzania tuna shida kubwa sana, kwani kulikuwa na ulazima gani kuandika hivi? Subiri magazeti yatakuandikia kiswahili
Tujifunze kuwa kiswahili sio lugha ya kila mahali na sio rafiki ya kila mtu ukiwamo wewe.
Wewe nina uhakika hata Kizungu kikizungumzwa huna uwezo wa kukielewa.

Unabaki na zile you know zea zea.. ofkozii.

Jikite na Kiswahili bwana mdogo. Usijitutumue.
 
Una hoja ila sasa umeiwasilisha kwa namna duni sana.

Nikupe tips:

1. Unapowasilisha hoja epuka maneno ya kihuni "uchwara", zea zea*
2. Epuka lugha ya kudhalilisha "uchwara"
3. Usionyeshe mlengo wako.
4. Weka hisia, chuki na hisia chanya pembeni.

Kwa kuwa una uwezo wa kuandika, ukizingatia hayo mambo hapo juu utakuwa mwandishi mzuri sana.
 
Back
Top Bottom