eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Rais Magufuli ateuliwa mshindi wa tuzo ya Ukombozi Afrika
Image copyrightAFP
Image captionWakosoaji wanasema amepunguza nafasi ya raia kujieleze kwa uhuru
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ameibuka mshindi wa tuzo ya Afrika katika masuala ya uchumi.
Makamo mwenyekiti wa kamati ya tuzo ya ukombozi Afrika, Mwebesa Rwebugia ameieleza BBC kwamba rais Magufuli ameibuka mshindi kutokana na mchango wake wa kiuchumi hasaa katika ukuaji wa miundo mbinu.
Hii ni mara ya pili kwa kiongozi wa Tanzania kupata tuzo hii, baada ya Mwalimu Julius Nyerere kutuzwa pia kutokana na mchango wake wa kuleta uhuru katika nchi za Afrika.
Kwa mujibu wa kamati hiyo ya Tuzo ya Ukombozi wa Afrika, ukombozi katika kipengelee cha elimu huangazia elimu na ujinga kama sehemu ya ukombozi.
Tanzania imetolewa mfano wa elimu ya bila malipo kutoka kutoka shule za msingi mpaka sekondari.
Image captionJulius Nyerere alikuwa na ushawishi mkubwa katika mataifa ya Afrika kujipatia uhuru.
Katika suala la umaskini, kamati imeangalizia hatua ya kuwajali watu wa kipato cha chini, ukitolewa mfano wa kusajiliwa kwa 'machinga' katika kuwatambua rasmi kwa shughuli zao, na pia kuondolewa kodi za mazao kwa wananchi.
Lakini sio kila mtu amepokea vyema ushindi huu wa rais Magufuli kutokana na kwamba kiongozi huyo hajakamilisha hata miaka mitano tangu aingie madarakani.
Wakosoaji wanasema amepunguza nafasi ya raia kujieleze kwa uhuru.
Na serikali yake imekosolewa kwa hatua za kuvizima vyombo vya habari na kinachotajwa kama kuvikandamiza vyama vya upinzani.
Mambo matano unayoyahitaji kuwa bilionea
Obama aikumbuka safari yake ya kwanza nchini Kenya
'Rais magufuli hakutazamwa kwa muda aliyoingia madarakani lakini tangu miaka 20 iliyopita. Tangu alipokuwa wizara ya ujenzi na mawasiliano na nyingine tofauti, mpaka kufikia hadi ya kuwa rais wa taifa. Je ni mambo gani aliyoyafanya?' Amefafanua Rwebugia.
Mnamo 2016 Magufuli alishinda tuzo ya Forbes Africa kwa kuwa mtu anayeheshimika zaidi - na aliteuliwa kwa kutambulika jitihada zake za "kushinikiza uchumi wa Tanzania".
Viongozi wengine walioishinda Tuzo ya Ukombozi:
Tuzo ya Ukombozi Afrika inatambuliwa barani Afrika na Kimataifa lengo lake ni kutambua mchango wa viongozi wa bara la Afrika , wapigania uhuru, wapatanishi wa amani na washiriki wengine wa Ukombozi wa Afrika.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni mwishoni mwa mwaka jana aliwahi kuteuliwa mshindi na kamati inayoratibu Tuzo hiyo ya Ukombozi Afrika.
Ushindi wake Museveni ulitangazwa baada ya kamati hiyo kuketi mwezi Oktoba, 2017 na kujiridhisha kupitia vigezo vilivyowekwa kuwa kiongozi huyo anakidhi vigezo vyote.
Image copyrightGETTY IMAGES
Alitambuliwa miongoni mwa mengine kwa mchango wake mkubwa wa kipekee alioutoa katika kusimamia amani katika nchi zilizokumbwa na migogoro ya ndani Somalia, Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo na Burundi.
Vigezo vinavyozingatiwa pia ili kuteuliwa mshindi ni pamoja na mchango wa kiongozi katika ukombozi wa taifa kutoka tawala dhalimu miaka ya nyuma.
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 17.07.2018
Viongozi wengine waliowahi kuishinda tuzo hiyo ni pamoja na Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Kenneth Kaunda wa Uganda ambao walitunukiwa tuzo hiyo mwaka 2014.
Rais Magufuli sasa anatarajiwa kupokea medali na cheti katika tarehe rasmi itakayotangazwa na kamati baada ya maridhiano kati ya mgeni rasmi na watu wa itifaki.
- 17 Julai 2018

- Mambo makuu kutoka kwa mkutano wa Trump na Putin
- Watu 40 wauawa kwenye mafuriko Nigeria
- Trump shutumani kwa kuitetea Urusi