Ule utu baina yetu sijui umeenda wapi?

Ule utu baina yetu sijui umeenda wapi?

Siwaelewi,jamaa analia kama mtoto kweli washindwe kugundua ?watu wamekuwa mafala sana
Watu walijua ni maigizo wewe halafu angekua kwao watu wanamjua angepiga kelele vile wakwao lazima wangeingilia ameenda mtaa gani huko watu wanajua maigizo ya Azam TV Sinema Zetu
 
.
1731505074277.jpg
 
Ile clip nimeiyona kila nikiskia jamaa analalamika wamsaidie naskia kama nataka kulia 😪inahuzunisha kwakweli basi tu
Mkuu binafsi huzuni niliopata baada ya kuiona clip ile, sijawahi pata huzuni na mfadhaiko wa aina hiyo kwa miaka mingi sana, na nimeazimia kbs mwaka huu nitafanya juu chini nimiliki silaha ndogo ya moto, binadamu amekuwa ni kiumbe katili sana! just imagine, mtekwaji anapiga kelele akiweka wazi kabisa kuwa anaenda kuuawa, na kwamba watu wale hawajui...lkn hana msaada zaidi ya kupambania roho yake mwenyewe! na hiyo ni mchana kweupe je usiku ingekuwaje?
 
Hili ni tatizo la serikali,ingetakiwa umma uambiwe kuanzia sasa hivi polisi wakija kumkamata mtu kwanza wawe na vitambulisho,nakwambia ingekuwa hivyo utekaji ungepungua,tatizo hajulikani nani ni tanpol na nani wasio julikana
Kwa vyovyote vile wa kuuambia umma ndiye mhusika mwenyewe kwenye asimilia kubwa ya matukio ya aina hiyo. Anajua atakavyokwamishwa kwenye kutimiza malengo yake iwapo atatoa tamko hilo kwa umma. Kama ni yeye kaweka utaratibu sahihi wa ukamataji, pamoja na kuongezeka kwa matukio hayo ya utekaji yanayoenda sambamba na upoteaji wa jumla wa watekwaji, shambulio, vilema na mauaji, na kama yeye angekuwa hahusiki ni kwa nini asiutangazie umma na kusimamia uzingatiaji wa utaratibu huo wa ukamataji?
 
Wakina Logikos wanafahamu vizuri zaidi



Na hayo niliyasema zamani sana..., ila inabakia palepale sisi kama Raia tuna utaifa in comparison na nchi nyingi sana especially USA tunawaacha mbali sana...., Wanasiasa walaghai, walamba asali na uongozi wenye Ombwe hauondoi ukweli huu.... Na hio naongelea leo..., tunapoelekea ni pabaya kwahio kwa huu upuuzi usijeniqoute 10 years down the line; sababu nimekuwa nikiendelea kuonya kinachoendelea kinaharibu kazi kubwa sana iliyofanywa na Mababu zetu...
 



Na hayo niliyasema zamani sana..., ila inabakia palepale sisi kama Raia tuna utaifa in comparison na nchi nyingi sana especially USA tunawaacha mbali sana...., Wanasiasa walaghai, walamba asali na uongozi wenye Ombwe hauondoi ukweli huu.... Na hio naongelea leo..., tunapoelekea ni pabaya kwahio kwa huu upuuzi usijeniqoute 10 years down the line; sababu nimekuwa nikiendelea kuonya kinachoendelea kinaharibu kazi kubwa sana iliyofanywa na Mababu zetu...
Nikupuuze tu kwasababu sidhani kama hata una uwelewa wa nini maana ya utaifa.
 
Samia ajitafakari yeye kama kweli ni kiongozi apime lugha anazoongea.

Watu walitekwa na kuuwawa akasema ni drama, watu wakatekwa tena na kuuwawa akasema kifo ni kifo.

Huu mgawanyiko alioleta leo sasa kauwawa kiongozi wa CCM nenda katika kurasa ya X ya CCM uone kauli watu wanazotoa.

Tuendako sasa ni kuwa raia wataanza kuchukua sheria mkononi tu kwa hawa watekaji na siku sio nyingi tutakuja kusikia raia wameua askari aliyekuja kuteka mtu.
 
Back
Top Bottom