Irene Darton
Member
- Feb 25, 2024
- 18
- 22
Na Mwandishi Wetu - Ngorongoro
Imethibitishwa kuwa Mbunge Jimbo la Ngorongoro Emmanuel Ole Shangai anatarajia kujiapisha kuwa laigwanan wa kisiasa kwa lengo la kuongeza nguvu yake ya kisiasa kwa kuwa sehemu ya kuchukua nafasi ya Laigwanan wa Afrika Mashariki iliyoachwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge mstaafuwa Jimbo la Monduli Hayati Edward Ngoyai Lowassa.
Baadhi ya Wananchi waliozungumza kwa hasira na mwandishi wetu wameeleza kuwa Lengo la kutaka kupata uongozi huo wa kimila ni kutaka kuongeza nguvu yake kisiasa, kuwa sehemu ya viongozi wa kimasai watakaodai ardhi ya wamasai kupitia Umoja wa wamasai wa Afrika Mashariki (Maasai land) na kupata nguvu ya ushawishi ya kuzuia watu wasihame kutoka ndani ya hifadhi.
Hata hivyo kitendo hicho kimelaaniwa na kudaiwa kuwa huenda kikaibua mgogoro mkubwa katika jamii hiyo kwa kuwa baadhi ya malaigwan hawakubaliani na mchakato wa Emmanuel Ole Shangai wa kujipa uongozi wa kimila kwa kuwa hana sifa za kuwa katika nafasi hiyo na kuwa ndani ya familia moja ya Shangai haiwezi kutoa viongozi wa wawili wa kimila.
Hili inatokana na ukweli kuwa jamii inamtaka Joseph Ole Shanghai ndio apewe uongozi wa kimila ambapo anatarajiwa kusimikwa uongozi wa kimila siku za hivi karibuni.
Aidha, wananchi hao wameeleza kuwa kama suala hilo likiachwa lifanyike litasababisha mgogoro wa kifamilia kwa kuwa ndugu hao watasababisha mpasuko hata katika jamii yao ya kimasai, jambo linaloweza kuchochea machafuko na kutokuelewana kwa jamii husika.