BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego amesema kati ya changamoto walizokutana nazo kwenye shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi katika mkoa huo ni ulevi kwa baadhi ya makarani na upotevu wa vishikwambi.
Amesema vishikwambi sita vilipotea tangu kuanza kwa kazi hiyo Agosti 23 mwaka huu lakini tayari vinne vimepatikana.
Akizungumza leo Jumapili Agosti 28, 2022 mjini Iringa, Dendego amesema hadi kufikia jana zaidi ya kaya 200,000 tayari zilikuwa zimeshahesabiwa.
"Changamoto tulizokutana nazo wakati wa sensa ni ulevi kwa makarani na upotevu vishikwambi 6, lakini tayari tumedhibiti na vinne vimeoatikana," amesema.
Ameeleza kuwa lengo la Serikali ni kuona kuna mabadiliko ya mifumo hivyo Sensa ya Watu na Makazi itasaidia kuleta maendeleo endelevu.
"Watu wa Iringa endeleeni kuonyesha ushirikiano kwa makarani wa Sensa ili tupate takwimu sahihi," amesema Dendego.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamesema kwa sababu imetumia siku nyingi, wana uhakika wote watafikiwa.
"Binafsi nilishinda nyumbani kama siku mbili nawasubiri, naamini leo au kesho watakuja kutuhesabu kwa hiyo sina wasiwasi," amesema Rahel Mgeni, mkazi wa Kihesa.
Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoa wa Iringa, Peter Milinga amesema kazi bado inaendelea na kuwataka ambao bado hawajahesabiwa kuwa watulivu.
"Kila mmoja atahesabiwa, tupo kwenye hatua ya mwisho kabisa kwa hiyo ambao bado wasijali," amesema.