Ulevi Unaninyima Amani. Ninaomba Msaada wenu

1. Tafuta marafiki ambao sio walevi
2. Jiunge na kwaya kanisani au uwe mtu wa ibada iwe Islamic au kristo
3. Tafuta KAZI ya kukuweka busy muda wote
4. Panga sehemu ambayo Haina bar Wala vilub vya pombe
 
Mkuu hii habari ya LIMIT ukishafikia levo ya uraibu ni haipo, ukisema ukaonje tu umeharibu! binafsi nimepambana sana na hili swala la LIMIT kwa miaka sasa ili nibaki kuwa mnywaji wa bia 2,3 lkn wapi! nikishaonja ya kwanza na ya pili ni kama ndio zinaamsha mzimu wa pombe, hivyo nitakunywa siku nzima niko bar na kutoa offer za kutosha kiasi kwamba kama nilibeba laki moja itaisha na benki naenda tena na tena...So ili niwe salama, ni bora nisionje kbs na nashukuru sina ile tabia ya kuzimiss pombe so naweza kaa hata mwezi na hicho ndo kinaniokoa...NB; Wanywaji wachache sana wanaweza kuwa na LIMIT.
 
Mimi Nina limit sababu uki abuse alcohol kesho una amka na hang over kichwa kinauma yanini yote hayo huwa nakunywaga Ile konyagi,black level, hason choice ndogo moja inatosha.

Kama inakupeleka puta ni Bora kuacha kabisaa
 
Mimi kwa upande wangu, nilianza kwa kujitenga na marafiki walevi, pia niliweka nia ya kutokwenda kwenye vilabu vya pombe hata nikitoka naenda sehemu ambazo mara nyingi hawana vilevi. Kubwa zaidi nililolifanya kushinda tamaa za mwili kama ulevi, uzinzi, uvutaji wa sigara ni kufunga na kuomba. Mwanzoni ni ngumu ila ukianza kwa kutenga walau siku 3 za kufunga kwa wiki utafanikiwa.
 
Bora umekiri mwenyewe, nenda Kanisani katubu dhambi zako au Msikitini, mrudie Mungu wako, usijaribu kutumia waganga kuacha pombe utakufa!!

Muda wa kunywa pombe we kunywa maziwa, utashinda
Pombe zinahusiana nini na kanisani?
 
Miiko mitatu ya pombe itakayokusaidia maishani
Kila unywapo pombe kumbuka haya
1. Wewe ni nani
2.Uko wapi
3. Unafanya nini
Ukiona huwezi kuyakumbuka hayo acha pombe mara moja
Nakubaliana na wewe kaka mkubwa.
 
Owa maana zile kero za kuulizwa kila muda uko wapi? Umeeanza teena mipombe yako, kununiwa mwisho utaacha kabisa.
 
Umeshafikia kiwango cha addiction. Ni ngumu sana kuacha. Inahitaji neema ya Mungu tu.
Nina kaka yangu alianza kujifunza kunywa pombe akiwa kidato cha 2. Akawa anakunywa kidogo kama starehe tu. Tulimsihi sana aache maana akishazoea hatoweza kuacha. Lakini alitubishia akiamini akiamua tu anaweza kuacha. Mwisho wa siku akangukia kwenye ulevi. Yaani sasa anakunywa chochote. Haya mataptap ndio ana uwezo nayo. Familia haijali tena. Watoto wake tumewachukua baada ya kuona hali ni mbaya zaidi. Mkewe akarudi kwao. Sasa anaweza kukaa hadi siku 4 hajala. Anakunywa tu pombe ya mataptap, gongo, n.k. sasa amejikatia tamaa maisha.

Kamwe usijifunze kuonja pombe ukiamini utaweza kuacha ukiamua. Never. Hata hao wanaosema wameacha ukwel ni kwamba wamepumzika tu. Yakija kutokea mazingira ya ushawishi wanarudia tena. Ni suala la muda tu.
 
Wakuu salam,hivi MTU unaweza jipeleka soba house mwenyewe.?
Mimi nilijua watu wanapelekwa either serikali,marafiki au familiya zao
 

Pole sana kaka.
Nina vitu vitatu vya kukushauri ufanye ila kwa iman.
1. Kama unaamini uganga tafta mganga wa kweli atakusaidia kujua shida yako
2. Kama una amini mungu nenda kanisani tube na utakacho kiomba cache kiache kabisa.
3. Kama umeoa jadili na mkeo hilo jambo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…