Ulianza lini kupenda na kufuatilia Siasa?

Ulianza lini kupenda na kufuatilia Siasa?

katika mazingira tofauti tofauti, mathalani mitandaoni, vyuoni na majukwaani kuna aina tofauti tofauti za wanasiasa na siasa. wapo vijana katika siasa, wazee, wanawake kwa wanaume.

wapo wanataaluma wa siasa za kitaifa na kimataifa. Lakini pia wapo wasio na taaluma bali vipaji na utashi wao tu kupenda na kuingia kufanya siasa..

Na katika makundi yote ya wanasiasa, wapo wanao weza kudhibiti hisia zao za kisiasa vema sana, na wengine bado ni dhaifu katika kujizuia na kuwastahimili wale wenye maoni na mitazamo tofauti na yao kisiasa...

na kwahivyo,
utashi, hekima na busara katika kujenga na kutetea hoja dhidi ya upande wenye utofauti wa maoni na wengine, imekua ni miongoni mwa vipimo muhimu sana kubainisha ukomavu wa kisiasa wa mwanasiasa husika, achilia mbali msimamo 🐒

nini kilikuchochea,
nini kilikuvutia na kukusababisha kuamua kufuatilia siasa katika kiwango hicho ulichonacho sasa?

uliwezaje kua katika hali hiyo ya ukomavu uliojaa ustahimilivu, hekima, busara na subra licha ya maoni na mitazamo ya wengine kua tofauti na wako vikiambatana na kejeli, mizaha, ghadabu na pengine matusi ya nguoni dhidi yako?🐒

tafadhali shirikisha uzoefu wako JF fraternity inufaike na maarifa hayo muhimu kuepuka lugha na mambo yasio faa katika siasa na tuwe wastahimilivu na wenye subra kama wewe na hatimae sote kwa pamoja tufanye siasa za kistaarabu 🐒
Tangu darasa la tatu mwaka 1987.Kilichonivutia kwanza ni walimu wangu,pili Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea,tatu Ahadi Kumi za Mwana TANU,Lugha ya Kiswahili na nchi yangu pendwa Tanzania.
 
wew una kipaji tu, na actually unafundishika kirahisi 🐒

ungekua mwanataaluma wa siasa uelewa na ufahamu wako katika siasa ungekua ni zaidi ya kujua kwamba mpira ni siasa .....

ungejua kwamba kule kwenye nyumba za ibada ni siasa inafanyika, inaitwa religious politics, kule kwenye family yako ni siasa inafanyika, inaitwa family politics, kule kazini kwako ni siasa inafanyika, ukiwa shuleni ni siasa inafanyika, huko kwenye mpira n.k

ndio maana tunasema siasa ni maisha....

ndio maana Aristotle alisema human being are political animals...

kwamba huwezi epuka siasa maishani mwako upende usipende 🐒

mipango yako yote maishani na maamuzi yako ni pure politics, ndio maana unaweza mwanmbia mwenzio ntakupigia cm baadae na usipige wala kutuma meseji ...🐒
Mie nazungumzia siasa katika mtazamo(angle) uliokuja nao wewe mleta mada.
Huwezi kuniambia maisha ni siasa halafu muda huo huo unaniambia nilianza kupenda lini siasa?

Ulianza lini kupenda na kufuatilia SIASA?​

 
Mie nazungumzia siasa katika mtazamo(angle) uliokuja nao wewe mleta mada.
Huwezi kuniambia maisha ni siasa halafu muda huo huo unaniambia nilianza kupenda lini siasa?

Ulianza lini kupenda na kufuatilia SIASA?​

so,
nawe mwanataaluma sio?

maana ni nadra mwanataaluma kuikana siasa aina yoyote ile, ila kwa mazingira ya sasa definitely a feel hii ya majukwaani na si vinginevyo 🐒

hata na hivyo si mbaya.....
natafuta uzoefu wa jinsi ya kufanya siasa safi blia kumdhihaki mwingine kwa maneno ya kuudhi au mabaya 🐒
 
Back
Top Bottom