Nilisubiri miaka 7 tangu kupata ajira kwa kuhofia kuanza, maana kila mtu aliniambia ujenzi ni ghali ingawa ni hao hao ambao walishakuwa wamejenga au wanajenga, for some unknown reason walinifanya nione kama sitaweza, nikiuliza bajeti estimates zao zilikuwa juu sikujua naanzia wapi. Nikafikia sehemu nikachukia kabisa kupanga. Nikaenda bank kuchukua mkopo. Kiwanja kipo sehemu tambarare(nilishanunua few years before) so nilifukua tu msingi na kushusha tofali na kuinua nyumba juu bila zile mbwembwe za nondo etc. Mkopo ukaipeleka nyumba hadi kwenye lenta. Pale nikasimama mkopo ukakata. Nikajipanga nikasave mishahara kadhaa na kumalizia kozi 3 za juu. Kisha nikatulia na kuwekeza kwenye bati yaani napeleka kwa mwenye duka kidogo kidogo ananiandikia risiti, yes ni risky, akifa unaweza kuhaha but ilinisaidia. Nilipomaliza nikazichukuwa bati zangu na kuziweka ndani. Nikajichanga na kumaliza bajeti ya mbao nikamwita fundi kwa mkopo. Fortunately ni yule yule aliyejenga boma, akasema nipe hela niwalipe wasaidizi wangu, yeye nilimpa mshahara ulipoingia a month later. Nyumba ikaezekwa. Over the course of several months later nikakamilisha taratibu chumba kimoja tu na Public toilet na milango miwili ya nje. Kabla sijahamia nikapata hela kidogo nikapiga lip kwa ndani vyumba vyote, korido na rough ya chini(hii process ni cheap sana kwenye ujenzi usiogope). Kabla sijaanza kukamilisha hicho chumba kimoja nilikuwa naweka taratibu grills za madirisha kwa ajili ya security, ile room moja ilipokuwa tayari nikaingia maisha yakaendelea, bado sijakamilisha kila kitu ila as we speak nyumba imepigwa chokaa yote, tiles na madirisha yote yamefungwa vioo nilikuwa nafanya hivyo kidogo kidogo. Zaidi zaidi bado washroom ya master bedroom, kupaka rangi na kupamba walls vile wanavyofanya siku hizi, na kuweka furniture mpya. Before nihamie shimo la choo lilikuwa limeshajengwa taratibu hivyo hivyo. Nimeingia nategemes maji ya jirani lakini baadae maji yalipopita kwangu nikayavuta. Ujenzi una vitu vingi vidogo vidogo, ushauri usivipuuzie, mfano kulaza mabomba na kuchimba mfumo wa umeme vinaweza kuonekana cheap lakini ukisema uvipe muda wake utachemka, wewe kwenye ujenzi mkubwa unganisha na hivyo vitu kimoja kimoja ili usiifeel gharama, wakati wanajenga wewe tafuta mtu ajaze udongo ndani. Wakati wanajenga boma tafuta mtu achimbe shimo la choo, wakati wanapaua ongea na fundi uweke grills moja moja kwa kadri ya bajeti. Cha msingi anza, maana ukianza hutaacha, ujenzi una kawaida ya kukufanya uwe focused kila hela utakayopata utaipeleka kwenye boma lako. Kuingia kabla nyumba haijaisha kuna kero lakini pia kunasave hela ya kodi inaelekea kwenye ujenzi. Nina marafiki wana watoto lakini walimanage kuingia hivyo hivyo pia. Hakikisha una chumba kimoja kimekamilika ili kuepuka intrusion ya personal space finishing zinapoendelea. The whole process ilinichukua 3 years tangu kuanza ujenzi hadi kuingia. It is totally doable, ningeanza the moment naanza kazi huenda ningekuwa na nyumba 2 sasa, ya kuishi na ya kupangisha, imagine hela niliyokuwa nalipia kodi!. Pia, kama una uwezo wa kupanda public kwenda kazini please do so, ukisema ununue gari ni bonge la liability, kulihudumia litakurudisha nyuma significantly, nasema hivyo sasa wakati nimenunua gari yangu ya bajeti kabisa mafuta kizibo cha soda, naona kama ingenishika shati sana kama ningekuwa sijajenga. All the best.