Walec
JF-Expert Member
- Apr 22, 2017
- 1,364
- 3,326
- Thread starter
- #2,341
Mkuu picha niliweka juu huko...pita vzr kweny uzi...au jion nikirud naweza fanya ustarabu tena..Kwasasa huu ni uzi wangu pendwa....leteni visa tupate motivation zaid
Mkuu Walec ukiwa kama cr wa huu uzi...
1. picha ya getto lako ihusike kimtindo ili kuleta hamasa zaidi.
2. Hebu tiririka kuhusu buying online na jinsi gani mtu anaweza save costs..Manake kuna vitu tunanunua kwa waha kwa gharama kubwa kumbe tungeagiza kwa bei cheap...Nawezaje nikaanza kutumia hizo application..tiririka please
Kuhusu kununua vitu online na jinsi utavyo weza piga hela..iko hivi
Wenzetu vitu kule ni bei chee sana..hasa masoko ya china...sana sana AliExpres...
Kitu unachotakiwa kufanya ni kufungua account huko kisha kujaza details zako za msingi na address yako ili kupokea mizigo yako..
Baada ya hapo utaingia sokoni sasa na kutafuta bidhaa ambazo ww unahis bongo zinasoko...utaweka order zako hapo na utalipia kisha shipping itafanyika..
Sasa uzuri wa haya masoko licha yakua na bei ndogo za bidhaa pia kuna misimu ya offa..yani hapa ndo unajibebea kapu zima[emoji1787]...mfano kuna offa kama black friday,11.11 , anniversary sales na zingine kibao..misimu hii yani vitu vinashuka bei sana...
Kwaiyo kitu huwa nafanya nasubirig hizi offa zije kisha nanunua items kibao hata kama sina mteja...vikifka bongo ndo naanza kuvipush..yani havikai watu wanavigombania..
Nimeanza kufanya hii biashara in a small scale ili kugain experience yakutosha kwanza..lakin nawaza kuifanya kwa ukubwa hapo badae kidogo...
Lakin pia ukiacha zile offa za misimu nilizozitaja pia kuna coupon zipo..zinatolewa free..ukiwa mjanja unakusanya tu coupon kisha wakat wa manunuzi zile coupon zinaleta discount...na pia kuna kitu kinaitwa promocode..hizi ni code flani nazo huwa zinatolewa...nazo ukizijaza sehem ya promocode wakat wa manunuzi huwa zinakupa punguzo la bei hivyo inakufanya upate bidhaa kwa bei rahis sana..
Kwaiyo faida inapatika nzuri tu...mfano bongo simu za xiaomi mfano redmi note 8 zlikua zinauzwa 550..wakati kipind nanunua mm online zilkua 350 tu...so mim nikawa nauza kwa 450 bdala ya 550 bei ya bongo..so faida yangu 100k sitaki tamaa..hapo unakuta nimenunua simu tatu au mbili tu kibingwa..
Lakin kuna watu pia huwa nawaagizia..so wao wananilipa tu hela ya kuagiza...sikosi 20 au 30 depends na kitu anachoagiza...na hapo hapo mtu ninapo muagizia nakua mjanja natafuta coupon, promocode na seller mwenye bei nzuri basi napata chajuu tena..
All in All nimeua [emoji3]
Kama utapenda kujifunza jinsi ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao basi nitaweka link ya group la telegram lenye kutoa hayo mafunzo mpaka naww uweze kua gwiji wa Manunuzi ili kusudi ujikwamue na maisha ya gheto....
The funny thing saizi karbia item kibao sinunui tena kariakoo...yani mm mpaka usb nanunua china[emoji16]....nina vitu wana wakija..huwa wanshangaa nimevipata wapi..basi nawambia nipeni hela hiyo mnivue..basi wananipa kweli naagiza vingine [emoji3]...
Life is funny my brothers [emoji3]
NB kam kuna mtu atapenda kufunza basi aseme nami bila hiyana nitawapa link ya mafunzo..ipo telegram..bure kbisa