Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

wakati nipo chuo, nilikuwa tayari nimenunua assets za kuanzia maisha, hapa namaanisha vitu ambavyo mtu anaweza kuanza maisha akiwa na mke kabisaa, yaani ni beba tubebe, nikaviweka home, na plan yangu ilikuwa nikimaliza chuo ambapo nilikuwa nakaa daharia (hostel) niende kwenye nyumba ya urithi ambayo mzee alituachia,

bahati mbaya ama nzuri, nyumba ilikuwa na ugomvi, kwa sababau mzee wangu alikuwa na mke zaidi ya mmoja, kwa vile mama yangu alitangulia mbele ya haki takriban miaka 16 iliyopita, mama wa kambo ambae pia ni mama wa mdogo wangu alikuwa na vibweka juu ya pesa ya kodi ya nyumba ile, na hivo kutaka kukata shauri juu ya naye kunufaika, jambo moja ni kwamba, nimemuita mke kwa kua alishazaa na baba yangu, ila hakuwa mke wa ndoa.

kabla ya haya yote, nilishawataarifu walezi wangu (ndugu wa baba yangu) ambao ni shangazi pamoja na baba mdogo kwamba ningehamia na kuanza maisha hapo, habari hii ilikuwa ngumu kwao kumeza, japo nikiri tu kwamba kwa kipindi hiko walikuwa na nguvu ya kusema "ndio" ama "hapana" nami, nikatii.

tuachane na hayo, suala ni hili baada ya kumaliza chuo, amini usiamini, pale nilipokuwa naishi, yaani kwa baba yangu mkubwa, aliyenilea tangu mtoto, walizifanya assets zangu zote kuwa za nyumbani, yani nikakuta madogo wamefunga kitanda wanalalia vizurii kabisa, na wengine vikojozi walikuwa wameshaanza kuwakilisha, set yangu ya masofa ndio hivo tena watu wanalindima nayo, nikakuta mpaka kabati imepigwa polish, wameweka na vyombo, mixa mashuka yangu kujigubika, niliumia sana, hapo sina pa kuanzia, nikaona isiwe shida................

na kaelimu kangu ka ualimu, nilianza kujitolea shule moja mitaa ya ubungo, bila malipo nikakomaa nikijua kuna siku natoboa, mpaka ilipofika mwezi wa 12 mwaka 2019, sina hata mshahara wa 20k kwa mwezi, naenda ila silipwi, ilikuwa ni mwalimu wa somo husika ananipa tuu 2k, 5k itategemea ameamkaje siku hiyo, ilikuwa shughuli pevu, kutoka napokaa mpaka napofundisha ni kama 6km hivi, kwa hivo sometimes nilikuwa napiga ngondi.............

nikaamua kuhama mitaa niliyokuwa nakaa, nkahamia mbezi kwa shangazi yangu, sina hata kikombe wala kijiko, nimekaa pale huku naendelea kujitolea kule kule, ilikuwa ni kasafari karefu, magari mawili mpka napofika kazini, na kurudi jumla 4, kuna muda nikawa siendi................

asikwambie mtu, ukishakuwa above 20, kuna ka aibu kanakutafuna pindi unarudi home, unakuta kuna hot pot ya ugali na kidume hujatafuta hata pilipili hoho, nikaanza udalali, nimefanya kwa miezi kadhaa, na vile korona ilifunga shule, udalali ulikuwa umekolea, lakini cha kushangaza all that time sikuwa na smart phone (hata napoandika sasa hivi), nilipokuwa chuo nilinunua assets za saluni pia, yaani complete, ni kwa hela ya boom tuu, kwa muda huu sasa nikaamua kuviuza nipate simu nzuri ya kufanya hiyo kazi, kuna muda madili yakikubali unapata kitu, amini usiamini siku moja nikaotea dili ya 100,000/= ndio pesa niliyonunulia godoro ya inch 8 kwa jamaa wangu, nikaishusha kulee kwenye ghetto la urithi, nikanunua na pallets za shilingi 20....(kitanda tayari)

kuna muda kodi ilitoka hapo, nikapokea, japo ni kidogo, lakini nikajivuta kariakoo kidume kubeba mashuka, na mapazia, hivi sasa nikaviweka kwa mwanangu mmoja hivi, vilikaa kitambo tangu mwezi wa Septemba 2020, awamu hii sasa nikasema sitaki kusikia la mtu, lazima nihamie kwenye gheto langu, nikakusanya kusanya pesa kubeba vitu vingine, amini usiamini, nikauza kasimu kangu, nikaenda pale gheto, nikagawa sebule kati kati, yaani nikagawa pamoja na plywoods lengo langu nikaanze maisha, nimeshachoka kukaa kwa aunt, mbaya zaidi ilikuwa nalala ndani ya net ya kutandaza chini, nilijiona mjinga sana, wakati huo mwezi wa 10 nimetoka kusimamia uchaguzi, nikanunua jiko, na vyombo, yaani hapa sasa geto lilibaki mlango tuu, mwanaume nitimbe, suala la kula ningejua pa kula huko mbele ya safari, mwezi wa 12, nikaanza kuzungusha CVs kwenye mashule kibao, yaani mpaka kibaha, shule nyingine sikujua endapo napata nafasi nafikaje, ikawa balaa, mwezi wa 1 nikaendelea kujitolea kule kule, na hivi nilisikia majina yetu yamechukuliwa na TAMISEMI basi hapo nikasema, mambo ndo haya, nikaendelea kukomaa, mwezi mzima ukapita holaa, nikasema liwalo na liwe, naamia mwezi wa pili, hata bila mlango fresh tuu ntaweka hata kitambaa

tarehe 28, mwezi wa 2, inaingia simu shule moja mitaa ya kibamba, kwamba nahitajika kufanya interview, wakati huo nimekata tamaa ya kufundisha, nikajinyanyua kesho yake kwenda kwenye interview, kwa kuwa tulikuwa kama 10 hivi, nikasema kabisa, siwezi kutoboa, ila nikajipa moyo kwamba, wengi niliofanya nao interview pale ni freshers, hawana uzoefu, bila kuzingatia kuna issue kama board-interest au nepotism, siku mbili zikapita bila simu yoyote, nikaona hapa 0-0 niendlee na mambo yangu, nikapigiwa simu tarehe 2/2 nahtajika shuleni, hapo nipo kwa msuguri naelekea Ilala boma kwenye kesi ya dogo, nika diverge kwenda kuitikia simu, nafika kule nikajikuta nipo na director wa shule tuna jadiliana mshahara, yaani sikutaka mambo mengi, hela aliyotaja nikamwambia tupige kazi babaaa, nikazama mfukoni kwa aunt, nikamtonya,a akanieelewa, nikapiga kazi baada kama ya siku 17, nikapata half-salary, nikaaga tu nyumbani kwamba mwisho wa mwezi, nacheza, ulipofika nikalipa tu dereva wa kunibebea vitu vyangu, kwisha habari yake shughuli ikaanza hapho...... hivi navoongea nipo ghetoo, bado halipo stable in such, ila nina amani kwa kweli, japo moyo unaniambia niweke demu, ila najua kwa sasa hili ni pepo tuu..........................

USHAURI: Suala ni kuanza tuu, ukiamua na ukiondoa hofu, inawezekana.

ingawa ndio naanza, naamini MUNGU wangu ananiona, ntazidi kumea na siku moja nami nitaitwa baba mwenye nyumba kwa nyumba ya mikono yangu mwenyewe, sio kurithi
saluti brother...set ya sofa ulinunua bei gani?
 
Duuuh mbona cheap hivyo...ni sofa zenyewe kali zile kama za carpet au za vitambaa..ningepata picha ingependeza mkuu au connection maana mimi nahitaji hizo vitu na nipo Tabata
Mimi nilimpa pesa baba yangu mdogo, akaniletea, ni sofa nzuri since 2017 wanakalia na bado nzima, ni ya watu watatu, na kimoja cha watu wawili, mito ya box, picha haitawezekana mana sipo kule siku hizi.
 
Mkuu picha niliweka juu huko...pita vzr kweny uzi...au jion nikirud naweza fanya ustarabu tena..

Kuhusu kununua vitu online na jinsi utavyo weza piga hela..iko hivi

Wenzetu vitu kule ni bei chee sana..hasa masoko ya china...sana sana AliExpres...

Kitu unachotakiwa kufanya ni kufungua account huko kisha kujaza details zako za msingi na address yako ili kupokea mizigo yako..

Baada ya hapo utaingia sokoni sasa na kutafuta bidhaa ambazo ww unahis bongo zinasoko...utaweka order zako hapo na utalipia kisha shipping itafanyika..

Sasa uzuri wa haya masoko licha yakua na bei ndogo za bidhaa pia kuna misimu ya offa..yani hapa ndo unajibebea kapu zima[emoji1787]...mfano kuna offa kama black friday,11.11 , anniversary sales na zingine kibao..misimu hii yani vitu vinashuka bei sana...
Kwaiyo kitu huwa nafanya nasubirig hizi offa zije kisha nanunua items kibao hata kama sina mteja...vikifka bongo ndo naanza kuvipush..yani havikai watu wanavigombania..

Nimeanza kufanya hii biashara in a small scale ili kugain experience yakutosha kwanza..lakin nawaza kuifanya kwa ukubwa hapo badae kidogo...

Lakin pia ukiacha zile offa za misimu nilizozitaja pia kuna coupon zipo..zinatolewa free..ukiwa mjanja unakusanya tu coupon kisha wakat wa manunuzi zile coupon zinaleta discount...na pia kuna kitu kinaitwa promocode..hizi ni code flani nazo huwa zinatolewa...nazo ukizijaza sehem ya promocode wakat wa manunuzi huwa zinakupa punguzo la bei hivyo inakufanya upate bidhaa kwa bei rahis sana..

Kwaiyo faida inapatika nzuri tu...mfano bongo simu za xiaomi mfano redmi note 8 zlikua zinauzwa 550..wakati kipind nanunua mm online zilkua 350 tu...so mim nikawa nauza kwa 450 bdala ya 550 bei ya bongo..so faida yangu 100k sitaki tamaa..hapo unakuta nimenunua simu tatu au mbili tu kibingwa..

Lakin kuna watu pia huwa nawaagizia..so wao wananilipa tu hela ya kuagiza...sikosi 20 au 30 depends na kitu anachoagiza...na hapo hapo mtu ninapo muagizia nakua mjanja natafuta coupon, promocode na seller mwenye bei nzuri basi napata chajuu tena..

All in All nimeua [emoji3]

Kama utapenda kujifunza jinsi ya kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao basi nitaweka link ya group la telegram lenye kutoa hayo mafunzo mpaka naww uweze kua gwiji wa Manunuzi ili kusudi ujikwamue na maisha ya gheto....

The funny thing saizi karbia item kibao sinunui tena kariakoo...yani mm mpaka usb nanunua china[emoji16]....nina vitu wana wakija..huwa wanshangaa nimevipata wapi..basi nawambia nipeni hela hiyo mnivue..basi wananipa kweli naagiza vingine [emoji3]...

Life is funny my brothers [emoji3]

NB kam kuna mtu atapenda kufunza basi aseme nami bila hiyana nitawapa link ya mafunzo..ipo telegram..bure kbisa
hz biashara za online zina mambo sana bro. siku za nyuma nishawahi kuagiza vioo viwili vya samsung J5.(kwa lengo la kuja kuuza bongo) . nilijaribu kutafuta vya bei rahisi ali Express nkapata vya 45000 kila kimoja. nikaagiza viwili. vioo vimefika bongo natangaza sipat wateja asee. nkaamua kwenda kariakoo nikawauzie mafundi smu, duh ile nawaambia nauza kioo! wakanambia mbna hki kioo ni namba 2 (yaan ni copy) na sisi tunaviuza kwa 35000 tu!!! Asee nilichoka ikawa mwisho kuagza
 
Kufupisha story ni kwamba gari ile niliifanya uber kipindi hicho ndo uber imeanza hope nilizisha mapambano kwani nlikuwa nahakikisha nalaza laki kila siku ya mungu na wife wakati yupo na ujauzito mkubwa akaajiri mtu wa kusambaza vitu vyake kwa wateja huku na mimi nikisambaza vyangu kwa gari huku wakati mwengne nikimsambazia na yeye,mwisho wa siku nilifungua duka ambalo wife baada a kujifungua akawa ndo msimamizi na pia deni la mzee la 20k kila siku nililitimiza na mwisho wa siku gari ikawa yetu,nakumbuka siku ya harusi babamkwe akatupa kiwanja kwa ksema altupa mtihani wa kujinunulia wenyewe means ile hela tulokuwa tunampa kila siku aliitu za na kutununulia zawadi ya kiwanja huk nasi tukiwa na vingine vitatu hiyo ndo story yangu ya geto ambayo imenipa mke na nyumba ambayo naimalizia now,watoto wangu mapacha,pamoja na gari 3,maduka na biashara nyingine na kunifanya nisahau kuajiriwa japo nna degree yangu ya first class
Pesa ya board umelipa.?
 
daa umefanya uzembe kama wangu,nikiwa shule nilikua nakaa na manzi tukanunua kila kitu kwa malengo baada ya shule tuanze maisha.

akiba tukiwa na m.1 na laki 6, uoga kitu cha ajabu sana nikaona ntafanya nini nikala kona kurudi home nikamuachia manzi kila kitu. alinililia sana nirudi ila ule uoga haukuwa wa nchi hii

now nimepanga ila najilaumu sana kumkimbia yule manzi kwa uoga wa maisha mji wa watu
Ungekuwa mbali sana aseee
 
Kama unaweza vp njoo tujivinjari lkn jee unaweza kuulumangia ugali na kachumbariView attachment 1753143
20170710_150235.jpg
 
Back
Top Bottom