wakati nipo chuo, nilikuwa tayari nimenunua assets za kuanzia maisha, hapa namaanisha vitu ambavyo mtu anaweza kuanza maisha akiwa na mke kabisaa, yaani ni beba tubebe, nikaviweka home, na plan yangu ilikuwa nikimaliza chuo ambapo nilikuwa nakaa daharia (hostel) niende kwenye nyumba ya urithi ambayo mzee alituachia,
bahati mbaya ama nzuri, nyumba ilikuwa na ugomvi, kwa sababau mzee wangu alikuwa na mke zaidi ya mmoja, kwa vile mama yangu alitangulia mbele ya haki takriban miaka 16 iliyopita, mama wa kambo ambae pia ni mama wa mdogo wangu alikuwa na vibweka juu ya pesa ya kodi ya nyumba ile, na hivo kutaka kukata shauri juu ya naye kunufaika, jambo moja ni kwamba, nimemuita mke kwa kua alishazaa na baba yangu, ila hakuwa mke wa ndoa.
kabla ya haya yote, nilishawataarifu walezi wangu (ndugu wa baba yangu) ambao ni shangazi pamoja na baba mdogo kwamba ningehamia na kuanza maisha hapo, habari hii ilikuwa ngumu kwao kumeza, japo nikiri tu kwamba kwa kipindi hiko walikuwa na nguvu ya kusema "ndio" ama "hapana" nami, nikatii.
tuachane na hayo, suala ni hili baada ya kumaliza chuo, amini usiamini, pale nilipokuwa naishi, yaani kwa baba yangu mkubwa, aliyenilea tangu mtoto, walizifanya assets zangu zote kuwa za nyumbani, yani nikakuta madogo wamefunga kitanda wanalalia vizurii kabisa, na wengine vikojozi walikuwa wameshaanza kuwakilisha, set yangu ya masofa ndio hivo tena watu wanalindima nayo, nikakuta mpaka kabati imepigwa polish, wameweka na vyombo, mixa mashuka yangu kujigubika, niliumia sana, hapo sina pa kuanzia, nikaona isiwe shida................
na kaelimu kangu ka ualimu, nilianza kujitolea shule moja mitaa ya ubungo, bila malipo nikakomaa nikijua kuna siku natoboa, mpaka ilipofika mwezi wa 12 mwaka 2019, sina hata mshahara wa 20k kwa mwezi, naenda ila silipwi, ilikuwa ni mwalimu wa somo husika ananipa tuu 2k, 5k itategemea ameamkaje siku hiyo, ilikuwa shughuli pevu, kutoka napokaa mpaka napofundisha ni kama 6km hivi, kwa hivo sometimes nilikuwa napiga ngondi.............
nikaamua kuhama mitaa niliyokuwa nakaa, nkahamia mbezi kwa shangazi yangu, sina hata kikombe wala kijiko, nimekaa pale huku naendelea kujitolea kule kule, ilikuwa ni kasafari karefu, magari mawili mpka napofika kazini, na kurudi jumla 4, kuna muda nikawa siendi................
asikwambie mtu, ukishakuwa above 20, kuna ka aibu kanakutafuna pindi unarudi home, unakuta kuna hot pot ya ugali na kidume hujatafuta hata pilipili hoho, nikaanza udalali, nimefanya kwa miezi kadhaa, na vile korona ilifunga shule, udalali ulikuwa umekolea, lakini cha kushangaza all that time sikuwa na smart phone (hata napoandika sasa hivi), nilipokuwa chuo nilinunua assets za saluni pia, yaani complete, ni kwa hela ya boom tuu, kwa muda huu sasa nikaamua kuviuza nipate simu nzuri ya kufanya hiyo kazi, kuna muda madili yakikubali unapata kitu, amini usiamini siku moja nikaotea dili ya 100,000/= ndio pesa niliyonunulia godoro ya inch 8 kwa jamaa wangu, nikaishusha kulee kwenye ghetto la urithi, nikanunua na pallets za shilingi 20....(kitanda tayari)
kuna muda kodi ilitoka hapo, nikapokea, japo ni kidogo, lakini nikajivuta kariakoo kidume kubeba mashuka, na mapazia, hivi sasa nikaviweka kwa mwanangu mmoja hivi, vilikaa kitambo tangu mwezi wa Septemba 2020, awamu hii sasa nikasema sitaki kusikia la mtu, lazima nihamie kwenye gheto langu, nikakusanya kusanya pesa kubeba vitu vingine, amini usiamini, nikauza kasimu kangu, nikaenda pale gheto, nikagawa sebule kati kati, yaani nikagawa pamoja na plywoods lengo langu nikaanze maisha, nimeshachoka kukaa kwa aunt, mbaya zaidi ilikuwa nalala ndani ya net ya kutandaza chini, nilijiona mjinga sana, wakati huo mwezi wa 10 nimetoka kusimamia uchaguzi, nikanunua jiko, na vyombo, yaani hapa sasa geto lilibaki mlango tuu, mwanaume nitimbe, suala la kula ningejua pa kula huko mbele ya safari, mwezi wa 12, nikaanza kuzungusha CVs kwenye mashule kibao, yaani mpaka kibaha, shule nyingine sikujua endapo napata nafasi nafikaje, ikawa balaa, mwezi wa 1 nikaendelea kujitolea kule kule, na hivi nilisikia majina yetu yamechukuliwa na TAMISEMI basi hapo nikasema, mambo ndo haya, nikaendelea kukomaa, mwezi mzima ukapita holaa, nikasema liwalo na liwe, naamia mwezi wa pili, hata bila mlango fresh tuu ntaweka hata kitambaa
tarehe 28, mwezi wa 2, inaingia simu shule moja mitaa ya kibamba, kwamba nahitajika kufanya interview, wakati huo nimekata tamaa ya kufundisha, nikajinyanyua kesho yake kwenda kwenye interview, kwa kuwa tulikuwa kama 10 hivi, nikasema kabisa, siwezi kutoboa, ila nikajipa moyo kwamba, wengi niliofanya nao interview pale ni freshers, hawana uzoefu, bila kuzingatia kuna issue kama board-interest au nepotism, siku mbili zikapita bila simu yoyote, nikaona hapa 0-0 niendlee na mambo yangu, nikapigiwa simu tarehe 2/2 nahtajika shuleni, hapo nipo kwa msuguri naelekea Ilala boma kwenye kesi ya dogo, nika diverge kwenda kuitikia simu, nafika kule nikajikuta nipo na director wa shule tuna jadiliana mshahara, yaani sikutaka mambo mengi, hela aliyotaja nikamwambia tupige kazi babaaa, nikazama mfukoni kwa aunt, nikamtonya,a akanieelewa, nikapiga kazi baada kama ya siku 17, nikapata half-salary, nikaaga tu nyumbani kwamba mwisho wa mwezi, nacheza, ulipofika nikalipa tu dereva wa kunibebea vitu vyangu, kwisha habari yake shughuli ikaanza hapho...... hivi navoongea nipo ghetoo, bado halipo stable in such, ila nina amani kwa kweli, japo moyo unaniambia niweke demu, ila najua kwa sasa hili ni pepo tuu..........................
USHAURI: Suala ni kuanza tuu, ukiamua na ukiondoa hofu, inawezekana.
ingawa ndio naanza, naamini MUNGU wangu ananiona, ntazidi kumea na siku moja nami nitaitwa baba mwenye nyumba kwa nyumba ya mikono yangu mwenyewe, sio kurithi