NA MIMI NGOJA NISHEE KIDOGO NILIANZAJE KUKAA GHETTO
Sikuwahi kuamini ntakaa getto labda hadi siku mambo yangu yangekaa sawa na sikujua ni lini [emoji1]...
Kama wewe n kijana ambaye umelose ramani naomba soma hapa...
Baada ya mambo yangu kwenda kombo kuanzia kielimu na kimkakati nikaamua kurudi home.. Aisee aibu hiyo usiombe coz kero n nyingi dharau kama zote... Halafu michongo ikawa haisongi kabisa washikaji zangu wengi wako mikoa mingine, wengine washaoa na wengine wana michongo kadha wa kadha dah. Wakati Mimi sina A wala B..
Basi mwaka huu mwezi wa sita nikapiga dili za hapa na pale nikapata vilaki kadhaa nikaapa safari hii sifanyi biashara yyt bora nipange geto langu tu hata kama ntakua nalala njaa but niwe Huru... Langa aliwahi kuimba bora kurogwa kuliko kukosa Uhuru.. Sasa nilikua nimekereka sana na maisha ya home hata mademu nilikua nikipata wananiuliza hivi unakaa kwenu au umepanga nikisema kwetu inakua tabu wengine nilishindwa kula tunda kimasihara.. Shahidi Riki boy [emoji1][emoji1787]
Basi bana nikapata room tsh 30k per month bahati nzuri huku mkoani n bonge la chumba kwa hiyo bei full marumaru... Na Mimi nilipangilia 60k iwe kwa ajili ya rent nikapay na kuanza life nakumbuka siku ya kwanza nilikua na kitanda tu 4 kwa 6 na dogoro langu la bei chee.. Da hata kuna manzi alinitembelea niliona aibu sana.
To cut a story nashukuru Mungu nimekuwa nikipiga vibarua na kununua baadhi ya vitu vya ndani hadi sasa japo sijafika viwango navyotamani but at least nina amani ya moyo hata mgeni anaweza nitembelea akala akaoga na kulala...[emoji16] Maisha ya home yasikie tu mambo ya kuamushwa kuchota maji au kusafisha uwanja ili Nile ugali wa shikamoo yalinitesa sana... Nashukuru Mungu sasahivi nipo huru now nimejifunza sana maisha hata jero ina thamani sana na pia najichanganya sana kwenye madili mbalimbali sichagui kazi na nshapiga kazi ambazo sikiwahi kuamini kama ntazimudu[emoji6][emoji23]... Kubwa zaidi nimepata na mchumba if God wish tutaoana very soon japo nimepitia machungu but final I can smile now... Niishie hapo.. Kijana usiogope kutoka nyumbani Mungu atakupigania niseme tu ukweli ukiwa home huwezi pata akili ya kufight maisha yaani hizo harakati nazopiga ili nisifukuzwe nilipopanga ningezipiga wakati nipo home basi ningekua mbali mno.... Na mengi sana ya kusimulia but niishie hapa kwa leo.
Mungu ni muweza
Cc Wakipekee