Ulianzaje kukaa gheto?

Safi mkuu
 
Wakuu mm nataka panga geto ila kwa boom la diploma pale dit first year.Nawasilisha kwenu kama inawezekana coz sitalajii kufanya kazi yoyote nategemea boom pekee.Sitarajii kufanya biashara sababu nachukua course ngumu kiasi
Kutegemea boom tu nayo ni kazi hiyo mkuu
 
Nilianza kuishi geto la kujitegemea mwaka 2010 nilikua naishi maeneoya nema kwa mjomba baada ya kumaliza la Saba nikafaulu nikaenda sec myaka miwili nikachemka nikakacha shule na kuja mjini kwa mjomba angu alikua fundi ujenzi nikanza kuzunguka nae kupiga kazi Mimi msaidizi au kibalua yeye fundi katika mishemishe za kujenga sikumoja tukiwa saiti tunajenga alikuja kibalua kuomba kazi akapata yule jamaa alikua rafiki yangu Sana alikua mtu wa iringa alikuja tanga kusoma veta akaniuliza waishi wapi nikamwambia nakaa nema na mjomba akaniambia yeye anachumba twende takakae wote nilishukulu Sana Mana nema mbali Sana na mjini tunapofanya kazi ilikua kila siku ni kusugua pumb tu umbali mlefu basi nikamwambia mjomba nahamia mjini akakubali nikaenda kukaa na yule jamaa myezi mitatu ilipopita jamaa akawa amemaliza veta anataka kulidi kwao iringa akaniambia Kodi imebaki mwezi mmoja Mimi naludi home Baki na geto mwana nikakubali jamaa akasepa akaniachia kigodoro tulichokua tunalali Cha ulimi wa ng'ombe vili vya futi 3 na jiko la mchina na visufulia nikaanza kujitegemea nilikaa kile chumba mpaka nikanunu kiwanja na nikawa tayali nishakua fundi najenga nyumba nikapata vyumba viwili ndo nikahama kwenye ile nyumba na kwangu ukweli sikuwai kubadilisha chumba tangu nianze kupanga pale nashukulu mungu nashi geto langu sasaivi ila geto la pale mjini sito lisahau limenipa mtoto na nimewala Sana wasambaa na wadigo pale tanga Raha Sana buku tu unakula Safi si asubuhi si mchana Wala usiku Yani bajet ya buku tatu tu unashi siku nzima
 
Cha pili ukiwa unaishi geto epuka kumiliki vitu visivyo vya lazima kama makabati masofa sio vitu ambavyo vinafaa Sana kumiliki Kama unaishi chumba kimoja Tena ukiwa unandoto za kujenga nunua vitu vichache tu tena vya muhimu sio unakua na geto Kama dsico mzuki mnene mpaka mwenye nyumba akuchukie
 
Nimejifunza kitu hapa.
 
Aisee mkuu big up sana...kwaiyo totoz unasema ukazitafuna sana? [emoji1787][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Well said hivyo vitu vinafaa kama una chumba na sebule..tena sio vya kuanzia..ni vya badae
 
Mwaka wa korona, nilidhamilia kuhama skan baada ya kuanza kujishughulisha na Michongo ya kuuza nafaka za chakula, nilimfata mother nkamtel,,,,, daaaah,,, ilikua kipengele aisee,,, yaan alikubal kwa shingo upande na baada ya kusepa tyuu Mazaa aliangua kilio[emoji26].

Baada ya korona kupungua na kutangazwa kuwa wa kusoma warudi makambini mwao, nkamwachia jamaa angu geto, baada ya miez kadhaa ya Likizo ckumkuta mshkaji coz alikua kasafir na muda wa kodi ndo unaisha, ikanibidi nisalim amri kwa kurudisha majeshi nyuma[emoji4][emoji4].

Ile natua skani na vitu vyangu, nliwakuta Maza na Fath, daaah Mazaa alicheka balaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787],,, akanitolea na mfano wa kwenye Bible (Mwana mpotevu). Surely ckupenda kurud lkn ilinibidi tyuuu.......!!!!!!

Hapa napanga mipango ya kuset ka_double room house kanguuuuu...[emoji123][emoji123][emoji123]
 
Exactly mkuu...kurudisha sio kufel...set michongo usepe zako..big sana mkuu
 
Wakuu mm nataka panga geto ila kwa boom la diploma pale dit first year.Nawasilisha kwenu kama inawezekana coz sitalajii kufanya kazi yoyote nategemea boom pekee.Sitarajii kufanya biashara sababu nachukua course ngumu kiasi
ukiwa peke yako na kama una support ya ndugu sawa utatoboa, ila kama ndio boom kila kitu support ya ndugu ni chenga basi mcheki mwanao mwenye itikadi kama zako( yan chuo kimoja na course moja) ili mpange, mkiwa wawili cost huwa zinapungua

kuhusu eneo ni nyie tu, Either magomeni, kigamboni au Manzese
 
Yes unachukia vile vya muhimu tu, accessories ndio zitafata baadae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…