Kwa wale ambao tupo magetoni na hatuja ajiriwa napenda kuwatia moyo kua tupambane tu kitaa. Kama huna mishe maalumu piga kazi yoyote ile iliyo halali. (mm sio mdau wa madili haramu, ingawa nilishawahi kufanya baadhi)
Lengo Ni kujitengenezea kipato kitakachofanya uendelee kusurvive maghetoni (pango, na mahitaji mengine madogo. Yaan hapo usichague kazi Kama huna kazi maalumu ilimradi unanguvu, Basi nguvu na akili iwe mtaji wako wa kwanza.
Pia usisahau kutafuta mishe maalumu utakayoitegemea Kama shughuli kuu ya kiuchumi, hii itasaidia kufocus na maisha. Ukiwa na mishe maalumu itakufanya uwe na uchumi flani stable, mfano Kama inakupa laki 300000 kwa mwezi Basi inakua uhakika, yaani inakua stable lazima hicho kiasi kiingie. Hapa pia malengo ya maisha kwa kiasi fulani hua yanafanikiwa au yanakaa sawaa.
Wadau Jambo kubwa usiisahau kuishi vizuri na jamii inayokuzunguka toka kwenye misiba, changia rambirambi, changia shughuli za maendeleo ya mtaa, Kijiji, kata. Maana utahitaji uwepo wao hasa viongozi ikitokea baadhi ya vitu kma umeibiwa, umeugua Sana na ndugu wako mbali, umefiwa, umepata ajali, au majanga ikapelekea kupelekwa polisi n.k. hivyo jamii itakuokoa pia.
Hapo chini ndo mishe zangu nauza mawe ya kujengea.
View attachment 2068429