Ulianzaje kukaa gheto?

Ndugu yan nilipanga kutoka tangu mwezi wa 7....sema kila ikipatikana hela naweka kweny biashara....nataka niwe stable kbsaa...ila mwezi huu afe kipa afe beki....!!am in marathon
Hahah yani make sure unahama kweli..vinginevyo unashangaa mwaka unaisha upo tu...inahtaj commitement kweli...kunakuaga kama na kauzito kutoka
 
Kutokana na masharti ya mzee nilishindwa kuvumilia, kwanza nilitoka kijijini kuja DAR na nikawa nakaa kwa baba mdogo hata chuo pia nilikuwa naenda na kurudi home wakati huo tunakaa buguruni.

Kitu cha kwanza kilichokuwa kinaniboa ni kupangiwa muda wa kurudi home , saa mbili hujarudi utakutana na sms upo wap usiku wote huu, nikiwa kwenye mpira sasa utakuta sms njoo uende mwananyamala kwa shangazi yako upeleke kitu fulani daaah nilikuwa naboreka kupita maelezo ukizingatia ni kwanzaa dakika ya 55 manchester united vs chelsea enzi za kibabu fergie wanaojua mpira watanielewa vizuri hapa.

nilichofanya nikaenda dukani wanapouza vitanda na magodoro nikaongea na muuzaji nilipe kidogo kidogo wakanikubalia, kitanda na godoro nikaambiwa laki tatu na ishirini nikalipa laki na nusu nikapewa risiti nikasepa kwa makubaliano mwezi unaofuata nikamalizie, hiyo mipango nilikuwa naifanya bila mzee kujua .

MUNGU SI ATHUMANI nikamaliza deni kitanda na godoro nikampa mshikaji wangu wa tabata akae navyo nikawa naunga pesa ya kodi ya miezi sita chumba ni 35000 kwa mwezi kwa miezi sita ni 210,000.

Hatimae nikapata chumba na nikakilipia nikahama kwa mzee japo ilikuwa mbinde kukubali nihame kwao lakini nilihama na kujiamulia mambo yangu hata mpira wa saa nne usiku nilikuwa naangalia bila wasiwasi. kukaa kwako unakuwa huru na akili inakomaa sio kukaa kwa baba au mama muda wote.
 
Daahh
 
Mkuu una uandishi mbaya sana,
Jitahidi kuandika kama msomi uliefika Chuo.
 
[emoji38][emoji38][emoji38] we jamaa kiboko....ila nice mkuu umesepa hom...Sasa uyo manz wako akikuta huu uzi utapata tabu mkuu
Ilikuwa kitambo sana hata sasa sijui yupo wapi but ninachojua ameolewa na ana familia
 
Daaah!!nimekumbuka mbali Sana,Yani nimeanza gheto na godoro limechoka Yani unalala mbavu zinauma hadi unaamua kuamka usingizini upumzike kidogo halafu unarudi Tena kulala!!
Hahah pole sana mkuu...ila najua leo sio kama jana
 
Umetisha sana mkuu
 
Mkuu naamini saiz ushasepa [emoji16]
 
Mi mwanzoni sikutaka kuondoka home maana niliona ka sijajipanga. Mzee alinipa kazi ya mshahara ila siku ananipa akaniambia utaondoka baada ya miezi 3. Mi ikapita nikajikausha ila nishanunua vitu vya maandalizi. Siku moja kaniita kaniambia unaondoka kwangu lini. Niliondoka kishingo upande ila nashukuru. I can now stand on my feat. He taught something using the hard way and am proud of his actions thou i had planed to shift after six month. I was waiting to purchase everything.
 
Bless mkuu...mzee alikua mkaksi ila ndio alikua anakuandaa na maisha..
 
Very inspiring....wewe ni mwanaume! Mkeo na wakwe wako ni vifaa vya moto pia! Usisahau kumshukuru Mungu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…