Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Haha.. dah mkuu kwaio manzi aliuza vyombo vyote ulivyomwachia hakukupa ata cent ? Au ghetto lilikua halijashona kiivyo.
angefanyaje ikiwa nilizima simu na kupatikana kimachale

sijawahi muuliza na sita muuliza mana mie ndo huwa mkosaji. kikubwa zaidi sina mawasiliano nae hata fb nilisha m-block
 
angefanyaje ikiwa nilizima simu na kupatikana kimachale

sijawahi muuliza na sita muuliza mana mie ndo huwa mkosaji. kikubwa zaidi sina mawasiliano nae hata fb nilisha m-block
Hehe imeishia[emoji119][emoji119]
 
One of amazing post, people try to explain their beginning transition life fr parents to getto with alot of fun ......real am learning some madini from here.....!!!! Pls more comment[emoji23][emoji23]
Mkuu tunasubr experiance yako [emoji3]
 
2019 hyo inajongea wenye mipango ya kuwapsha madogo wamiliki vyumba tujipange mapema haina kurudi nyuma hiyo[emoji41]
Huu ndio mwaka wenyew sasa [emoji3]

Sent from my SM-G920P using Tapatalk
 
ebuana tangu nimezaliwa mimi nilikuwa naishi na mama angu pa1 na wadogo zangu, katikati ya mwaka 2015 nikiwa form four mama aliamua kwenda dar es laam kujichanga kimaisha, akaniacha mimi na wadogo zangu kama watatu, baada ya mwezi akaagizia mtu amuijie yule mdogo kuliko wote(wakati wote huo alikuwa anagharamia pesa za matumizi na kodi ya pango, na Mimi nikiwa bado nipo maskul).

Sasa baada ya kumaliza shule kimbembe ndipo kilipo anza, kwanza kodi ikaanza kusumbua kwa mother, pia hela ya mahemezi nayo ikawa taaabu kweli kweli. mara mama atume buku10 kwa juma zima ikafkia hatua madogo wote wakatoweka home. Mwingine alienda kwa rafki yake mama na mwingine akawa kaenda kwa ndugu zetu nikawa nimebaki peke angu

Nikatafakari maybe niangalie upande wa pili yaani kwa mshua(yupo dar miaka mingi ila yeye ana maisha yake na mama ana harakati zake) ambaye kiuharisia sijakuwa naye wala sijawahi kukaa nae hata siku nzima ikapita, nikamwambia anisaidie walau pesa ya mtaji hata laki1 iweze nisaidia kupata chanzo (wakati huo mama ana kama miezi miwili hatumi pesa ya kodi wala ya magenta). Mara baada ya baba kumuomba pesa alichonijibu sikuwahi kutarajia kujibiwa, aliniambia kuwa "MTAJI WAKO WA KWANZA NI JAMII INAYOKUZUNGUKA" sikuwa na jinsi ilinibidi nikubaliane na matokeo..

Baada ya mda flan iv mama alituma elfu40 pekee akadai nihamie sehem nyingine maana mwenye nyumba alikuwa keshakuwa mbogo.. pia niangalie nyumba yenye bei poa kwa kuwa nimebaki peke angu afadhari nichukue walau single isiyo na umeme ili inisadie kupunguza gharama ya kodi nikalipia hela ya miezi miwili(ila kipindi nahama baba mwenye nyumba ninapo hama alikaba baadhi ya vitu ila nilikuja kuvikomboa baadae, baada ya kupata pesa yake).

Namshukuru mungu baada ya muda kweli ushauri ule wa baba ambao niliuona wa kipuuzi niliutumia kuifanya jamii yangu kuwa mtaji, niliajiliwa kuuza DVD mtaani(yaani kama nikiuza elf2 ya boss ni buku na yangu buku, hata nkiuza zaidi ya elfu mbili ya boss ni buku tu kwa kila DVD) kama mwez kama wa 10, 2016 wadogo zangu walimfuata mama. nikawa nimebaki peke angu..

Kiukweli biashara ilinilipa sana maana kwa siku niliweza kutunza faida ya hadi elf 3o nikawa nanunua mifugo mbuzi&ng'ombe napeleka kwa babu kijijini, nikaanza kujipanga maana vitu vyote vya ndani nilimtumia mama, na mm nikaanza maisha yangu hadi sasa najitegemea na mama anaomba msaada wowote kutoka kwangu..

2017 nilibadili biashara na kuwa mqchinga nilipambana sana na mwanzoninmwa mwaka jana nikaamua kuwa wakala wa mitandao ya kipesa hadi hivi leo nimejiajiri mwenyewe kama wakala.. kiukweli mimi kama mimi hakuna hata sumuni ya mtu nilioipata kutoka kwa mtu yeyote zaidi ya juhudi zangu na nia yangu ya kuishi kwa imani kuwa naweza.

Wito:mwanzoni nilijua kauli ya baba ilikuwa ni ya kunivunja moyo, lkn hadi hivi leo naishi nikiamini siku moja nimuaminishe baba kuwa niliishi kwa kutegemea jamii inayonizunguka ndio maana nimefka hapa nilipo, kila kijana ana kila sababu ya kutokukaa nyumbani kwa kigezo cha kutokuwa na pa kuanzia..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom