Ulianzaje kukaa gheto?

Safi sana[emoji109]
 
Karibu sana mkuu. Mwanzilishi wa huu uzi tumpe big up maana unasaidia vijana wengi kupata upenyo wa kuanza maisha.

Siku nikipata muda mzuri nitaweka kisa changu jinsi nilivyoanza life na wenzangu mpaka nilipofikia.
Nakufuatilia kwa karibu mkuu,shuka nondo tupate madini zaidi.
 
Hongera sana Mkuu,naamini kila kitu kitazidi kuwa sawa kabisa.
 
Neno hili mkuu[emoji109][emoji109]
 
Roger👮‍♂️
 
Safi sana mkuu .Ukianza kuhangaika na wanawake mda si mrefu unarusha taulo unarudi nyumbani
 
Daah mi waizi wamenirudisha nyuma wameniibia kila kitu ndani hapa nilipo ndio naanza moja tuombeane wakuu [emoji120]

Nikikumbuka nilijinyima kazi zenyewe ni hizi za kungaunga ghetto wachuchu walikuwa wanalielewa sana ukimleta mtoto anakuganda kila saa text uko wapi nije leo hii imebaki story.

Mda mwengine nafikiria nitafute mganga wacha nitoboke nimuue mwizi wangu.
 
Nashauri usinunue boda boda mtumba kama huna uzoefu nazo. Ishawahi kuniingizia hasara kubwa sana
 
Duh pole,,, ila hyo mitaa ya mazese kuna wezi sana kwa nn usihamie sehem zenye usalama kiasi asee?
 
Safi sana mkuu .Ukianza kuhangaika na wanawake mda si mrefu unarusha taulo unarudi nyumbani
Kabisa,wanawake wanarudisha maisha ya vijana nyuma sana, kama unaye weka malengo naye,na yeye awe na malengo mazuri kwako.

Mwanamke mwenye malengo mazuri huwa siyo pasua kichwa, huumizi kichwa kuwa naye karibu, asipokuwa karibu na wewe ndipo unahisi umepungukiwa kitu.

Mambo yako yakienda hovyo unamtafuta hata usikie ushauri wake akutie moyo upate nguvu mpya ya kuendelea mbele.

Sisi wanaume tulishapewa akili na Mungu,kuna mambo tunayafanya hayahitaji nguvu wala akili tulizopewa isipokuwa ni kutiwa moyo na jinsia ya kike.

Ukiwa na mtu wa namna hii, huwezi kukwama moja kwa moja sana sana utapitia kipindi fulani tu cha mpito.

Kama una mama mzazi /mlezi wako ni vizuri kumjulia hali mara kwa mara na kumuomba awe anakutamkia baraka na mafanikio kila akukumbukapo.

Ukipata zawadi hata kama ni kidogo usiache kumtumia maana unakuta vijana wanaishi mbali na wazazi wao kwa muda mrefu.

Furaha ya mama na baba ni mafanikio yako tosha.Tusiwatelekeze wazazi kwasababu zisizo za msingi.
 
Kwanza nikupe pole.

Unasema wachuchu walikuwa wanalielewa ghetto lako maana yake ulikuwa unawabadilisha jinsi utakavyo.

Ulilifanya ghetto lako kama ulimbo wa wachuchu, nina wasiwasi labda walikuchoresha kwa wana uibiwe kama kulipa kisasi kwasababu uliwatumia na kuwatosa.

Au hao waliokuibia ni miongoni mwa wapenz wa wachuchu uliokuwa ukiwaleta kwako.

Ushauri wangu,sasa hivi angalia maisha yako na usiwe mwepesi kutafuta mtu au kuleta mtu kwako na kujua unaishije.

Ikibidi hama huo mtaa wasije wakakurudia tena maana wameshakujua nyendo zako. Pole sana hili nilishawahi kulisema huko juu kwamba kuibiwa kunarudisha maendeleo nyuma.
 
Fifa level nyngn sema apa kwang asilimia 90 wanachza pes
 
God of war ngp kaka 4 au 5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…