Merchante
JF-Expert Member
- May 9, 2017
- 1,365
- 2,842
Safi sana[emoji109]Kipindi Niko chuo siku za weekend nachomoka mara home kwa mzee, mara kwa bi.mkubwa, mara Kwa washkaji… sasa nikienda weekends kwa wana nakuwa inspired kinoma! Mpaka sometimes likizo Naweza kutumia hadi week mbili kwa washkaji staki tena kwenda maskani, baada ya wanangu kumaliza mmoja akaenda Ulaya mmoja akapata kitengo Mkoa fulani kwa sababu kwao walikuwa na watu upande wa ujombani. Kipindi wana wana-separate mimi Niko home kwa Bi.mkubwa life ikaanza kuwa michosho hamna michongo wala nini na kama unavojua nyumbani dharau na kejeli+ nyodo Hasa kutoka kwa madogo huwa haziishi. Sasa pale home bi.mkubwa alikuwa kaolewa tu inamana sio kwetu kwa “100%” mzee mzima nikawa Uncomfortable siku moja nilivurugwa vibaya mno mapema alfajiri nikasepa kuelekea Magomeni kwa jamaa zangu wengine ambapo ni nyumbani kwao na mwanangu mwingine wa Karibu sana ambaye yuko Mamtoni kitambo tangu tuko O-level ila bahati nzuri ukaribu na urafiki wetu wa kushibana ulikaribisha undugu mpaka nikaweza kukaa kwao bila pingamizi. Kama zali baada ya kukaa pale siku kadhaa rizk ikawa inapatikana na mfukoni sikaukiwi ingawa ugenini ni ugenini tu Sio wote walipenda uwepo wangu pale. Msimamizi wa ile nyumba ambaye alkuwa ni shangazi yake na mwanangu alinipenda sana na kuniamini kutokana na nidhamu na uaminifu kiasi kwamba mpaka kunishirikisha maswala kadhaa ya familia… kimbembe kikaja kuna shangazi yake mwingine wa huyo mwanangu ambaye nilienda kuishi kwao kutokana na ups and down za familia alikuwa anaishi mtoni na yeye sasa akaja bongo kula goodtime na kufatilia michongo yao mingine huku bongo ya ujenzi na biashara zao akanikuta naishi pale na kabla alipata taarifa. Dahh! Yule shangazi hakupenda kabisa uwepo wangu pale na akaagiza niondoke. Kwa sababu mwenye pesa ana kauli yule shangazi wa kwanza msimamizi wa mjengo hakuwa na namna akaniita na kuniweka wazi. Nikiwa kwenye tathmini nikapokea simu kutoka majuu hakuwa mwingine bali ni Mama mzazi wa rafiki yangu na akanitaka nibaki hapo kwa sababu mwana tayari nilimchana kila linaloendelea maishani kwangu kipindi hicho. Siku zilizidi kusogea ingawa maisha yalikuwa mazuri ya amani pale na utulivu lakini maneno ya chini chini yalikuwepo. Shangazi msimamizi wa nyumba anazidi kuwa pressurized kutoka kwa Dada’ake kwamba kijana aondoke hapo sasa ukawa mvutano kati ya mawifi dhidi yangu. Nikaona isiwe kesi nikiwa katika maandalizi ya kusepa mwanangu akanivutia waya akaniambia siku si nyingi nakuja bongo usiondoke kwanza. Mwana akaja na life ikawa inaendelea Kumbe mwanangu alikuja na Neema. Alijua wazi mwanae sina kitu na Niko kwenye situation ngumu ingawa rizq ya pesa za vocha na kubadili mashati inapatikana. Akanipatiaga kitita kirefu cha pesa nakumbuka ilkuwa baada ya mwezi mtukufu na baada ya sikukuu ya eid mnamo mwaka fulani. Nikafanye mafekechee ya kutafuta chimbo maeneo fulani maeneo ya Mikocheni “A” uswahilini ambapo Nlkuwa na mwanangu mwingine anaishi kule lakini alikuwa anafanya kazi dukani. Ikabidi aniunganishe na wana wengine ambao ni ndugu zake tukawa tunakaa ghetto moja. Nikarudi Magomeni na kuaga baada ya kuweka mambo sawa na nikaanza maisha rasmi kama mpangaji. Life ikasonga na siku zikasogea wale wana niliokuwa naishi nao wakapata kazi sehemu tofauti hivyo wakalazimika kuhama… mmoja akaenda Visiwani mmoja hapahapa Dar maeneo ya kawe karibia na Mbezi kamanda nikabaki peke yangu tena ingawa sikupapenda maeneo yale kutokana na mazingira machafu na palikuwa uswahilini nikasubiri kodi iishe… baada ya muda nikapata mchongo ukaniongezea pesa kidogo ikabidi nihame sasa nikahamia Mikocheni “B” ambapo ghetto hata unaweza kumleta demu akagoma kuondoka [emoji1][emoji39][emoji1786] na baada ya wiki chache nikapata kibarua ofisi fulani maeneo ya Mbezi beach. Safari ya maisha ikaanzia hapo ingawa si haba Hohehahe anasongesha siku