Ulianzaje kukaa gheto?

bora kupika, ila sio kuosha vyombo

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
Kuosha vyombo ni mtihani mkubwa kwetu sote[emoji2][emoji2]

Huwa naosha hadi nikipika tena[emoji2][emoji2][emoji1787][emoji1787] ila havipiti siku moja vikiwa vichafu

Au naweza viosha halafu vikakaa wiki nzima bila kutumika nagongea takeaways au mama nijazie sometimes.
 
Nakubali mkuu
 
Sikuwahi kutilia maanani sana huu uzi. Lakini kwa mara ya kwanza nimekutana na kitu. Link nilitumiwa na member wa jf mwaka juzi, lakini Leo baada ya kukosa cha kufanya nikaona niingie hapa. Mbarikiwe, naamini hadi kufika mwisho nitakuwa nimetoka na kitu.
 
Nipo mkoa mmoja wenye baridi nyanda za juu kusini, nipo geto hapa godoro tu nimeliweka chini pamoja na jiko la gesi la kupikia, maisha yanasonga mdogomdogo.
Komaa utatoboa. Ila chini ya godoro hakikisha unaweka mkeka chini ili lisije likapitisha unyevu ukakuathiri kiafya siyo mzuri. Mambo yakikaa sawa nunua kitanda kabisa usilale chini muda mrefu.
 
Hapa ni kisima cha maarifa mkuu. Ukisoma comments zote kuanzia juu unajikuta umeshapata ujasiri wa kupambana bila kukata tamaa. Karibu sana.
 
Natoroka kulipa bili nakimbilia kwa mshkaji wangu nakutana na mshkaji wangu naye anatoroka kulipa bili anakuja kwangu.

Tukaenda zetu kukaa baharini kuanzia asubuhi mpaka saa nne usiku tukaenda kulala kwa mshkaji wetu mwingine na ndiyo tumeamka hapa.
 
Natoroka kulipa bili nakimbilia kwa mshkaji wangu nakutana na mshkaji wangu naye anatoroka kulipa bili anakuja kwangu.

Tukaenda zetu kukaa baharini kuanzia asubuhi mpaka saa nne usiku tukaenda kulala kwa mshkaji wetu mwingine na ndiyo tumeamka hapa.

[emoji23][emoji23]afu si ulisema una watoto 3 hukai nao ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…