Ulianzaje kukaa gheto?

Wale wadau wa mwezi wa nane,,,mshaanza life la gheto,

Kuna mmoja kapata kitanda na godoro kahama kwao[emoji16],sasa maisha yanamkoroga hana kazi wala biashara[emoji16]


Bado sijashawishika kuhama home[emoji6]
Sasa maisha yanapokukoroga ndipo muda muafaka wa kufahamu uwezo wako wa kujisimamia. Utafahamu vipaumbele vyako na mambo ya kupuuza. Mfano hautahonga hovyo ili uweze kununua mahitaji ya ndani.

Umeshawahi kugundua ukiwa unaishi kwenu, kwa shemeji yako au popote ambapo huwa haulipi kodi wala kuchangia gharama, unakuwa na akili ya kuleta videmu ndani ila ukishaanza kuishi mwenyewe na kujitegemea utaona unaanza kuona ni upuuzi kuleta videmu maana linakuwa ni jambo la kawaida na unaloweza fanya muda wowote ukitaka.

Huko sasa ndiko kukua kiakili na kupevuka. So unapoishi kuna mambo yatakuzonga mfano, kodi kila baada ya kuisha, bili ya umeme, maji, takataka, ulinzi.

Lakini pia utajikuta unawajibika na mambo ya kijamii ambayo yatakushape kuwa mtu mzima. Na hii itakufanya utafute mwanamke ambaye mtashirikiana kujenga maisha na si kupoteza muda.
 
Safi sana. Sasa ujitahidi kupambana na hayo maisha hadi yakupe siti uyaendeshe mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…