Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Taratibu ktk harakati za kuanza maisha ya ghetto.
IMG_20220812_170635_565.jpg
IMG_20220812_170659_492.jpg
IMG_20220812_170438_592.jpg
 
Wale wadau wa mwezi wa nane,,,mshaanza life la gheto,

Kuna mmoja kapata kitanda na godoro kahama kwao[emoji16],sasa maisha yanamkoroga hana kazi wala biashara[emoji16]


Bado sijashawishika kuhama home[emoji6]
Sasa maisha yanapokukoroga ndipo muda muafaka wa kufahamu uwezo wako wa kujisimamia. Utafahamu vipaumbele vyako na mambo ya kupuuza. Mfano hautahonga hovyo ili uweze kununua mahitaji ya ndani.

Umeshawahi kugundua ukiwa unaishi kwenu, kwa shemeji yako au popote ambapo huwa haulipi kodi wala kuchangia gharama, unakuwa na akili ya kuleta videmu ndani ila ukishaanza kuishi mwenyewe na kujitegemea utaona unaanza kuona ni upuuzi kuleta videmu maana linakuwa ni jambo la kawaida na unaloweza fanya muda wowote ukitaka.

Huko sasa ndiko kukua kiakili na kupevuka. So unapoishi kuna mambo yatakuzonga mfano, kodi kila baada ya kuisha, bili ya umeme, maji, takataka, ulinzi.

Lakini pia utajikuta unawajibika na mambo ya kijamii ambayo yatakushape kuwa mtu mzima. Na hii itakufanya utafute mwanamke ambaye mtashirikiana kujenga maisha na si kupoteza muda.
 
Uzi ulionitoa kwnye kiza Hadi Sasa nauona mwanga japo haikuwa rahisi kuwashawishi wazazi kuondoka nyumbani na kupanga chumba ilihali umeacha chumba ama vyumba nyumbani , ikibidi nikimbie kinyemera baada ya mambo kuwa magumu na dharau kuwa nyingi kwa wadogo zangu pindi wakirudi likizo kutwa unagombana nao na ukijitzama n mtu mzima hapo ndipo nilipoamua kusepa nakumbuka mfkon nilikuwa na tsh 40,000 nikampga saundi Dem wangu ambaye Sasa n wife aknipa 80,000 nikakodi chumba elf tisini na mkeka wa 7000 pazia nilichomoa nyumban na life likaanzia hapo.
Safi sana. Sasa ujitahidi kupambana na hayo maisha hadi yakupe siti uyaendeshe mwenyewe.
 
Back
Top Bottom