Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Hii ni kwetu wanangu wa Maghetton!

Tusisahau kusave kila tunapopata mkwanja,hata kama umepata buku ten fanya saving walau ya buku sio mbaya. Jambo lingine na muhimu zaidi,ni kuwekeza katika kitu ambacho una ujuzi au ufahamu nacho kiundani,itapendeza zaidi kitu hicho kiwe kinagusa kwa namna moja au nyingine katika shughuli zako za kila siku.
Hapa namaanisha,mfano mimi msimamizi wa masuala ya mbao,basi mara moja moja nanunua miti kadhaa,au sometimes nanunua mbao kadhaa na kuziuza.
Kwa mfano ukiwa fundi katika workshop ya mtu,unaweza kununua hata MDF-Boards zako,au bawaba,handles,nob,n.k na kuwauzia baadhi ya mafundi wenzio.

Hivyo hivyo hata ukiwa dukani,kama bosi sio mkuda weka hata mzigo wako pale unapoona boss hajaleta mzigo kwasababu either kakwama au lah.
Muhimu ni pesa izunguke.

La mwisho na kubwa zaidi,usisahau kuwapa watu wenye uhitaji,toa msaada kwa watu wanaohitaji,mfano masikini,wazee,watoto yatima,n.k. Wakuu hii issue ya kutoa ni zaidi ya ndumba,milango mingi sana ya kimafanikio hufunguka. Mtu anaposhukuru kuna kitu kikubwa sana unapata. Mtumie hata Mshua, Mother au madogo chochote kile bila kujali uko katika hali gani.


NB: Pahala ambapo unaamka kila siku kwenda kusaka mkate wa kila siku ni pahala muhimu na nyeti sana.
So, Ghetto liheshimiwe,na si kila mtu anapaswa kulazwa ghetto kwako.

Tuendelee kupambana wanangu wa damu,JAH bless us![emoji109]
Ubarikiwe[emoji1545]

Kuna vijana kila mwanamke wakiokota huko wanapeleka gheto hii haipo sawa,
 
Ubarikiwe[emoji1545]

Kuna vijana kila mwanamke wakiokota huko wanapeleka gheto hii haipo sawa,
Uko sahihi Mkuu, kwanza hata issue ya kuwa na mahusiano mengi nayo haijakaa poa si tu kwa kijana mtafutaji ila hata kwa mtu yeyote yule. Ukiachilia mbali kwamba unaathiri uchumi wa huyu mtafutaji,pia kuna athari nyingi sana nyinginezo ni za kiroho pia.
 
Ado ado washkaji nimevunja kibubu hapa nimechoka sina hata mia mazee,nimejilipua lakini fresh hela inatafutwaView attachment 2427087

Hongera
Akili uliyotumia kufanya servings kununua tv na subwoofer
Ile ile itumie kufanya vingine vikubwa
Nunua vitu vyote vya kukaa ndani
I mean make sure ukirud geto ni sehemu itakufanya u refresh akili yako itulie
Ukimaliza anza kuweka fedha nunua kiwanja
Mwaga mawe
Mchanga anza kuinua kidogo kidogo

Vitu vyote tunayonafasi yakuanavyo as long as tumeweka malengo
Kikawaida malengo ndio humuendesha mtu
Hopefully next days tukaona nyumba yako na vingine vijubwa
Keeps it up man[emoji1316][emoji1374]
 
Hongera
Akili uliyotumia kufanya servings kununua tv na subwoofer
Ile ile itumie kufanya vingine vikubwa
Nunua vitu vyote vya kukaa ndani
I mean make sure ukirud geto ni sehemu itakufanya u refresh akili yako itulie
Ukimaliza anza kuweka fedha nunua kiwanja
Mwaga mawe
Mchanga anza kuinua kidogo kidogo

Vitu vyote tunayonafasi yakuanavyo as long as tumeweka malengo
Kikawaida malengo ndio humuendesha mtu
Hopefully next days tukaona nyumba yako na vingine vijubwa
Keeps it up man[emoji1316][emoji1374]
100% 💪💪💪
 
Mimi nilipomaliza tu chuo nikapata sehemu ya kujitolea wakawa wananipa hela kidogo nilikuwa nakaa home ila sikuweza kununua kitu nawakati nakula bure hela naenda tu saluni
Siku nilipochoka kujitolea nikaondoka na home nikawa nakaa na rafiki angu tunashare kodi na nilikuwa sina kaz lakini niliweza kununua vitu vingi tu
Mmmh nawasiwasi na upataji wako wa pesa ya hivyo vitu vingii....
 
Yeah umenena vyema kabisa, hii ya kuweka vitu na kuwauzia umenipa darasa kubwa sana. Maana nafanya kazi ya drilling na blasting explosive hua tunanua ghalani, sijawahinkuwaza kununua vingi kuvisave kwa ajili ya kuuza nikipata kazi.
Nunua hivo vibati,cotex,futa na mazaga mengine kikubwa tafuta eneo zuri uweze kufihifadhi,unakua unawauzia wachimbaji mdogo mdogo,vinalipa sana mkuu
 
Mimi miaka kadhaa iliyopita tulipishana na mzee wangu akanifukuza nikamwambia kama ni kuondoka nitaondoka na vitu vilivyopo chumbani kwangu, akasema wee thubutu wakati nanunua ulijua nilipataje hela, na mm nikakomaa kwamba nimelala kwenye chumba hicho miaka zaidi ya ishirini, nimevitunza I've earned them, hata mke akiachana na mwanaume wanagawana pasu hata kama alikuja na nguo tu mana alivitunza, mzee akadinda, nikatega siku wameenda kanisani nikachukua godoro la 5×6, kabati la nguo subwoofer ndogo pamoja na tv ya chumbani kwake, nilikua na kama laki tano ndo nimetoka kupiga dili nikaipata, nikaondoka nikaenda kupangisha nikiwa sina mishe yoyote nikalipa kodi ya miezi 3 nikanunua sufuria jiko la gesi na vyombovyombo nikaishi, nikawa sipokei simu mpaka mzee akaacha kupiga, mama hakuwahi kuacha kupiga nikawa napokea baada ya muda.
Nikapata kazi kwa wahindi flani maisha yakasonga kodi nalipa na maisha yanaendelea, kwa vile nazungumza na mama akawa ananipa feedback kwamba hapa home tunakumiss mana nilikua ndo nashughulika na usafi wa nje kuweka garden fensi maua maua yakae mkao, kazi zile zinazomhitaji mwanaume, sasa hakuna mtu na mze kazeeka, kwaiyo ananikumbuka sana hata alishanisamehe, nikapata mchumba ndio kwa mara ya kwanza tangu kuondoka nyumbani nikarudi kumtambulisha, nikachinja mbuzi ilikua shangwe sana.
Tangu hapo nikaoa nina watoto na kila jumapili lazima twende kwa wazee kushinda huko, watoto wangu wakifunga shule wanaenda huko wanaishi kabisa, mdogo ndio kahamia huko yani humtenganishi na babu yake. Mzee akanipa kiwanja kati ya vingi alivyokuwa navyo nikajenga nyumba simple tu room 3.

Ila nisingefukuzwa siku ile nisingekuwa hapa mana nilikua naogopa sana maisha ya kupangisha, hasa ukiimagine kila kitu unapata
Wakati mwingine jambo zuri linawezakutokea kwenye jambo baya

Sent using Jamii Forums mobile app
Oya uliipiga kibabe hivo ndio safi

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Yeah ila dah hao wenye nyumba jau maana asilimia 80% ya watu majumbani wameweka Tv ukutani
Me napokaa kipindi nahamia nimepewa notice/mkataba kusoma kuna kipengele HURUHUSIWI KUTOBOA UKUTA ila nachoshukuru mwenye nyumba madirisha yote katoboa kabisa kaweka bomba za kuwekea pazia na ukutani kwenye tv katoboa kabisa kama mtu utataka kuning'iniza Tv uweke so kazi ni kwako mpangaji.
 
Me napokaa kipindi nahamia nimepewa notice/mkataba kusoma kuna kipengele HURUHUSIWI KUTOBOA UKUTA ila nachoshukuru mwenye nyumba madirisha yote katoboa kabisa kaweka bomba za kuwekea pazia na ukutani kwenye tv katoboa kabisa kama mtu utataka kuning'iniza Tv uweke so kazi ni kwako mpangaji.
Huyo mwenye nyumba ni smart

Ila wengine unaambiwa usitoboe halafu hamna mafekeche aliyofanya inakua noma mpaka umtafute fundi akufanyie wepesi
 
Nimeshakamata showcase la kibabe na kitchencabinet milango 3 bado gheto tu hapo nisepe home
PXL_20221125_112303053.jpg
 
Back
Top Bottom