mawardat
JF-Expert Member
- Apr 27, 2021
- 23,965
- 131,949
Ubarikiwe[emoji1545]Hii ni kwetu wanangu wa Maghetton!
Tusisahau kusave kila tunapopata mkwanja,hata kama umepata buku ten fanya saving walau ya buku sio mbaya. Jambo lingine na muhimu zaidi,ni kuwekeza katika kitu ambacho una ujuzi au ufahamu nacho kiundani,itapendeza zaidi kitu hicho kiwe kinagusa kwa namna moja au nyingine katika shughuli zako za kila siku.
Hapa namaanisha,mfano mimi msimamizi wa masuala ya mbao,basi mara moja moja nanunua miti kadhaa,au sometimes nanunua mbao kadhaa na kuziuza.
Kwa mfano ukiwa fundi katika workshop ya mtu,unaweza kununua hata MDF-Boards zako,au bawaba,handles,nob,n.k na kuwauzia baadhi ya mafundi wenzio.
Hivyo hivyo hata ukiwa dukani,kama bosi sio mkuda weka hata mzigo wako pale unapoona boss hajaleta mzigo kwasababu either kakwama au lah.
Muhimu ni pesa izunguke.
La mwisho na kubwa zaidi,usisahau kuwapa watu wenye uhitaji,toa msaada kwa watu wanaohitaji,mfano masikini,wazee,watoto yatima,n.k. Wakuu hii issue ya kutoa ni zaidi ya ndumba,milango mingi sana ya kimafanikio hufunguka. Mtu anaposhukuru kuna kitu kikubwa sana unapata. Mtumie hata Mshua, Mother au madogo chochote kile bila kujali uko katika hali gani.
NB: Pahala ambapo unaamka kila siku kwenda kusaka mkate wa kila siku ni pahala muhimu na nyeti sana.
So, Ghetto liheshimiwe,na si kila mtu anapaswa kulazwa ghetto kwako.
Tuendelee kupambana wanangu wa damu,JAH bless us![emoji109]
Kuna vijana kila mwanamke wakiokota huko wanapeleka gheto hii haipo sawa,