Anigrain
JF-Expert Member
- Nov 15, 2020
- 1,680
- 4,204
Kama unataka kitanda imara na kizuri usiwe na haraka, kwa Dar wapigaji ni wengi sana mwanangu, unanunua kitanda baada ya miezi 4 tu unaanza kuskia wadudu wanapokezana Kula MbaoMkoani sina mkuu, kama kuna vitanda vya kijanja mnavijua niambieni nichukue kimoja.
Jaribu kuongea na mshkaji huyo wa Iringa ili uone kama anaweza kukutolea kitu unachokitaka na kama mtafikia makubaliano basi uagize kwake
Na kama itashindikana basi itabidi umcheki jamaa mwingine ye yupo Iringa pia na wala hanaga shida, unamcheki mnayajenga kisha anakupa terms zake and conditions basi unakaa kusubiri Mali yako ambayo ni kweli Mninga
ila kama hizo condition zitakuwa ngumu basi tafuta washkaji wenye mazoea na mafundi wa Dar wakupeleke eneo la tukio ili usipigwe, Dar kuna mbao za ajabu sana ndugu yangu, ukikuta imepigwa Rangi unasema furniture sindo hii sasa...! Sasa subiri balaa lianze