Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

M napenda kuwa na fridge ndogo kama iyo yako siku moja ,Bei yake inaenda kias gan na uimara wake na kampuni ipi nzuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekupata mkuu, ila kama tukisema tuieweke kimakundi hiyo Fridge basi haitokaa kwenye kundi la Fridge ndogo labda picha tu ndo imefanya uhisi ni ndogo, ila hiyo tuiite size ya Kati ambayo inafaa ata kwa wenye Familia maana ina ujazo wa 141 Litres

Sasa tukija upande wa bei ndomana me nimemwambia ndugu yangu Depal kuwa ni Hisense mkombozi wa Wanyonge kutokana vitu vyao kuwa na ubora kiasi chake ila pia bei zake ni rafiki, hiyo me nilichukua 680k tu Mkuu
 
Hiyo friji sio ndogo
Ni medium
Akitaka ndogo yake ziko za mlango mmoja kwa 450.

Nilipo ni 650
Bei ya kujuana mwisho 630 ‘ mpaka mjuane ile ya uhakika.
 
Wadau nina 800k nataka ninunue kitanda na godoro zuri vya kudumu ila juzi kati nilienda kwa fundi wa vitanda akaniambia kitanda kizuri cha mbao za mninga minimum niwe na 800k akanionesha na picha baadhi ni vizuri kiukweli nikamwambia nitarudi ngoja nijipange, ninachotaka kujua ni kweli vitanda vya mninga vina bei kiasi hicho? au kama kuna mtu anajua sehemu naweza pata kitanda kizuri cha kudumu aniambie wakuu at least 600k naweza kununua.
 
Kwa Mninga mkuu ni kweli kabisa, tofauti na hapo labda uwe na fundi mzuri Mkoani kisha akutengenezee design unayotaka wewe akuagizie ndio utapunguza gharama na kufikia 550-600k
 
Ulikosea sana kurudi nyumbani.

Mimi bado nipo chuoni Mwaka wa mwisho ila ninaishi getto, nitanunua kila kitu kadri ya uwezo, ili nikimaliza chuo nisirudi home.
Really aiseee. Maana sometime unaeza pata nafas ya kumuonesha muelekeo mzaz au mlez kwakua umeonesha nia ya kuyaanza
 
Sio muda mwafaka mkuu, Kwanza jua unataka nini na kwa wakati gani, me pia nilianza kazi na mshahara kama wako

Na kipindi hicho nilikuwa natoka mbali sana ili kwenda kazini, kama ni mwenyeji wa Dar, Me nilikuwa naishi sehemu moja panaitwa Kisewe, kupita mbagala na unaingia Chamanzi, unatokea Mbande

ilikuwa inanilazimu kuamka sa 10:30 usiku kujiandaa na hadi sa 11:15 napanda daladala kwenda kariakoo, nilikuwa nafika mjini sa 12:30-12:45 na kuondoka sa 12:45 jioni na home kufika sa 4 usiku

Pamoja na kupata kazi ila sikuona kama ni muda sahihi wa kuondoka home, ilibidi nianze kwenda kuwekeza hela kwa muuza godoro, nilianza kuwekeza 70k ili ninunue godoro Dodoma QFL inch 10 ambalo Kwa kipindi hicho lilikuwa likiuzwa 220k

Kutokana na nauli kuwa ndani ya hiyo hiyo pesa ndomana nikaw naweka 70k na kiasi kingine nilikuwa nahemea vyakula pale home, baada ya miezi 3 nikawa nimemaliza kulipia godoro na mshahara wa mwezi wa 4 ndo nikaenda kutafuta chumba Kigogo

Nilianza na chumba cha 30k nikalipia miez 3 na kununua baadhi ya mahitaji, ndipo nikahama home na kwenda kujitegemea rasmi, kwahiyo kama home hakuna ugai gai we kaza tu ata miez 3 ili ujiandae kisha usepe

Baada ya hapo ndo nikaanza kuweka tena hela ya kununua kitanda na baadhi ya vitu mdogo mdogo huku nikiendelea kulalia maandazi na marage ya kuomba hati punguzo ili nipate Kwa nusu bei

At least saizi Mambo sio mabaya sana maana naishi kwenye kanyumba kenye unafuu wa muonekano na ata ndani sio haba sana, mtu akija home hawezi kujua kama nilikuwa sina ata 200 ya kulipia huduma ya Choo pale kariakoo

Ukisema uondoke na hiyo 150k utaambulia chumba tu na kagodoro Ka hovyo alafu itakulazimu kuja kununua tena godoro lingine zuri kwahiyo utakuwa umeongeza gharama ambazo sio za ulazima na usiombe hicho kibarua kikaota nyasi mwezi wa 2 tu alafu uwe umesepa home mapema

Kama hapo ulipo sasa kero zilizopo au shida zilizopo zinavumilika basi we jipe Malengo na uishi malengo yako ili baada ya Muda uliojiwekea uwe umetimiza na kuendelea na mambo mengine ambayo View attachment 2469212
Ushauri mzuri sana umempa,ila kama kero anazokutana nazo zinazidi hata kero za kulala chini na kula mkate na maharage. Basi namshauri ahamie kwake mapema sana.
Mkuu hiko chupa ni inches ngapi?
 
Wadau nina 800k nataka ninunue kitanda na godoro zuri vya kudumu ila juzi kati nilienda kwa fundi wa vitanda akaniambia kitanda kizuri cha mbao za mninga minimum niwe na 800k akanionesha na picha baadhi ni vizuri kiukweli nikamwambia nitarudi ngoja nijipange, ninachotaka kujua ni kweli vitanda vya mninga vina bei kiasi hicho? au kama kuna mtu anajua sehemu naweza pata kitanda kizuri cha kudumu aniambie wakuu at least 600k naweza kununua.
Uko mkoa gani Mkuu? Huku niliko mninga ni 950k-800k (6*6), 5*6 ni 750k-600k.
 
Mti wa mninga unapatkana mkoa gan?? Na ntajuaje kwamba hk ktanda kweli kimetengenezwa kwa mninga?
Mninga unakua na mwonekano huo,utaujua kwa mabaka mabaka yake,uzito,n.k.
JPEG_20230105_163136_8528725050475407450.jpg
 
Hiyo formula nzuri mkuu, kama home hakuna shida bora ujiwekeze tu kila kitu na siku ukihama unakuwa full package

Me niliwahi kutoka home kutokana na changamoto ya usafiri na umbali, nilikuwa natumia muda mwingi sana kwenye daladala

Ata job nilikuwa nasinzia tu, nikaona hapa hii kazi itakuja kuwa mateso kwangu badala ya faraja, ikabidi nisepe
Kabisa nataka nitoke full package mkuu hm na job ni karibu.
 
Mti wa mninga unapatkana mkoa gan?? Na ntajuaje kwamba hk ktanda kweli kimetengenezwa kwa mninga?
Ni ngumu kujua mkuu kama huna uzoefu na mbao, ila mara nyingi waga ni busara za fundi tu kama unajuana nae hawezi kukupiga

ila kwa baadhi ya sifa za Mninga ni mbao nzito sana tofauti na mbao zingine lakini pia unakuwa hauna Rangi moja, unakuwa na mabaka mabaka

Pia ukipigwa tu msasa na kupigwa vanish unawaka hatari unaweza kusema umepigwa mapambo ya Kipemba kumbe vanish tu

Kwa upande wangu Mara nyingi Mninga nilifanikiwa kuona Tabora na Iringa ila Dar sinaga kabisa imani nao
 
Ushauri mzuri sana umempa,ila kama kero anazokutana nazo zinazidi hata kero za kulala chini na kula mkate na maharage. Basi namshauri ahamie kwake mapema sana.
Mkuu hiko chupa ni inches ngapi?

Ni kweli mkuu uko sahihi...! Aisee hiyo chupa ni 55" tu kishkaji
 
Back
Top Bottom