Ulianzaje kukaa gheto?

Daaah!!nimekumbuka mbali Sana,Yani nimeanza gheto na godoro limechoka Yani unalala mbavu zinauma hadi unaamua kuamka usingizini upumzike kidogo halafu unarudi Tena kulala!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Upo form 2?una miaka mingap?
 
Utakua mwanafunzi wa bamaga wewe mkuu
 
You are hero
 
Ilikuwa 2012 mwezi wa sita tunafanya UE ya mwisho tarehe 23 kisha tufunge chuo. Home mkoani Dar kuna shangazi. Nikawaza kweli mimi ndio niende kwa shangazi, nikajisemea HAPANA siwezi!

Nikaingia Hostel za mabibo pale nikaiba godoro ambalo tulikuwa tunalalia chini (enzi hizi za sasa sio rahisi kwa madogo wa chuo kuelewa ilikuwaje) nikatafuta chumba chenye watu waliolipia kukaa pale kipindi cha field na nikalala pale miezi mitatu yote ya field (kumbuka hostel zote za chuo zinafanya kazi kipindi cha field kwa wale wanaohitaji.

Mungu aliniwezesha kupata ajira ndani ya week moja baada ya kumaliza chuo so nikaanzia life langu la mtaani hostel kiwiziwizi bila warden kujua maana kila nikiamka nilikuwa nabebanisha godoro na mwanafunzi alielipia kihalali. Baada ya ile miezi mitatu nikachukua chumba self kwaTsh 60,000 nikahamia rasmi gheto huku napiga kazi baada ya kama mwaka nikaenda mkoani kikazi nikakaa kama mwaka nikawaachia madogo wa chuo wakae pale gheto.

Nikawa nikirudi nakaa kama siku mbili au tatu nageuza mkoani. Mwishoni kabisa nikaamua kurudisha gheto kwa baba mwenye nyumba wakati huo kazi nyingi nazopiga ni za mkoani. Mpaka sasa nimeoa nipo mjengoni na mke wangu na watoto wetu.

Funzo kwenye huu uzi.
Ukiwa gheto usiwe mtu wa kuwaza mademu wala usitumie gheto lako kama danguro. Tafuta dem mmoja hata kama sio wa malengo ila awe mmoja kisha muda mwingi kuwa bize kutafuta maisha Mungu atakuonyesha njia na mwisho utafanikiwa.

Kwa wale waliopo cho na wanaishi gheto nawashauri msiyaachie hayo magheto hata baada ya chuo anzieni maisha hapo.
 
hongera sana
 
Hapo penye kuliacha geto ndio paliniponza mimi..Thanks mkuu kwa kushare
 
🤣 Nashukuru sana huu uzi, ulinihamasisha nikajipinda, nimechukua kitanda, godoro na kabati vya kuvutia nimehama home, sasa endeleeni kutuma madini zaidi nizidi kuhamasika .... shida ninayopata huku ni vyakula vya kununua havina ubora pia upweke
 
Shukrani
 
[emoji16] hongera mkuu kwa kuchukua hatua,ilo la upweke kamata mpangaji mwenzako
 
Baki nyumbani. Form 2 unataka kupanga? Ugundue nini?
 
Hasara ya vyumba vya bei ya chini kabisa ni usalama na ulinzi wako na mali zako. Hiyo ndio shida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…