Kabla ya kuanza kukaa geto nakumbuka 2012 naingia DAR sina ndugu nimjuae,rafiki,wala jirani nimekuja nataka kuwa na maisha yangu...mkononi nina begi la nguo tu sina Cheti hata cha drs la 7...nimetua Ubungo tu nikawaza leo naenda kulala wapi?
Mfukoni nakumbuka nilikua na 14000 alafu nilikua na simu yangu ya bLACKberry bold,begi zito ntaenda nalo wapi nkawa najiuliza? nikawa nimetoka nnje ya stand ya ubungo nakuja mdg mdg na hii road ya shekilango huku naburuza begi langu usiku huo.
Nikaja mdogo mdogo hadi nikafika manzese Tip Top kufika pale nikapata wazo la kwenda kulala kwanza guest alafu kesho yake pakikucha ntajua cha kufanya..nikavuka road nikaenda ndani ndani huko kutafuta guest ya bei rahisi nikabahatika pata guest sh 7000 nikaingia nikaoga nikabadilisha nguo nikawa nawaza sasa..mkononi nina 7000 tu imebaki.
Akili ikanijia..usiku huo huo nikaamka nikatoka nnje ilikua mida ya saa 7 inaenda 8 usiku nikamkuta mlinzi mbabu anakunywa kahawa basi nikamuita,nikamuuliza "samahani babu,nimetoka safari nina nguo chafu nahitaji mtu wa kuzifua napata wapi maana kesho asubuhi natakiwa kuondoka"..yule babau akaniuliza kwahiyo unataka zifuliwe usiku huu uondoke nazo kesho? nikamwambia hapana nitaziacha nitarudi jioni.
Akanambia hata yeye anaweza kuzifua zitoe tuzihesabu na kuziona...basi nikamtolea tukahesabu nikamwachia,hapo nguo wala hazikua chafu nilitaka tu kupata mtu wakubaki na begi langu la nguo..baada yakukubaliana nikampa kisha nikarudi kulala sasa vizuri..palipokucha kazi yya kutafuta kazi ikaaanza.
Nakumbuka nilienda MOSHI HOTEL ipo pale tip top jikoni nikamkuta mzee mmoja nikamwomba kazi,akaniangalia kisha akanambia hapa kazi za wanaume hamna kuna kazi za wanawake tu kama kuosha vyombo na kufanya usafi,unaweza fanya? nikamwambia Baba mimi nafanya kazi yyte naomba kazi..akanambia pita ndani nakumbuka nilikua nimevaa tracksuit nyekundu ya manchester juu mpk chini na raba zangu..nikaingia ndani nikaonyeshwa karo la vyombo lina vyombo masahani na masufuria..
Nikaanza kuosha sahani zinazotoka kwa wateja kazi ikaendelea hadi muda wa kufunga,nikasugua masufuria makubwa mpk yakatakata,nikapiga deki jiko ki ufupi jiko lili meremeta hiyo siku..maana sio kwa kupanga Kule..baada ya kila kitu yule baba alonipa kazi alikua kashaondoka wafanyakazi tunalipwa na keshia mshika daftari na hela so akanambia nimeambiwa nikupe 4000..Nikapokea nikamshukuru akanambia Poa kesho uwahi mapema basi,nikamjibu sawa.
So nikaondoka usiku huo ilikua mida ya saa 7 hv sina pakulala..nikawa nawaza leo naenda wapi kulala! bahati nzuri nikiwa nazunguka mitaa ile ile kuna pub moja iNaitwa LAMBO HUWA kuna wadada wanajiuzaga hapo so wanakesha 24hrs nikaingia mle ndani nikawa nashangaa pool table,na kuangalia vituko vya mle ndani...
Usingizi ukawa unanishika nikawa natamani sana kulala,nikiwa pale nimesimama nasinzia alikuja BAUNSA akanambia oyaaa hatulali humu nenda kalale kwenuuu,kama ushamaliza kinywaji sepa zako...hapo hapo nikaskia DJ akitangaza "BAUNSA TUSAIDIENI KUTOA NNJE WATU WASIO NA VINYWAJI" BASI baunsa akanambia toka nnje..nikamwambia Mi nasubiri game liishe nicheze pool table,akanambia Chukua kinywaji basi....nikamwambia nletee PEPSI basi akanletea pepsi..wanauza 1000.
Nikawa na pepsi yangu,sasa kwakua nina kinywaji nikatafuta kiti na meza nikakaaa na PEPSI yangu,nikawa siiinywi maana ikiisha unafukuzwa nnje au ununue ingine,basi nkaiweka mezani mimi nkawa nasinzia...ivyo ivyo kufika mida yya saa 10 hivi nikanywa pepsi yangu nikatoka nnje nikarudi kule kazini.
Nikafika nikaingia jikoni nikaanza kukoleza moto na kuweka kila kitu mkao yani...saa 11 wakati boss wa jikoni analeta nyama za supu na kongoro,utumbo anakuta nishakoleza Moto nishachemsha maji nipo naota Moto,akaniuliza DOGO VIPI unaipenda kazi yako eeeeh? SAFI SANA.
Basi tukaosha utumbo tukabandika kwa mara yya kwanza saa 12 na nusu supu ilikua ishaiva SIFA ZOTE kwangu yani..basi maisha yangu yakaendelea hivyo usiku nikitoka kazini naenda LAMBO nanunua soda ya buku nakaa mezani nalala hapo hapo ikifika saa 10 nainywa soda natoka naenda kazini...
Nikifika kazini pale naingia kwenye vyoo vya wateja naoga nafua nguo yangu naikamua naikung'uta naivaaa hyo hyo alafu naenda nakoleza moto chap chap nakaa NAOTA basi nilifanya kazi pale sana hadi siku moja yule boss akanishtukia kuwa sina mahali pakulala akaniuliza unakaa wapi? nikamwambia sina pakukaa nikamuelezea kwa ufupi.
AKanambia nitaongea na meneja wa hii hotel utakua unalala na wafanya usafi wa hapa so utakua unakaa hapa hapa,basi alifanya hivyo nikawa nakaa pale pale hotelini nikawa siendi tena LAMBO,maisha yaliendelea hadi nilipopata vicent vya Kupanga GETO ambapo nakumbuka kwa mara ya kwanza kupanga nilipanga chumba cha 15,000 Maisha yaliendelea vizuri nikapata experiance ya vitu vingi.
kwa sasa naishi kwangu naishi maisha ya Ndoto zangu japo bado nazidi kupambana...
Naosha sufuria kupita maelezo yani mdada ukija kwangu ukagusa sufuria zangu kijinga jinga ukaziacha,nazirudia upya
Napika vyakula hadi wadada nikiwapkiaga wananambia we kaka Umejulia wapi kupika vyakula hivi? jibu ni SIRI YANGU.
Nilikujaga kurudia lile BEGI LANGU la nguo nililoachaga kwa BABU japo alinambiaga nimpe 30,000 na kwakua nilikua nayo wala sikuona shida nilimpaga na nikachukua nguo zangu..maisha yakaendelea.