Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Kabla ya kuanza kukaa geto nakumbuka 2012 naingia DAR sina ndugu nimjuae,rafiki,wala jirani nimekuja nataka kuwa na maisha yangu...mkononi nina begi la nguo tu sina Cheti hata cha drs la 7...nimetua Ubungo tu nikawaza leo naenda kulala wapi?

Mfukoni nakumbuka nilikua na 14000 alafu nilikua na simu yangu ya bLACKberry bold,begi zito ntaenda nalo wapi nkawa najiuliza? nikawa nimetoka nnje ya stand ya ubungo nakuja mdg mdg na hii road ya shekilango huku naburuza begi langu usiku huo.

Nikaja mdogo mdogo hadi nikafika manzese Tip Top kufika pale nikapata wazo la kwenda kulala kwanza guest alafu kesho yake pakikucha ntajua cha kufanya..nikavuka road nikaenda ndani ndani huko kutafuta guest ya bei rahisi nikabahatika pata guest sh 7000 nikaingia nikaoga nikabadilisha nguo nikawa nawaza sasa..mkononi nina 7000 tu imebaki.

Akili ikanijia..usiku huo huo nikaamka nikatoka nnje ilikua mida ya saa 7 inaenda 8 usiku nikamkuta mlinzi mbabu anakunywa kahawa basi nikamuita,nikamuuliza "samahani babu,nimetoka safari nina nguo chafu nahitaji mtu wa kuzifua napata wapi maana kesho asubuhi natakiwa kuondoka"..yule babau akaniuliza kwahiyo unataka zifuliwe usiku huu uondoke nazo kesho? nikamwambia hapana nitaziacha nitarudi jioni.

Akanambia hata yeye anaweza kuzifua zitoe tuzihesabu na kuziona...basi nikamtolea tukahesabu nikamwachia,hapo nguo wala hazikua chafu nilitaka tu kupata mtu wakubaki na begi langu la nguo..baada yakukubaliana nikampa kisha nikarudi kulala sasa vizuri..palipokucha kazi yya kutafuta kazi ikaaanza.

Nakumbuka nilienda MOSHI HOTEL ipo pale tip top jikoni nikamkuta mzee mmoja nikamwomba kazi,akaniangalia kisha akanambia hapa kazi za wanaume hamna kuna kazi za wanawake tu kama kuosha vyombo na kufanya usafi,unaweza fanya? nikamwambia Baba mimi nafanya kazi yyte naomba kazi..akanambia pita ndani nakumbuka nilikua nimevaa tracksuit nyekundu ya manchester juu mpk chini na raba zangu..nikaingia ndani nikaonyeshwa karo la vyombo lina vyombo masahani na masufuria..

Nikaanza kuosha sahani zinazotoka kwa wateja kazi ikaendelea hadi muda wa kufunga,nikasugua masufuria makubwa mpk yakatakata,nikapiga deki jiko ki ufupi jiko lili meremeta hiyo siku..maana sio kwa kupanga Kule..baada ya kila kitu yule baba alonipa kazi alikua kashaondoka wafanyakazi tunalipwa na keshia mshika daftari na hela so akanambia nimeambiwa nikupe 4000..Nikapokea nikamshukuru akanambia Poa kesho uwahi mapema basi,nikamjibu sawa.

So nikaondoka usiku huo ilikua mida ya saa 7 hv sina pakulala..nikawa nawaza leo naenda wapi kulala! bahati nzuri nikiwa nazunguka mitaa ile ile kuna pub moja iNaitwa LAMBO HUWA kuna wadada wanajiuzaga hapo so wanakesha 24hrs nikaingia mle ndani nikawa nashangaa pool table,na kuangalia vituko vya mle ndani...

Usingizi ukawa unanishika nikawa natamani sana kulala,nikiwa pale nimesimama nasinzia alikuja BAUNSA akanambia oyaaa hatulali humu nenda kalale kwenuuu,kama ushamaliza kinywaji sepa zako...hapo hapo nikaskia DJ akitangaza "BAUNSA TUSAIDIENI KUTOA NNJE WATU WASIO NA VINYWAJI" BASI baunsa akanambia toka nnje..nikamwambia Mi nasubiri game liishe nicheze pool table,akanambia Chukua kinywaji basi....nikamwambia nletee PEPSI basi akanletea pepsi..wanauza 1000.

Nikawa na pepsi yangu,sasa kwakua nina kinywaji nikatafuta kiti na meza nikakaaa na PEPSI yangu,nikawa siiinywi maana ikiisha unafukuzwa nnje au ununue ingine,basi nkaiweka mezani mimi nkawa nasinzia...ivyo ivyo kufika mida yya saa 10 hivi nikanywa pepsi yangu nikatoka nnje nikarudi kule kazini.

Nikafika nikaingia jikoni nikaanza kukoleza moto na kuweka kila kitu mkao yani...saa 11 wakati boss wa jikoni analeta nyama za supu na kongoro,utumbo anakuta nishakoleza Moto nishachemsha maji nipo naota Moto,akaniuliza DOGO VIPI unaipenda kazi yako eeeeh? SAFI SANA.

Basi tukaosha utumbo tukabandika kwa mara yya kwanza saa 12 na nusu supu ilikua ishaiva SIFA ZOTE kwangu yani..basi maisha yangu yakaendelea hivyo usiku nikitoka kazini naenda LAMBO nanunua soda ya buku nakaa mezani nalala hapo hapo ikifika saa 10 nainywa soda natoka naenda kazini...

Nikifika kazini pale naingia kwenye vyoo vya wateja naoga nafua nguo yangu naikamua naikung'uta naivaaa hyo hyo alafu naenda nakoleza moto chap chap nakaa NAOTA basi nilifanya kazi pale sana hadi siku moja yule boss akanishtukia kuwa sina mahali pakulala akaniuliza unakaa wapi? nikamwambia sina pakukaa nikamuelezea kwa ufupi.

AKanambia nitaongea na meneja wa hii hotel utakua unalala na wafanya usafi wa hapa so utakua unakaa hapa hapa,basi alifanya hivyo nikawa nakaa pale pale hotelini nikawa siendi tena LAMBO,maisha yaliendelea hadi nilipopata vicent vya Kupanga GETO ambapo nakumbuka kwa mara ya kwanza kupanga nilipanga chumba cha 15,000 Maisha yaliendelea vizuri nikapata experiance ya vitu vingi.

kwa sasa naishi kwangu naishi maisha ya Ndoto zangu japo bado nazidi kupambana...

Naosha sufuria kupita maelezo yani mdada ukija kwangu ukagusa sufuria zangu kijinga jinga ukaziacha,nazirudia upya

Napika vyakula hadi wadada nikiwapkiaga wananambia we kaka Umejulia wapi kupika vyakula hivi? jibu ni SIRI YANGU.

Nilikujaga kurudia lile BEGI LANGU la nguo nililoachaga kwa BABU japo alinambiaga nimpe 30,000 na kwakua nilikua nayo wala sikuona shida nilimpaga na nikachukua nguo zangu..maisha yakaendelea.
Nimetokwa na machozi.... Pole na hongera kwa kuwa na moyo wa uvumilivu..... Mungu akubariki zaidi
 
Hahahaha Ghetho la wadada ukikaribisha marafiki ni kero Nashukuru nimepanga nyumba nzimaa wakija nawatupa chumba cha wageni
Na mnavojua kujazana sasa[emoji1787][emoji1787]
 
Nilikuwa naenda kazin narud nakuta wamelala wanachat na madanga hata hawapiki duuuh na mm kuwakomesha nakula juu kwa juu nawaambia kabichi hilo hapo mwenye njaa apike aisee wakichek mboga kabichi wanainuka kwenda kununua chips na mm naingia room najifungia usingizi mpaka kesho yake nasepa zangu job

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nilikuwa naenda kazin narud nakuta wamelala wanachat na madanga hata hawapiki duuuh na mm kuwakomesha nakula juu kwa juu nawaambia kabichi hilo hapo mwenye njaa apike aisee wakichek mboga kabichi wanainuka kwenda kununua chips na mm naingia room najifungia usingizi mpaka kesho yake nasepa zangu job
Daah mwanmke baharia ww [emoji1373][emoji1373][emoji1373][emoji1787]
 
Safi sana. Nimependa huu ujasiri.
Daaaah nimekumbukaa mbali sana nimemaliza chuo 2015 nimesota mno 2016 nikajilipua nikatoka home kigambon mpaka tabata cna kaz uzur nilikuwa nakila kitu kuanzia godoro kitanda fen redio tv chumba 70k nikalipa six month pesa niliomba nikabakia na laki hiv piga mishe kitaa na laki ikakata maisha yakawa magum sana nikawa nafanya kaz yyte iliyopo mbele yangu nimebeba tofali nimeuza sabun lkn wap baada ya miez mitano nikarudisha mpira kwa kipa nikaenda home nikakaa miez mitano nikasepa tena nikaona nihame mkoa mpaka sasa niko arusha mi siiti gheto naita nyumba sahiv nipo nishazoea
 
Mm nilipanga getho mapema sana kwa sababu wazazi wangu ni watu wa kusafir sana nikaona Hizi kero za kubak home Mara wajomba ma mabinamu wamejazana alafu vurug kwenye kazi wacha nikajipangie zangu sasa marafiki wa kike wengi wanazeekea makwao wakiona hivyo wanakuja kujazana ghetto ili wapate Uhuru wa kudanga vizur
Daah mwanmke baharia ww [emoji1373][emoji1373][emoji1373][emoji1787]
 
Mm nilipanga getho mapema sana kwa sababu wazazi wangu ni watu wa kusafir sana nikaona Hizi kero za kubak home Mara wajomba ma mabinamu wamejazana alafu vurug kwenye kazi wacha nikajipangie zangu sasa marafiki wa kike wengi wanazeekea makwao wakiona hivyo wanakuja kujazana ghetto ili wapate Uhuru wa kudanga vizur
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Acha ni changamoto watatumia vibaya maji umeme vyakula kwenye fridge ukiondoka ukirud ghetto kama jalala aisee na kuwafukuza huwez inabidi uwapige matukio ya juu kwa juu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wakuu mungu ni mkubwa, mimi ni kijana nina miaka 22, saivi nmepata kazi ambayo kidogo itakua inanilipa vizuri tena ya serikali.

ila bado nko chuo ndo naingia mwaka wa 2 saivi, na nyumbani ni mkoani mbali kabisa, na hali ya nyumbani so nzuri kiafya apa naishi kwa ndugu yangu.

sasa apa mawazo ya kupanga ndo yamekuja maan nilkua naogopa kozi kuingi mtaani ivi ivi unaweza kurudisha mpira kwa golikipa.

saivi nawaza kupanga, mwaka huu haupitui wakuu na mimi ntakua na geto langu, yaani nina miaka 22 ila naagizwa vitunguu swaumu aibu sana, tuombeane wakuu
 
Nilikuwa naenda kazin narud nakuta wamelala wanachat na madanga hata hawapiki duuuh na mm kuwakomesha nakula juu kwa juu nawaambia kabichi hilo hapo mwenye njaa apike aisee wakichek mboga kabichi wanainuka kwenda kununua chips na mm naingia room najifungia usingizi mpaka kesho yake nasepa zangu job
Kwanza una moyo!?? Kukaa room moja zaidi ya watu wawili? Hahahahahaah tena maslay kwini hawapendi kupika!!! Hongera bora ulivyoachana nao.

Mimi siwezi, napenda utulivu Muda wote, sipendi mtu ambae hapendi kupika au kufanya usafi. Siku zote nakaa mwenyewe tu
 
Mm nilipanga getho mapema sana kwa sababu wazazi wangu ni watu wa kusafir sana nikaona Hizi kero za kubak home Mara wajomba ma mabinamu wamejazana alafu vurug kwenye kazi wacha nikajipangie zangu sasa marafiki wa kike wengi wanazeekea makwao wakiona hivyo wanakuja kujazana ghetto ili wapate Uhuru wa kudanga vizur
Hahahahahahaha wakae kwako wadange?? Tobaaaaa
 
Nilikuwa naenda kazin narud nakuta wamelala wanachat na madanga hata hawapiki duuuh na mm kuwakomesha nakula juu kwa juu nawaambia kabichi hilo hapo mwenye njaa apike aisee wakichek mboga kabichi wanainuka kwenda kununua chips na mm naingia room najifungia usingizi mpaka kesho yake nasepa zangu job
Ni kweli wengi uwa ni wazinguaji na wanapenda kula vinono ila kupika hawataki
 
Back
Top Bottom