Nunua mchele kilo 30,saga unga wa dona kilo 20,nunua mafuta lita kumi au vile vigalon vya lita 5 viwili, sukari nunua kati ya kilo 10 hadi 15. Weka hapo ndani.
Fanya mpango upate pressure cooker, jiko la gesi la plate mbili na mtu mkubwa wa gesi, halafu friji ile ya milango miwili ya juu na chini chukua za kisasa kama Hisense hizi ndio nzuri. Nunua blender.
Unapika maharage kilo moja kwenye pressure cooker, unaweka kwenye friji kazi yako inakuwa ni kuyachota na robo unaunga unakula mara nne yaani asubuhi mchana jioni na asubuhi tena siku inayofuata breakfast.
Wali ukipika unaweza kula mchana, jioni asubuhi na ukafika tena mchana siku ya pili kama kiporo. Friji litakusaidia sana kutunza vyakula muda mrefu.
Pressure cooker itakusaidia sana kupika vyakula kwa muda mfupi kwa gharama nafuu. Stock hiyo ya chakula ukiitumia vizuri itakuvusha mwezi mzima au miezi hata miwili bila kuhangaika na vyakula.