Ulianzaje kukaa gheto?

Mimi kwenda kukaa gheto haki nilifosi,yaani wazazi walikua wabishi kukubali woiii ikabidi niingie gharama ya kutafuta chuo niongezee elimu,nikaondoka home kwa kigezo cha kwenda kujisomea nikaenda kupanga ilala mchikichin karibu na kiwanda cha bia lol.

Aisee kile kiwanda cha bia kilinifanya niwe nalewa kila mara maana ule upepo wa pombe ukivuma nahisi mawenge[emoji23].Tokea hapo ndo ukawa mwanzo wa kujitegemea.
 
Vizuri
 
Hahaa wewe utakua mchaga[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aiseee [emoji1787]
 
Huyo alikuwa zaidi ya danga
 
Mi nimeanza maisha ya geto toka nikiwa na miaka 20 tu,,hadi saiv miongo kadhaa imepita.

Ila sina sijanunua na sitanunua jiko milele maana sipendi kupika balaa.
Anza kupika boss[emoji1787]
 
mm akili ya geto nimeipata baada ya fundi mmoja alikuwa ametengeneza bed kali alafu mteja wake haeleweki lile bed akaniuzia kwa 200k pale ndio nikapata mzuka aisee nikapambana nikanunua godoro nikaweka darini na kitanda nikanunua sofa nikaweka store hapo bado niko home mzee nikanunua showcase nikaweka store.

mzee ugali wa bure mtamu asikuambie mtu mziki nilikuwa nao pamoja na desktop siku nikasaka kodi nikapata mazee nikawaaga kwa mbwembwe zote geto nikahamia wakuu nikahamia ile siku ya kwanza sikulala joto la kufa mtu kwa hasira nikarudi home nikasema huku siji hadi nipate feni.

Hahaa kama wiki hivi nikarudi na feni aisee maisha ya geto ni swafi hadi leo niko zangu geto mzee ananambia chumba chako vipi hukitaki namwambiaga hakina hajaaaa.

Miaka kadhaa sasa nipo geto full amani geto limesheheni hadi nikitembelewa naulizwa vipi utaoa lini. [emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…