Ulianzaje kukaa gheto?

Baada ya kupata kazi mkoa mwengine
 
daa umefanya uzembe kama wangu,nikiwa shule nilikua nakaa na manzi tukanunua kila kitu kwa malengo baada ya shule tuanze maisha.

akiba tukiwa na m.1 na laki 6, uoga kitu cha ajabu sana nikaona ntafanya nini nikala kona kurudi home nikamuachia manzi kila kitu. alinililia sana nirudi ila ule uoga haukuwa wa nchi hii

now nimepanga ila najilaumu sana kumkimbia yule manzi kwa uoga wa maisha mji wa watu
 
mkuu utakuta unachepuka
 
Daah kwel mkuu...ila ulitisha kurud kupambana upya.....manz kwaiyo akalisongesha mwenyew? Si ungerud tu mkuu
 
Hahah nice mkuu...ilikua kibingwa sana hiyo
 
Baaada ya kumaliza chuo mwaka jana....nikaaanza piga harakati za kutafuta hela through temporary work...ni miez minne sasa imepita toka nimeanza maisha ya kuishi gheto. Pamoja na changamoto za hapa na pale...kila mwezi gheto naona linabadilika...bado kidogo nitalipiku gheto la mangwair..
 
Ume ni inspire sana mkuu, nimeamini maisha hayana formula kwani popote yanaanzia na siku zote safari moja huleta safari nyingine, na upendo wa shemeji yetu unaoekana dhahiri siyo wa kinafiki, kwani sidhani kama kuna msichana wa chuo ambaye ataacha mambo ya kula bata na kuamua kukomaa na msela mpaka kuhitimu.
 
Umetupa somo zuri sana mkuu
 
Ulivyokuwa unaanza kuelezea nilikuchukulia poa, but hadi sasa nadiriki kusema " you are an inspiration ".
 
Mh! hii ya leo balaa,,, kila MTU nilipomaliza chuo,, ooh! First year, watu tumetoka mbali... Kitendo cha kumaliza la saba ndo tiketi ya kuhama nyumbani. Nakumbuka kauli ya mzee huu ndo mlo wako wa mwisho cha ajabu sikumuelewa kilichonikuta asbuh nilijikuta natimuliwa ndani kama mbwa koko aliyekosea njia.nikijichek nimevaa kaptula na kaushi nikajichanganya kitaa.. okota skrepa sana!! nikajichanganya car wash zoote nikawa najulikan mwish wa siku nikaingia geleji. Ila geto letu ndo lilikua balaa watu 14 chin maboksi utajua pakula alafu kunuka kam beberu ilikua kawaida
 
Hahaha msoto kama wote mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…