Ulianzaje kukaa gheto?

Mke wa mtu ndio alifanya nianze kuishi ghetto peke yangu. Mpaka leo hua nnamshukuru saana yule dada. Wanawake mnaakili saana [emoji109][emoji109][emoji109] niwe mkweli bila yy mpaka sasa ningekua nnaishi ghetto na masela yan full mvululu. Mwanamke alijua kunishauri yule alinipa msaada wa kila ninacho hitaji ili niweze kuishi peke yangu. Mungu ni mwema niliweza kutoka kwenye ghetto changanyikeni mpaka kuishi mwenyewe. Sasa nnaujua uchungu wa kodi, uchungu wa vitu nilivyonunua kwa senti zangu. Uchungu wa kulipia bills, utamu wa ghetto na uchungu wake. Yote kwa yote Kuna wanawake wanajua kushauri aisee! Ila ndio vile washaolewa n mijamaa mibandidu yani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa
 
Nilivyomaliza chuo tu nikapata kibarua cha kujishikiza na walikuwa wananilipa 100k kwa mwezi,chakula na usafiri bure nikaona si sawa na kukaa home,bora nikubali.

Sasa baada ya miezi mitatu tu kuanza kibarua,maneno yakaanza naanza lini kujitegemea,mana hapo nilikuwa naishi kwa baba mdogo.

Nikaona si kesi mwezi uliofuatia nikanunua godoro,nikatafuta chumba nikapata cha elf 15,kwasababu sikuwa na vitu vingi nikamuomba jamaa mmoja muuza maji anibebee vitu vyangu kwenye mkokoteni wake nikampoza elfu 2,ndo maisha yakaanza hapo mwaka 2007 hadi leo nashukuru Mungu nilishasimama vizuri.
 
Hongera sn mkuu
 
yupo pale....
 
Nilipanga kuhama home mwezi huu Nimelipa kila kitu tayari changamoto bado napapenda home Kama Nina kauoga hivi kila siku nasema kesho nahamia jumamosi jumapili hii week ya 3 sasa napeleka nanunua vitu nikitoka mission napeleka Baada ya muda nafunga mlango narudi home nasema bado bado

Maombi yenu jamani wadau


N.B motisha imetokea kwenye huu uzi nilipania mwaka huu naenda kwangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahah mkuu siku utapolala kwako hutatamani kurudi home bwana Transporter
 
Unafanana na mimi mkuu.
Imagine naenda kukaa peke yangu, hamna mtu wa kuongea naye nikichoka kujifungia room
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…