Ulianzaje kukaa gheto?

Aisee mkuu kwanza hongera sana kwa kuchukua hatua madhubuti,hongera pia kw kupambania kombe mpaka saiz upo getoni kwako...

Pia nafurah kuona shuhuda kama hzi kweny huu uzi.. hatumuachi mtu nyuma lazma wana wote tusepe hom.....

Kama ungeweza elezea hyo formula ya commerce hata kwa ufupi..huenda ikasaidia na wengne..mana issue sio unapata sh ngap.. issue unatumia sh ngapi..

Big up sana mdau...[emoji119]
 
Nimetumia dakika 4 kusoma post yako mkuu other time highlights inatosha ila congratulations
 
Nimetumia dakika 4 kusoma post yako mkuu other time highlights inatosha ila congratulations
Asante kaka na sorry kwa usumbufu...By the way, napenda sana kuandika hasa ikiwa ni mtiririko kama story..Ila asante kwa ushauri, next time nitauzingatia ili hata wale wasioweza kusoma story ndefu wasiache bila kupata ujumbe uliokusudiwa 🀝
 
Mkuu...asante sana na naahidi nitaielezea (kwa jinsi ninavyoelewa) then tutashea madini...ila pia naomba utupe mrejesho wako binafsi, ukiwa kama mwanzilishi wa huu uzi, toka 2018 hadi leo plan yako imefikia wapi..tunaomba mrejesho mkuu!!!
 
Mkuu...asante sana na naahidi nitaielezea (kwa jinsi ninavyoelewa) then tutashea madini...ila pia naomba utupe mrejesho wako binafsi, ukiwa kama mwanzilishi wa huu uzi, toka 2018 hadi leo plan yako imefikia wapi..tunaomba mrejesho mkuu!!!
Oke mkuu tunasubr hyo formula...

Mkuu mrejesho nilishatoa mda sana...siku update kweny thread nilifanya kupost tu kama members wengne..nashukuru nilifanikiwa kusepa...nipo mitaa ya kimara kwa sasa...
 
Oke mkuu tunasubr hyo formula...

Mkuu mrejesho nilishatoa mda sana...siku update kweny thread nilifanya kupost tu kama members wengne..nashukuru nilifanikiwa kusepa...nipo mitaa ya kimara kwa sasa...
Sawa mkuu.. mda sio mrefu nitaipost
 
Oke mkuu tunasubr hyo formula...

Mkuu mrejesho nilishatoa mda sana...siku update kweny thread nilifanya kupost tu kama members wengne..nashukuru nilifanikiwa kusepa...nipo mitaa ya kimara kwa sasa...
ELIMU KIDOGO KUHUSU CAPITAL FORMATION...Sorry kwa wasiopenda kusoma msg ndefu πŸ‘

Nilipokuwa High school, moja ya somo nililosoma kwenye combination yangu ni ECONOMICS na ndani ya hili somo tulifundishwa capital formation.

Capital formation au kwa lugha isiyo rasmi ni KUKUSANYA MTAJI. Yes, ni kitendo cha kuweka akiba (saving) ya kidogo unachokipata ili kiweze kukufaa kesho. Watu wengi tunashindwa kuweka akiba kwa sababu nyingi, kuu hasa ni

1. Sio wavumilivu yaani tunataman tukuze akiba haraka kwa kusave hela kubwa, hatuamini katika kusave kidogo kidogo mara nyingi na kusubili muda mrefu (Binafsi ilinibidi nisubili miezi 8 kabla ya kupata hela ya kutosha kodi. Nilianza saving toka November mwaka jana hata kabla sijapata ajira, kodi nimeitimiza July...KUJINYIMA + UVUMILIVU.

2. Tunaamini tunapata hela kila siku so hatuna hofu ya kesho. Mfano kuna mtu ana uwezo wa kupata wastani wa 3000 kila siku,huyu muda mwingine hawezi iona thamani ya kuweka 1000 kwasababu anaona hata akiitumia sio mbaya maana na kesho anaipata..WRONG PERCEPTION...Tujitahidi kuwa na hofu ya Kesho.

NB: Saving nzuri ni ile ambayo ukisave hauipunguzi piga ua (naongea na watu ambao leo wataweka akiba kesho wanaipunguza kidogo afu keshokutwa wanaweka tena). Sasa, ili kuweza kusave bila kupunguza, fanya hivi:-

Mfano umebeti ukapata 20, 000, usiweke akiba 15000 maana lazima utaitoa tu. Chakufanya weka akiba kiasi kidogo labda 5000, then baki na 15000 ambayo itakulinda hadi upate zali jingine. Kwasisi ambao hatuna kipato cha uhakika cha kupata kila siku, tujaribu kuweka angalau 30% ya hela tunayopata ili 70% itulinde. ila kama una uhakika wa kupata 10000 kila siku, weka akiba hata 60% daily...na ile inayobaki kulinda mfuko uitumie kibahili/kwa utaratibu..Ukifanya hivi, saving itakaa..

Kama binadamu, tuna challenge nying zinazoharibu akiba zetu, ila chagua challenge za kukufanya ukachukue akiba yako.sio kila tatizo unawahi kuchukua kwenye kibubu..Usikae na akiba ndani au kwenye simu, iweke benki (kwasisi waweka akiba NMB CHAPCHAP A/C ndio mkombozi wetu, haina makato).

SITAKI kuandika sana, mwanangu mkuu Saint hapendi sana kusoma 😁 (joke)...la mwisho, kuna matumizi ya kila siku sio muhimu..usipokaa sawa unaweza unga 3000 mara mbili kwa wiki (6000 hapa huwezi toboa). Sawa, lazima tukae online maana ndo kuna matangazo ya ajira ila mitandao ming inakula bundle mfno insta au whatsapp status....JF iko fair sana kwenye bundle so 90% ya updates za ajira unazozipata kwenye mitandao mingine zinapatikana JUKWAA LA AJIRA NA TENDA hapa JF..Ukiwa unapitia huko bundle litakaa na utasave hiyo 3000..Kama bundle linakumalizia pesa aisee fanya hivyo nilivyoshauri ila tu uwe hewani kwa normal calls 24/7.....MAY GOD BLESS OUR HUSTLES.

FOHADI: Focus Hadwork Discpline
 
Asante sana mkuu..ubarkiwe sana
 
Hii ni nzuri sana kwa wadau wa mageto shukran mkuu
 
Mimi bado nipo om illa nmeshanunua kitanda 5x6 na godoro lake ,pia nmenunua mtungi wa gas kitaa tu hapa ,meza na stuli zake mbili na vidude vingne vidogo vidogo kama sufuria mapazia na ndoo na vyombo vya kulia. Na pesa hta ya kupanga chumba miezi sita nnayo na pesa ya kunua chakula cha kuanzia nnayo na inanibakia akiba kama 300k . Lakini changamoto inayonikwamisha nmekosa mishe ya kunisaidia kuzngusha ela kwa sasa ndo kinachonipa waswas hta nkichomoka home naweza nkafeli mapema ikawa shida tena .

Naombeni ushauri ndugu zangu nifanyeje?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…