Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Nimekuwa mfatiliaji wa jamii forum kwa muda mrefu sasa, takribani miaka 3 nimekuwa nikipita na kupata updates mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusoma mikasa tofauti tofauti.

Mara ya kwanza nakutana na hii thread ilikuwa mwezi march mwaka huu 2020, enzi hizo corona ndio imeingia Tanzania. Nilikuwa nimerudisha mpira kwa kipa (nilimaliza chuo mwaka jana chuo kimoja maarufu hapa jijini, badae nikaona nisiende home kwa bimkubwa Temeke, bora niende kwa uncle wangu anaishi eneo moja maarufu wilaya ya Ilala). Nilienda kwa uncle coz ye ni hustler wa mtaani nikaaona bora nijichanganye nae ili tu nisikae home kwa bimkubwa kizembe.. Namshukuru Mungu yalikuwa ni maamuzi sahihi zaidi niliyoyafanya kuhusu kesho yangu. Bahati nzuri nilikuwa na vyombo kadhaa vya ndani (nilinunua kipindi niko chuo), nilichofanya ni kubeba vyombo vyangu na kuvihifdhi kwa uncle. Huku nyuma bimkubwa namwambia nimepanga kumbe nisharudisha mpira kwa uncle (sikutaka kumpa bimkubwa stress).​

Toka niione hii thread, nilihamasika sana sana na nikaomba Mungu anisaidie kabla huu mwaka haujaisha niwe nimerudi getto kwangu. Aiseee, nilijibana, vitu visivyo vya lazima kama nguo, kuangalia mechi kila week wakati bukubuku zinapotea nikapunguza..Niliuheshimu mtaa, nikawa napiga kila kazi halali, nimesaidia mafundi umeme site, nimesomba maji kwenye mkokoteni, nimemsaidia uncle kazi zake anazofanya kwa ujira mdogo kama kukata miti, kubeba mizigo ya watu kwenye toroli..Nilikuwa eneo ambalo hakuna mtu anaenijua (Niliogopa kurudi kwa bimkubwa maana nisingekuwa free kufanya hizi kazi coz ningewaza watanionaje, hii ni changamoto kubwa sana na inahitaji ujasiri mkubwa sana na wachache wanaweza, naamini hata wanaowashauri vijana kuondoa aibu, hawawezi hii kitu).

Mungu ni mwema, nikabahatika kupata internship kampuni moja, wakawa wananisupport kwa allowance kidogo, akili kichwani kwangu sasa, nikaishi kibahili sana, nikaweka sana akiba, nikapunguza matumizi yasiyo ya lazima..Nikatumia knowledge ya capital foramation through saving (waliosoma commerce watanielewa). Kupitia hiyo allowance ndogo (naithamini sana) niliamini nitapiga hatua na kujenga kesho yangu iliyo bora. Nilijitahidi kupiga kazi kwa bidii nikiamini kuwa hii nafasi niliyoipata ni kama zali tu la mentali maana haikuwa na connection na kiukweli sina connection, niliamini juhudi yangu na kujituma ndo itafanya nipewe extended contract. Niliyakumbuka maneno ya jasiri muongoza njia (RIP), Nafasi, jina halafu Pesa (If you know you know), nikasema nimepata nafasi, natengeneza jina theni pesa zitakuja..Ndani ya miezi 6, nilihakikisha nusu ya posho yangu inakaa akiba, nilijua kidogo ukikiweka sana kinakuwa kikubwa, hatimae tarehe za mwishoni mwezi wa 7 nikalipia room yangu mkataba wa miezi 6.

Hii THREAD ilinihamasisha sana, ilinipa tamaa nikasema eenh Mungu nisaidie. Leo hii nalala kwangu, nimeridhika napo na ni getto kali sana..Naweza nikajibana hata miezi 4 ili kuja kununua asset ya kudumu..Now kila mgeni anaekuja getto kwangu (ambae hajui story yangu) akiliona getto anahisi mimi nina hela kumbe mipango tu na malengo.

Nimejifunza kuwa, there is no perfect time in life, just take the time and make it perfect. Pengine ningerudi home kwa bimkubwa nisingekuwa hapa leo, hata kusaidia mafundi na kusomba ,aji ningeona aibu, ila kuwa mbali na home kumenifanya nifungue milango mingi sana. Bado sijafika ila angalau leo nafurahia maamuzi niliyoyafanya miezi 11 iliyopita (kurudi kwa uncle). Marafiki zangu wananiona mimi bahili sana ila hawajui kuwa najinyima ili niweke misingi ya kesho vizuri (najinyima vyote ila sio msosi, nakula vizuri na nakula ninachotaka coz kupika is cheap).

KWA WANANGU WOTE TUNAOHASO:

Aiseee, najua baadhi mtakuwa mnapitia kipindi kigumu sana now, pengine matamanio nia makubwa kuliko uhalisia..Nataka niwaambie kuwa this is temporary, yana mwisho ila tu tusikate tamaa..Hiyo 2000 ambayo unaiona ndogo na kuunga bundle mara kibao kwa week bila mpangilio ukiamua kuitunza mara 50 itakuwa ni laki moja ambayo unalipia kodi miezi 3 (mikoani unapata room kali sana)...Tuzidi kupambana, tuzidi kuweka akiba...no one knows tommorow, pengine after 1 year ukawa mbele ya wengi waliokutangulia...Kuna mwanangu aliwahi kupata getto mda mrefu kabla yangu (bahati mbaya namfundisha ubahili positive hanielewi), leo akiliona getto langu analitamani na kujiona kuwa amechelewa kuweka malengo ikizingatia ana kipato kikubwa kuliko mimi. Huwezi amini leo anaomba kutumia getto langu kuvutia mademu wakati analo lake hahahaahahahha namimi simpi hata siku 1..By the way, naishi vyema na washikaji zangu, tunasapotiana sana ila kitu kimoja tu ambacho nawenyewe wanakijua kutoka kwangu, nishawambia sitakuja kumpa mtu yeyote getto langu alale na pisi kali..Hii ni sheria nimeiweka inayoapply kwa wote na wanaelewa..Pengine ni roho mbaya ila kwangu mimi getto langu ndio nyumba yangu, pale kitandani ndipo napumzisha akili yangu inayowaza jinsi gani nitatoboa katika maisha, so naheshimu kwangu zaidi ya ninavyojiheshimu...

All the best wakuu, wakati wa Mungu ni wakati sahihi ila tusiache kuuforce kila wakati kuufanya uwe sahihi ili Mungu aupe kibali chake....!!!!..Huu uzi ulinifanya nijiunge rasmi JF mwezi wa 7 na leo nimeleta ushuhuda kwenu..I'm so grateful to the writer of this thread....This is a testimony from the invisible reader of the thread.

FOHADI: Focus Hardwork Discpline
Aisee mkuu kwanza hongera sana kwa kuchukua hatua madhubuti,hongera pia kw kupambania kombe mpaka saiz upo getoni kwako...

Pia nafurah kuona shuhuda kama hzi kweny huu uzi.. hatumuachi mtu nyuma lazma wana wote tusepe hom.....

Kama ungeweza elezea hyo formula ya commerce hata kwa ufupi..huenda ikasaidia na wengne..mana issue sio unapata sh ngap.. issue unatumia sh ngapi..

Big up sana mdau...[emoji119]
 
Nimetumia dakika 4 kusoma post yako mkuu other time highlights inatosha ila congratulations
 
Asante kaka na sorry kwa usumbufu...By the way, napenda sana kuandika hasa ikiwa ni mtiririko kama story..Ila asante kwa ushauri, next time nitauzingatia ili hata wale wasioweza kusoma story ndefu wasiache bila kupata ujumbe uliokusudiwa 🤝
 
Aisee mkuu kwanza hongera sana kwa kuchukua hatua madhubuti,hongera pia kw kupambania kombe mpaka saiz upo getoni kwako...

Pia nafurah kuona shuhuda kama hzi kweny huu uzi.. hatumuachi mtu nyuma lazma wana wote tusepe hom.....

Kama ungeweza elezea hyo formula ya commerce hata kwa ufupi..huenda ikasaidia na wengne..mana issue sio unapata sh ngap.. issue unatumia sh ngapi..

Big up sana mdau...[emoji119]
Mkuu...asante sana na naahidi nitaielezea (kwa jinsi ninavyoelewa) then tutashea madini...ila pia naomba utupe mrejesho wako binafsi, ukiwa kama mwanzilishi wa huu uzi, toka 2018 hadi leo plan yako imefikia wapi..tunaomba mrejesho mkuu!!!
 
Baada ya mihangaiko
JPEG_20201008_182343_3123300767226221401.jpg
 
Mkuu...asante sana na naahidi nitaielezea (kwa jinsi ninavyoelewa) then tutashea madini...ila pia naomba utupe mrejesho wako binafsi, ukiwa kama mwanzilishi wa huu uzi, toka 2018 hadi leo plan yako imefikia wapi..tunaomba mrejesho mkuu!!!
Oke mkuu tunasubr hyo formula...

Mkuu mrejesho nilishatoa mda sana...siku update kweny thread nilifanya kupost tu kama members wengne..nashukuru nilifanikiwa kusepa...nipo mitaa ya kimara kwa sasa...
 
Sawa mkuu.. mda sio mrefu nitaipost
 
Oke mkuu tunasubr hyo formula...

Mkuu mrejesho nilishatoa mda sana...siku update kweny thread nilifanya kupost tu kama members wengne..nashukuru nilifanikiwa kusepa...nipo mitaa ya kimara kwa sasa...
ELIMU KIDOGO KUHUSU CAPITAL FORMATION...Sorry kwa wasiopenda kusoma msg ndefu 👍

Nilipokuwa High school, moja ya somo nililosoma kwenye combination yangu ni ECONOMICS na ndani ya hili somo tulifundishwa capital formation.

Capital formation au kwa lugha isiyo rasmi ni KUKUSANYA MTAJI. Yes, ni kitendo cha kuweka akiba (saving) ya kidogo unachokipata ili kiweze kukufaa kesho. Watu wengi tunashindwa kuweka akiba kwa sababu nyingi, kuu hasa ni

1. Sio wavumilivu yaani tunataman tukuze akiba haraka kwa kusave hela kubwa, hatuamini katika kusave kidogo kidogo mara nyingi na kusubili muda mrefu (Binafsi ilinibidi nisubili miezi 8 kabla ya kupata hela ya kutosha kodi. Nilianza saving toka November mwaka jana hata kabla sijapata ajira, kodi nimeitimiza July...KUJINYIMA + UVUMILIVU.

2. Tunaamini tunapata hela kila siku so hatuna hofu ya kesho. Mfano kuna mtu ana uwezo wa kupata wastani wa 3000 kila siku,huyu muda mwingine hawezi iona thamani ya kuweka 1000 kwasababu anaona hata akiitumia sio mbaya maana na kesho anaipata..WRONG PERCEPTION...Tujitahidi kuwa na hofu ya Kesho.

NB: Saving nzuri ni ile ambayo ukisave hauipunguzi piga ua (naongea na watu ambao leo wataweka akiba kesho wanaipunguza kidogo afu keshokutwa wanaweka tena). Sasa, ili kuweza kusave bila kupunguza, fanya hivi:-

Mfano umebeti ukapata 20, 000, usiweke akiba 15000 maana lazima utaitoa tu. Chakufanya weka akiba kiasi kidogo labda 5000, then baki na 15000 ambayo itakulinda hadi upate zali jingine. Kwasisi ambao hatuna kipato cha uhakika cha kupata kila siku, tujaribu kuweka angalau 30% ya hela tunayopata ili 70% itulinde. ila kama una uhakika wa kupata 10000 kila siku, weka akiba hata 60% daily...na ile inayobaki kulinda mfuko uitumie kibahili/kwa utaratibu..Ukifanya hivi, saving itakaa..

Kama binadamu, tuna challenge nying zinazoharibu akiba zetu, ila chagua challenge za kukufanya ukachukue akiba yako.sio kila tatizo unawahi kuchukua kwenye kibubu..Usikae na akiba ndani au kwenye simu, iweke benki (kwasisi waweka akiba NMB CHAPCHAP A/C ndio mkombozi wetu, haina makato).

SITAKI kuandika sana, mwanangu mkuu Saint hapendi sana kusoma 😁 (joke)...la mwisho, kuna matumizi ya kila siku sio muhimu..usipokaa sawa unaweza unga 3000 mara mbili kwa wiki (6000 hapa huwezi toboa). Sawa, lazima tukae online maana ndo kuna matangazo ya ajira ila mitandao ming inakula bundle mfno insta au whatsapp status....JF iko fair sana kwenye bundle so 90% ya updates za ajira unazozipata kwenye mitandao mingine zinapatikana JUKWAA LA AJIRA NA TENDA hapa JF..Ukiwa unapitia huko bundle litakaa na utasave hiyo 3000..Kama bundle linakumalizia pesa aisee fanya hivyo nilivyoshauri ila tu uwe hewani kwa normal calls 24/7.....MAY GOD BLESS OUR HUSTLES.

FOHADI: Focus Hadwork Discpline
 
ELIMU KIDOGO KUHUSU CAPITAL FORMATION...Sorry kwa wasiopenda kusoma msg ndefu [emoji106]

Nilipokuwa High school, moja ya somo nililosoma kwenye combination yangu ni ECONOMICS na ndani ya hili somo tulifundishwa capital formation.

Capital formation au kwa lugha isiyo rasmi ni KUKUSANYA MTAJI. Yes, ni kitendo cha kuweka akiba (saving) ya kidogo unachokipata ili kiweze kukufaa kesho. Watu wengi tunashindwa kuweka akiba kwa sababu nyingi, kuu hasa ni

1. Sio wavumilivu yaani tunataman tukuze akiba haraka kwa kusave hela kubwa, hatuamini katika kusave kidogo kidogo mara nyingi na kusubili muda mrefu (Binafsi ilinibidi nisubili miezi 8 kabla ya kupata hela ya kutosha kodi. Nilianza saving toka November mwaka jana hata kabla sijapata ajira, kodi nimeitimiza July...KUJINYIMA + UVUMILIVU.

2. Tunaamini tunapata hela kila siku so hatuna hofu ya kesho. Mfano kuna mtu ana uwezo wa kupata wastani wa 3000 kila siku,huyu muda mwingine hawezi iona thamani ya kuweka 1000 kwasababu anaona hata akiitumia sio mbaya maana na kesho anaipata..WRONG PERCEPTION...Tujitahidi kuwa na hofu ya Kesho.

NB: Saving nzuri ni ile ambayo ukisave hauipunguzi piga ua (naongea na watu ambao leo wataweka akiba kesho wanaipunguza kidogo afu keshokutwa wanaweka tena). Sasa, ili kuweza kusave bila kupunguza, fanya hivi:-

Mfano umebeti ukapata 20, 000, usiweke akiba 15000 maana lazima utaitoa tu. Chakufanya weka akiba kiasi kidogo labda 5000, then baki na 15000 ambayo itakulinda hadi upate zali jingine. Kwasisi ambao hatuna kipato cha uhakika cha kupata kila siku, tujaribu kuweka angalau 30% ya hela tunayopata ili 70% itulinde. ila kama una uhakika wa kupata 10000 kila siku, weka akiba hata 60% daily...na ile inayobaki kulinda mfuko uitumie kibahili/kwa utaratibu..Ukifanya hivi, saving itakaa..

Kama binadamu, tuna challenge nying zinazoharibu akiba zetu, ila chagua challenge za kukufanya ukachukue akiba yako.sio kila tatizo unawahi kuchukua kwenye kibubu..Usikae na akiba ndani au kwenye simu, iweke benki (kwasisi waweka akiba NMB CHAPCHAP A/C ndio mkombozi wetu, haina makato).

SITAKI kuandika sana, mwanangu mkuu Saint hapendi sana kusoma [emoji16] (joke)...la mwisho, kuna matumizi ya kila siku sio muhimu..usipokaa sawa unaweza unga 3000 mara mbili kwa wiki (6000 hapa huwezi toboa). Sawa, lazima tukae online maana ndo kuna matangazo ya ajira ila mitandao ming inakula bundle mfno insta au whatsapp status....JF iko fair sana kwenye bundle so 90% ya updates za ajira unazozipata kwenye mitandao mingine zinapatikana JUKWAA LA AJIRA NA TENDA hapa JF..Ukiwa unapitia huko bundle litakaa na utasave hiyo 3000..Kama bundle linakumalizia pesa aisee fanya hivyo nilivyoshauri ila tu uwe hewani kwa normal calls 24/7.....MAY GOD BLESS OUR HUSTLES.

FOHADI: Focus Hadwork Discpline
Asante sana mkuu..ubarkiwe sana
 
Hii ni nzuri sana kwa wadau wa mageto shukran mkuu
 
Mimi bado nipo om illa nmeshanunua kitanda 5x6 na godoro lake ,pia nmenunua mtungi wa gas kitaa tu hapa ,meza na stuli zake mbili na vidude vingne vidogo vidogo kama sufuria mapazia na ndoo na vyombo vya kulia. Na pesa hta ya kupanga chumba miezi sita nnayo na pesa ya kunua chakula cha kuanzia nnayo na inanibakia akiba kama 300k . Lakini changamoto inayonikwamisha nmekosa mishe ya kunisaidia kuzngusha ela kwa sasa ndo kinachonipa waswas hta nkichomoka home naweza nkafeli mapema ikawa shida tena .

Naombeni ushauri ndugu zangu nifanyeje?.
 
Back
Top Bottom