Walec
JF-Expert Member
- Apr 22, 2017
- 1,364
- 3,326
- Thread starter
- #1,661
Aisee mkuu kwanza hongera sana kwa kuchukua hatua madhubuti,hongera pia kw kupambania kombe mpaka saiz upo getoni kwako...Nimekuwa mfatiliaji wa jamii forum kwa muda mrefu sasa, takribani miaka 3 nimekuwa nikipita na kupata updates mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusoma mikasa tofauti tofauti.
Mara ya kwanza nakutana na hii thread ilikuwa mwezi march mwaka huu 2020, enzi hizo corona ndio imeingia Tanzania. Nilikuwa nimerudisha mpira kwa kipa (nilimaliza chuo mwaka jana chuo kimoja maarufu hapa jijini, badae nikaona nisiende home kwa bimkubwa Temeke, bora niende kwa uncle wangu anaishi eneo moja maarufu wilaya ya Ilala). Nilienda kwa uncle coz ye ni hustler wa mtaani nikaaona bora nijichanganye nae ili tu nisikae home kwa bimkubwa kizembe.. Namshukuru Mungu yalikuwa ni maamuzi sahihi zaidi niliyoyafanya kuhusu kesho yangu. Bahati nzuri nilikuwa na vyombo kadhaa vya ndani (nilinunua kipindi niko chuo), nilichofanya ni kubeba vyombo vyangu na kuvihifdhi kwa uncle. Huku nyuma bimkubwa namwambia nimepanga kumbe nisharudisha mpira kwa uncle (sikutaka kumpa bimkubwa stress).
Toka niione hii thread, nilihamasika sana sana na nikaomba Mungu anisaidie kabla huu mwaka haujaisha niwe nimerudi getto kwangu. Aiseee, nilijibana, vitu visivyo vya lazima kama nguo, kuangalia mechi kila week wakati bukubuku zinapotea nikapunguza..Niliuheshimu mtaa, nikawa napiga kila kazi halali, nimesaidia mafundi umeme site, nimesomba maji kwenye mkokoteni, nimemsaidia uncle kazi zake anazofanya kwa ujira mdogo kama kukata miti, kubeba mizigo ya watu kwenye toroli..Nilikuwa eneo ambalo hakuna mtu anaenijua (Niliogopa kurudi kwa bimkubwa maana nisingekuwa free kufanya hizi kazi coz ningewaza watanionaje, hii ni changamoto kubwa sana na inahitaji ujasiri mkubwa sana na wachache wanaweza, naamini hata wanaowashauri vijana kuondoa aibu, hawawezi hii kitu).
Mungu ni mwema, nikabahatika kupata internship kampuni moja, wakawa wananisupport kwa allowance kidogo, akili kichwani kwangu sasa, nikaishi kibahili sana, nikaweka sana akiba, nikapunguza matumizi yasiyo ya lazima..Nikatumia knowledge ya capital foramation through saving (waliosoma commerce watanielewa). Kupitia hiyo allowance ndogo (naithamini sana) niliamini nitapiga hatua na kujenga kesho yangu iliyo bora. Nilijitahidi kupiga kazi kwa bidii nikiamini kuwa hii nafasi niliyoipata ni kama zali tu la mentali maana haikuwa na connection na kiukweli sina connection, niliamini juhudi yangu na kujituma ndo itafanya nipewe extended contract. Niliyakumbuka maneno ya jasiri muongoza njia (RIP), Nafasi, jina halafu Pesa (If you know you know), nikasema nimepata nafasi, natengeneza jina theni pesa zitakuja..Ndani ya miezi 6, nilihakikisha nusu ya posho yangu inakaa akiba, nilijua kidogo ukikiweka sana kinakuwa kikubwa, hatimae tarehe za mwishoni mwezi wa 7 nikalipia room yangu mkataba wa miezi 6.
Hii THREAD ilinihamasisha sana, ilinipa tamaa nikasema eenh Mungu nisaidie. Leo hii nalala kwangu, nimeridhika napo na ni getto kali sana..Naweza nikajibana hata miezi 4 ili kuja kununua asset ya kudumu..Now kila mgeni anaekuja getto kwangu (ambae hajui story yangu) akiliona getto anahisi mimi nina hela kumbe mipango tu na malengo.
Nimejifunza kuwa, there is no perfect time in life, just take the time and make it perfect. Pengine ningerudi home kwa bimkubwa nisingekuwa hapa leo, hata kusaidia mafundi na kusomba ,aji ningeona aibu, ila kuwa mbali na home kumenifanya nifungue milango mingi sana. Bado sijafika ila angalau leo nafurahia maamuzi niliyoyafanya miezi 11 iliyopita (kurudi kwa uncle). Marafiki zangu wananiona mimi bahili sana ila hawajui kuwa najinyima ili niweke misingi ya kesho vizuri (najinyima vyote ila sio msosi, nakula vizuri na nakula ninachotaka coz kupika is cheap).
KWA WANANGU WOTE TUNAOHASO:
Aiseee, najua baadhi mtakuwa mnapitia kipindi kigumu sana now, pengine matamanio nia makubwa kuliko uhalisia..Nataka niwaambie kuwa this is temporary, yana mwisho ila tu tusikate tamaa..Hiyo 2000 ambayo unaiona ndogo na kuunga bundle mara kibao kwa week bila mpangilio ukiamua kuitunza mara 50 itakuwa ni laki moja ambayo unalipia kodi miezi 3 (mikoani unapata room kali sana)...Tuzidi kupambana, tuzidi kuweka akiba...no one knows tommorow, pengine after 1 year ukawa mbele ya wengi waliokutangulia...Kuna mwanangu aliwahi kupata getto mda mrefu kabla yangu (bahati mbaya namfundisha ubahili positive hanielewi), leo akiliona getto langu analitamani na kujiona kuwa amechelewa kuweka malengo ikizingatia ana kipato kikubwa kuliko mimi. Huwezi amini leo anaomba kutumia getto langu kuvutia mademu wakati analo lake hahahaahahahha namimi simpi hata siku 1..By the way, naishi vyema na washikaji zangu, tunasapotiana sana ila kitu kimoja tu ambacho nawenyewe wanakijua kutoka kwangu, nishawambia sitakuja kumpa mtu yeyote getto langu alale na pisi kali..Hii ni sheria nimeiweka inayoapply kwa wote na wanaelewa..Pengine ni roho mbaya ila kwangu mimi getto langu ndio nyumba yangu, pale kitandani ndipo napumzisha akili yangu inayowaza jinsi gani nitatoboa katika maisha, so naheshimu kwangu zaidi ya ninavyojiheshimu...
All the best wakuu, wakati wa Mungu ni wakati sahihi ila tusiache kuuforce kila wakati kuufanya uwe sahihi ili Mungu aupe kibali chake....!!!!..Huu uzi ulinifanya nijiunge rasmi JF mwezi wa 7 na leo nimeleta ushuhuda kwenu..I'm so grateful to the writer of this thread....This is a testimony from the invisible reader of the thread.
FOHADI: Focus Hardwork Discpline
Pia nafurah kuona shuhuda kama hzi kweny huu uzi.. hatumuachi mtu nyuma lazma wana wote tusepe hom.....
Kama ungeweza elezea hyo formula ya commerce hata kwa ufupi..huenda ikasaidia na wengne..mana issue sio unapata sh ngap.. issue unatumia sh ngapi..
Big up sana mdau...[emoji119]