Kufupisha story ni kwamba gari ile niliifanya uber kipindi hicho ndo uber imeanza hope nilizisha mapambano kwani nlikuwa nahakikisha nalaza laki kila siku ya mungu na wife wakati yupo na ujauzito mkubwa akaajiri mtu wa kusambaza vitu vyake kwa wateja huku na mimi nikisambaza vyangu kwa gari huku wakati mwengne nikimsambazia na yeye,mwisho wa siku nilifungua duka ambalo wife baada a kujifungua akawa ndo msimamizi na pia deni la mzee la 20k kila siku nililitimiza na mwisho wa siku gari ikawa yetu,nakumbuka siku ya harusi babamkwe akatupa kiwanja kwa ksema altupa mtihani wa kujinunulia wenyewe means ile hela tulokuwa tunampa kila siku aliitu za na kutununulia zawadi ya kiwanja huk nasi tukiwa na vingine vitatu hiyo ndo story yangu ya geto ambayo imenipa mke na nyumba ambayo naimalizia now,watoto wangu mapacha,pamoja na gari 3,maduka na biashara nyingine na kunifanya nisahau kuajiriwa japo nna degree yangu ya first class