Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Tulipanga chumba baada ya kupigwa exile na jamaa yangu usiku nikawa maeneo ya geto kama saa 7 usiku hapo tulishapanga na jamaa saa 8 nane anamtoa demu wake basi saa 7 ile sungu sungu wakanisomba aseeh nilizunguka nao mpaka saa kumi na moja wakanipelekwa kwa mwenyekit wa mtaa nilitoka pale saa moja asubuh . Siku ile ile nikatafuta dalali nikajisemea liwalo na liwe
Tokea nipange chumba mm ilikuwa hata likizo siend home natulia geto na hii ndo ilikuwa kimoja mpaka leo nyumban naenda kusalimia tu washukuriwe sungu sungu popote walipo
 
Sure mkuu, mtoto wa kiume ukikaa tu home akili inaalala, hainyumbuki kabisa, m nilipo Anza kukaa ghetto ndo nikakutana na changamoto za Maisha ikabidi niongeze ufanisi wa kazi ninayoifanya
At least now I can work and earn money easily.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
Sana Sana kakaka,akir inasave mazingila
 
Duuhhh Kazi kweli kweli.

Binafsi nimebaini Sisi weusi (waafrika) hatutaweza kuendelea kwa haraka na kuufukuza umasikini. Kila anaepanga anasema alipanga ili ipate akili ya maisha. Haya mmepata akili ya maisha mbona umasikini ungali umetamalaki?

Zamani katika baadhi ya jamii (mfano wasukuma) ulikuwa unaoa ukiwa nyumbani kisha unakaa nyumbani. Baada ya muda kupita unaruhusiwa kwenda kujitegemea. Hii nimeioana kwa wahindi na waarabu pia.

Familia inahitaji kushikamana na kuwa na upendo ili kutusua lakini kwa ngozi nyeusi maisha ni mapambano. Unapambana na Baba au mama utafika wapi zaidi ya kuangukia Pua. Tuzienzi mila zetu kwa kufanya utambuzi wa kubaini zilikuwa na tija ipi katika ustawi na maendeleo kwa ukoo na jamii
Kijana wa kileo kwa Afrika kwetu, ni we mwenyewe kupambana ukingoja ndg wakusaidue utaumia sana, pambana ww km ww
 
Kasebule kanakosa makochi ili kapendeze, nipeni fundi makini aka mtaalamu bei poa niweke sofa hapo
IMG_0308.jpg
 
Nilianza kukaa geto sina hata shuka la kujifunika, kile chumba kilikua ndo kimemaliza kukarabatiwa kukawa na ubao flani hivi umeachwa ndani, ndo nikawa nalalia ule ubao ili nisiumie na baridi kali ya sakafu, ubao wenyewe ulikua ni mfupi Sana ilinibidi nijikunje hadi magoti yaguse kifua ndo unitoshe... Sikua na namna niliishi hivyo hivyo had Mungu aliponifungulia kdogo katika rehma zake
 
mwenzenu nlikua gheto, biashara yangu ikabuma....nkakosa pesa ya kodi ...leo hii tarehe 14.06.2019 nmepiga kitu inaitwa U-turn

haya maisha sjui sie wengine tumeyakosea nn
Pole mkuu Mungu atakujalia rehema zake utasimama tena, amini wewe sio wakwanza kudondoka mimi nilichoma laki 750 kwenye kuku na juice mkuu hiyo nilidunduliza tmiaka 3 ya chuo na biashara yangu ya kwanza ndo ikala mweleka...

ulikuw unafanya biashara gani na upo mkoa gani mkuu??
 
Back
Top Bottom