Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Kwanza nikupe pole.

Unasema wachuchu walikuwa wanalielewa ghetto lako maana yake ulikuwa unawabadilisha jinsi utakavyo.

Ulilifanya ghetto lako kama ulimbo wa wachuchu, nina wasiwasi labda walikuchoresha kwa wana uibiwe kama kulipa kisasi kwasababu uliwatumia na kuwatosa.

Au hao waliokuibia ni miongoni mwa wapenz wa wachuchu uliokuwa ukiwaleta kwako.

Ushauri wangu,sasa hivi angalia maisha yako na usiwe mwepesi kutafuta mtu au kuleta mtu kwako na kujua unaishije.

Ikibidi hama huo mtaa wasije wakakurudia tena maana wameshakujua nyendo zako. Pole sana hili nilishawahi kulisema huko juu kwamba kuibiwa kunarudisha maendeleo nyuma.
Halafu sikuwahi kulifikiria hili mkuu umeongea pointi muhimu sana

Na hata hivyo nina mpango wa kuhama sema natafuta kodi ya miaza 3 kabisa na udalali maana kuhama napo inabidi ujipange

Yaani mimi mwizi siwezi muonea huruma kwakweli na siku nikiona anapigwa lazima niliunge
 
Umenifurahisha uliposema unasali sana. Ibada ni nzuri inakuondolea msongo wa mawazo na kutokujihusisha kwenye vikundi viovu.

Weka malengo usitumie pesa katika vitu ambavyo hujavipangilia au haviko kwenye malengo yako.Achana na anasa kabisa.

Hakikisha kila pesa unayoitoa kufanya manunuzi au matumizi yako unaiandika kwenye daftari ili utunze kumbukumbu vizuri.

Kabla hujatoka nyumbani, weka kumbukumbu vizuri umeondoka na kiasi gani cha pesa ili ukirudi ujue umepata shilingi ngapi na umetumia kiasi gani.

Jambo la muhimu la kuzingatia. Ukishaanza kupata pesa majukumu yanaanza kukusogelea, jipe majukumu unayoyamudu ambayo yako juu yako achana nayo.

Uwe na kiasi kwenye kutoa misaada, jiulize unayemsaidia, siku ukianguka atakuinua?Jiangalie wewe kwanza wengine baadaye.

Jiepushe na mapenzi, labda kama umri umeshaenda, kumuhudumia mtu,au mimba na kuoa huku hujajipanga inaweza kukuharibia malengo.

Ukiona kipato chako kimeongezeka ongeza kiwango cha elimu kwa fani uipendayo,hii itakupa kujiamini na kuwa na maarifa zaidi. Ni vizuri kusoma ukiwa bado hujakuwa na majukumu mengi.

Usishindane na mtu kwenye vitu vya anasa bali katika maendeleo, na usiwachukie waliofanikiwa na wanaofanikiwa bali jifunze wamefanikiwaje ikiwa wewe bado.

Ni hayo tu machache kwa leo.

Ahsanteni.

Ahsante kiongozi
 
Karibu sana mkuu. Mwanzilishi wa huu uzi tumpe big up maana unasaidia vijana wengi kupata upenyo wa kuanza maisha.

Siku nikipata muda mzuri nitaweka kisa changu jinsi nilivyoanza life na wenzangu mpaka nilipofikia.
Thanks mkuu [emoji119], siku ukitulia tusimulie kisa chako
 
Alienzisha huu Uzi ajengewe sanamu posta na apewe tuzo ameinspaire vijana wengi Sana, Kuna wengine tunasoma tu atucoment kitu, tupo wengi Sana naamini kupitia huu uzi tumepiga hatua moja,mbili tatu
Asante kwa feedback mkuu,,Hilo sanamu napendekeza liwe pale ferry [emoji23]
 
Ghetto ninaloishi lina mkeka,ndoo ya maji na mifuko yangu ya nguo..napambana nafanya biashara ya kutembeza bidhaa za urembo.wiki hii mambo ni mazuri jumatatu mauzo yalikuwa 37,000 leo 26,000 napambana kutafuta hela pia nasali sana ili mwaka 2023 nije kuwa na ghetto zuri lenye vitu vizuri ndani..

Matumizi yangu hayafiki 5000 kwa siku na mara nyingi ni chini ya 4000 hela ya kula naitoa kwenye biashara hii hii ambayo niliianza jumatano iliyopita hadi jumapili nilipumzika niweza kusave 63,000 hadi leo na nimeshatoa hela ya kwenda kuongeza vitu kesho kariakoo..

Lengo langu niongeze biashara ya pembeni ili inigharamie bill zangu za kila siku.Lengo langu la mwaka ujao niwe na ghetto zuri lenye vitu vizuri ndani vilevile ninunue bodaboda hata ya mtumba iniingizie pesa na vilevile niwekeze kwenye kilimo kama sitafanikiwa katika yote hayo matatu basi at least hayo malengo mawili yatimie.

Uzi huu umenigusa sana hadi nmeamua kuishi mwenyewe kwangu kiukweli sijawahi kuandika post ndefu kuliko hii hapa JF ila kwa hisani ya uzi huu nimeshare jambo langu smartphone yenyewe ninayotumia ni majanga panapo majaaliwa nitaleta mrejesho wa maendeleo ya biashara na picha ghetto langu kwa sasa..

Roger that!
Kila lakheri mkuu,Simamia hapo hapo,see you next time
 
Umenifurahisha uliposema unasali sana. Ibada ni nzuri inakuondolea msongo wa mawazo na kutokujihusisha kwenye vikundi viovu.

Weka malengo usitumie pesa katika vitu ambavyo hujavipangilia au haviko kwenye malengo yako.Achana na anasa kabisa.

Hakikisha kila pesa unayoitoa kufanya manunuzi au matumizi yako unaiandika kwenye daftari ili utunze kumbukumbu vizuri.

Kabla hujatoka nyumbani, weka kumbukumbu vizuri umeondoka na kiasi gani cha pesa ili ukirudi ujue umepata shilingi ngapi na umetumia kiasi gani.

Jambo la muhimu la kuzingatia. Ukishaanza kupata pesa majukumu yanaanza kukusogelea, jipe majukumu unayoyamudu ambayo yako juu yako achana nayo.

Uwe na kiasi kwenye kutoa misaada, jiulize unayemsaidia, siku ukianguka atakuinua?Jiangalie wewe kwanza wengine baadaye.

Jiepushe na mapenzi, labda kama umri umeshaenda, kumuhudumia mtu,au mimba na kuoa huku hujajipanga inaweza kukuharibia malengo.

Ukiona kipato chako kimeongezeka ongeza kiwango cha elimu kwa fani uipendayo,hii itakupa kujiamini na kuwa na maarifa zaidi. Ni vizuri kusoma ukiwa bado hujakuwa na majukumu mengi.

Usishindane na mtu kwenye vitu vya anasa bali katika maendeleo, na usiwachukie waliofanikiwa na wanaofanikiwa bali jifunze wamefanikiwaje ikiwa wewe bado.

Ni hayo tu machache kwa leo.

Ahsanteni.
Hakika ushauri huu hautakiwi kupuuzwa kwa mtu yeyote.
 
Daah mi waizi wamenirudisha nyuma wameniibia kila kitu ndani hapa nilipo ndio naanza moja tuombeane wakuu [emoji120]

Nikikumbuka nilijinyima kazi zenyewe ni hizi za kungaunga ghetto wachuchu walikuwa wanalielewa sana ukimleta mtoto anakuganda kila saa text uko wapi nije leo hii imebaki story

Mda mwengine nafikiria nitafute mganga wacha nitoboke nimuue mwizi wangu
[emoji23] pole mkuu,vtu vinatafutwa,achana na waganga
 
Umenifurahisha uliposema unasali sana. Ibada ni nzuri inakuondolea msongo wa mawazo na kutokujihusisha kwenye vikundi viovu.

Weka malengo usitumie pesa katika vitu ambavyo hujavipangilia au haviko kwenye malengo yako.Achana na anasa kabisa.

Hakikisha kila pesa unayoitoa kufanya manunuzi au matumizi yako unaiandika kwenye daftari ili utunze kumbukumbu vizuri.

Kabla hujatoka nyumbani, weka kumbukumbu vizuri umeondoka na kiasi gani cha pesa ili ukirudi ujue umepata shilingi ngapi na umetumia kiasi gani.

Jambo la muhimu la kuzingatia. Ukishaanza kupata pesa majukumu yanaanza kukusogelea, jipe majukumu unayoyamudu ambayo yako juu yako achana nayo.

Uwe na kiasi kwenye kutoa misaada, jiulize unayemsaidia, siku ukianguka atakuinua?Jiangalie wewe kwanza wengine baadaye.

Jiepushe na mapenzi, labda kama umri umeshaenda, kumuhudumia mtu,au mimba na kuoa huku hujajipanga inaweza kukuharibia malengo.

Ukiona kipato chako kimeongezeka ongeza kiwango cha elimu kwa fani uipendayo,hii itakupa kujiamini na kuwa na maarifa zaidi. Ni vizuri kusoma ukiwa bado hujakuwa na majukumu mengi.

Usishindane na mtu kwenye vitu vya anasa bali katika maendeleo, na usiwachukie waliofanikiwa na wanaofanikiwa bali jifunze wamefanikiwaje ikiwa wewe bado.

Ni hayo tu machache kwa leo.

Ahsanteni.
Asante sana mkuu
 
Halafu sikuwahi kulifikiria hili mkuu umeongea pointi muhimu sana

Na hata hivyo nina mpango wa kuhama sema natafuta kodi ya miaza 3 kabisa na udalali maana kuhama napo inabidi ujipange

Yaani mimi mwizi siwezi muonea huruma kwakweli na siku nikiona anapigwa lazima niliunge
Pamoja sana.Yalishanitokea haya ndio maana natoa experience ya maisha yangu ya huko nyuma.

Siku ukianza kutafuta nyumba fanya kimya kimya wasijue na siku unaondoka aga siku hiyo hiyo na usitoe location wapi unaenda, futa watu wote waliokujua hapo awali, hii itakupa ujasiri kwamba hakuna anayejua nyendo zako wala kukufuatilia mkuu.
 
Thanks mkuu [emoji119], siku ukitulia tusimulie kisa chako
Nitasimulia mkuu. Ngoja nipunguze majukumu niwe nina muda wa kutosha ili nikianza ni moja kwa moja bila kustop ili nisiwaweke watu alosto. [emoji4][emoji4]
 
Back
Top Bottom